Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mgomo wa Kariakoo umeibua mengi, lakini pamoja na kuonyesha madudu ya uncontrollable TRA na rushwa za nje nje zilizoishinda serikali kuzikabili, mgomo umeibua jambo serious la utendaji chini ya kiwango wa mawaziri wa Fedha na Mipango, pamoja na yule wa Biashara na Viwanda.
Wiazara hizi lazima zifanyekazi kwa pamoja, au kwa kiingereza, in tandem. Weledi na experience ya kiutendaji inatia mashaka. Mgomo wa Kariakoo umeonyesha hawa mawaziri ni mzigo kiuchumi. Hawajui kiuhalisia nini kinaendelea katika wizara zao na kwa wadau kwa ujumla.
Matamshi yao bungeni yameonyesha hawajui nini kinaendelea kwenye sekta zao. Mama Samia tunamshauri kuwa na mtu kuwa Dr wa PhD, ana umri mdogo, ujue hapo experience ni kile tu alichosoma na hana uxoefu wa ingalau hata miaka 10-15 kazini.
Tulikuwa na maProfesa kama Dr Ndulu waliofanya kazi miaka zaidi ya 30 kwenye sekta za Uchumi. Watu wa aina hiyo tunao. Si vema kuuweka uchumi wetu rehani kwa wasomi wachanga wasio na uzoefu wa aina yoyote.
Mwigulu Nchemba na Ashatu Kijaji wapelekwe vyuoni wakaendelee kufundisha tu kile walichosoma.
Kuongoza uchumi kitu ingine.