Mwigulu Nchemba: Tutaanza kutumia VAR msimu ujao ili kupunguza matukio yenye utata

Mwigulu Nchemba: Tutaanza kutumia VAR msimu ujao ili kupunguza matukio yenye utata

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Amayesema hayo wakati Akisoma Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024


===

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amependekeza kutoa msamaha kwenye uingizaji wa mashine za ‘’VAR’’ na vifaa vyake kwa ufafanuzi utakaotolewa hapo baadaye akisema uamuzi huo utasaidia kuwa na ‘’VAR’’ za kutosha katika viwanja vyote Tanzania.

Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni Jijini Dodoma leo June 13,2024, Waziri Mwigulu amesema yafuatayo “Kuhusu ubora wa eneo la kuchezea, yaani pitch kwenye viwanja mbalimbali, tayari Serikali ilitunga sheria inayotoa msamaha kwenye uingizaji wa nyasi bandia na vifaa vyake”

“Msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania tutaanza kutumia ‘’VAR’’ ili kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki maana kuna timu zimezidi msimu mmoja penati 10, halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa”

PIA SOMA

- Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma

- Wallace Karia: Msimu huu hakutakuwa na matumizi VAR Ligi Kuu
 
Safi sana na nadhani tutakuwa nchi ya kwanza afrika Niko tayari kukoselewa
 
Mwigulu tutazame Kwa jicho la upendeleo sisi wanywaji wa bia. Hebu punguzeni Kodi watu tuburudike ili tusikumbuke hata mabaya yenu huko serikalini
 
Waziri wa fedha yupo bize na var, ila ndo watz wanavyotuchukulia, ukitaka wasihoji mambo ya maana kama deni la taifa unawachomekea mambo ya var kidogo
 
Waziri wa fedha yupo bize na var, ila ndo watz wanavyotuchukulia, ukitaka wasihoji mambo ya maana kama deni la taifa unawachomekea mambo ya var kidogo
Tunaitaka hiyo VAR kwa udi na uvumba ili tuheshimiane
 
Back
Top Bottom