We mzee ushaambiwa tuweke mkeka world cup - Ufaransa vs Angentina - bingwa ni Angetina, tuweke Trilioni 60, baada ya mechi tuibuke na Trilioni 180 tulipe madeni yoote na chenji tukanunue umeme.
Ndio yanayoitesa Nchi hayo na mengi yamekopwa kipindi Cha Jiwe yaani ndani ya Miaka 5 yanaiva na riba kubwa .
Sekta binafsiMbona wamekopa Trilioni 20 ndani ya miezi sita?.
Yaani ulikopa kwa riba ya asilimia 20. Unanunua mkopo huo na utalipa mkopo huo kwa riba ya asilimia 2. Mheshimiwa wetu sana anamaanisha maelezo haya??“Tumeshafanya majaribio hata kutaka tupate fedha zenye masharti nafuu tununue madeni ya nyuma ambayo yaliwahi kukopwa commercial [kukopwa kwa masharti ya kibiashara] tuyapeleke kwenye masharti nafuu, [..] ili tuwape Watanzania unafuu.”
-Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba