Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mawakala hao wamekuwa wakikusanya kodi kutoka kwa Wananchi na wamekuwa wakiziwasilisha kusikotakiwa kwa mujibu wa sheria. Ni vyema ifahamike kuwa kodi. Ifahamike kuwa yoyote anayekusanya sio yeye anayewajibika kuilipa hiyo kodi hivyo anapotumia hivyo anapoitumia anaiibia serikali.
Wafanyabiashara hawa wenye wajibu wa uwakala wanapoamua makusudi kwenda kinyume na utaratibu wa sheria na kwakuwa wanafanya hivyo, wanazitumia kodi za walipakodi hawa wa kawaida ambao walishalipa fedha hiyo kwa ajili ya kwenda serikalini na kuleta maendeleo katika nchi yetu. Hii sio fedha binafsi ya biashara zao. Na hatimaye wanaonekana kuwa ndiyo matajiri kumbe wametumia fedha za watanzania wenzao.
Mawakala hawa wanaofanya hivyo wanaihujumu Serikali, wanaihujumu nchi na wanahujumu jitihada za Rais Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo.
Natoa rai kwa Mawakala hao, iwe ni Taasisi Binafsi, Taasisi za Serikali wakiwemo wale waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Kodi ya zuio, au ushuru wa bidhaa kuacha mara moja tabia hiyo ya kuzuia kodi zilizokusanywa kwa wengine na kuzitumia wao wenyewe badala ya kuziwasilisha serikalini.
Pia nawaelekeza TRA kuchukua hatua kali za kisheria kwa Mawakala wowotw watakaojikopesha fedha zilizotakiwa ziende serikalini kwa kutumia kigeo cha kuwa mawakala wa kukusanya kuchukua pesa za serikali
PIA SOMA
- LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma