Mwigulu Nchemba: Serikali kununua matrekta 10,000

Hapo hakuna tija itapatikana, Serkali haijawahi kusimamia jambo likafanikiwa vizuri, Mfano ni Waziri wa Kilimo aliyepita Bashe alikuwa na mipango mingi ya kuanzisha maeneo ya kilimo na kuwapa wahitimu vijana mashamba ya kilimo na hakufanikiwa kwa lolote na mabilioni ya shilingi yamepotea. Wakitaka kufanikiwa Mkulima apewe uhuru wa kujiendesha, kama matreka Mkulima akopeshe wa riba nafuu.

Pia serkali isitoe hela kwa watu hasa wanafunzi wanaomaliza vyuo kwenda kuanzisha kilimo maana wengi wao hawana uzoefu na huishia kukimbia na kutelekeza mashamba.

Serkali itoe elimu na mitaji kwa watu ambao tayari wanauzoefu na wanaujuzi wa kilimo kwa muda ili kuepuka kupoteza fedha nyingi kwa watu wababaishaji.

Kwa maana hiyo jambo hili la kununua matraki ni jema ila sidhani kama litafanikisha kwa lolote kwenye sekta ya kilimo na hofu yangu kubwa ni wakulima kufikiwa na matrekta hayo moja kwa moja badala ya kuwa chini ya madalali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…