Mwigulu: Nchi yetu inao vibaraka wengi. Inafanyika michezo ya kulipia baadhi ya watu wafanye vitendo vya kihalifu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu

Waziri mkuu Mwigulu Nchemba akiwa mkoani Iringa anasema:

Ujasusi wa dunia hii, ameufuatilia kwa miaka mingi sana. Anaijua michezo mingi.

"Najua haya yaliyotokea Ghana, najua yaliyotokea Congo, najua yaliyotokea Angola, na... najua maeneo mengi yaliyowahi kutokea. Tanzania si alikuwa kiongozi wa Liberation Movement? Alikuwa kiongozi wa masuala ya ukombozi wa bara la Afrika.

Nayajua, naijua michezo hiyo. Na hata michezo ya kisasa iliyofanyika katika baadhi ya nchi naijua. Ambayo hiyo hatujasimuliwa, tumeona.

Inafanyikaga michezo hii ya kulipia baadhi ya watu wafanye vitendo vya kihalifu katika nchi husika, lakini kwa malengo na sababu zitakazotajwa tofauti na zile zilizokusudiwa.

Sababu nyingi inakuwaga rasilimali, lakini zinazotumiwa zinatajwaga zingine. Lazima kila wakati tuwe makini. Na hata nchi yetu inao vibaraka, wako wengi tu. Vibaraka wa aina hiyo wapo wengi na wako kazini.

Na maisha yao wanaendesha kwa kulipwa hivyo hivyo. Wakati ninyi mnavuja jasho kutafuta kipato halali cha maisha yenu na kuiendeleza nchi, lakini wapo vibaraka ambao wao maisha yao yanatunzwa, na kazi maalum wanazofanya ni hizi za kuharibu amani katika nchi.

Wapo, na hata tunavyoongea hivi wapo, wako kazini. Familia zao zinatunzwa kwa kufanya kazi hizo hizo za ukibaraka. Na wengine hupenya mpaka na kwenye mifumo, wanapenya.

Kila siku yuko kazini, unaweza ukadhani anafanya kazi ya taifa, kumbe ni kibaraka anatumika."
​

Kamateni wote sasa..kama mkitaka kuongeza nguvu undeni SPECIAL FORCE RETIRED COMMANDOS wafanye hyo kazi ya kuwakamata..Sisi wananchi tunataka tusiishi kwa hofu..Mnasema kumetulia lakini leo tunaona hili kesho lile mnatutia wasiwasi...
 
Wakuu

Waziri mkuu Mwigulu Nchemba akiwa mkoani Iringa anasema:

Ujasusi wa dunia hii, ameufuatilia kwa miaka mingi sana. Anaijua michezo mingi.

"Najua haya yaliyotokea Ghana, najua yaliyotokea Congo, najua yaliyotokea Angola, na... najua maeneo mengi yaliyowahi kutokea. Tanzania si alikuwa kiongozi wa Liberation Movement? Alikuwa kiongozi wa masuala ya ukombozi wa bara la Afrika.

Nayajua, naijua michezo hiyo. Na hata michezo ya kisasa iliyofanyika katika baadhi ya nchi naijua. Ambayo hiyo hatujasimuliwa, tumeona.

Inafanyikaga michezo hii ya kulipia baadhi ya watu wafanye vitendo vya kihalifu katika nchi husika, lakini kwa malengo na sababu zitakazotajwa tofauti na zile zilizokusudiwa.

Sababu nyingi inakuwaga rasilimali, lakini zinazotumiwa zinatajwaga zingine. Lazima kila wakati tuwe makini. Na hata nchi yetu inao vibaraka, wako wengi tu. Vibaraka wa aina hiyo wapo wengi na wako kazini.

Na maisha yao wanaendesha kwa kulipwa hivyo hivyo. Wakati ninyi mnavuja jasho kutafuta kipato halali cha maisha yenu na kuiendeleza nchi, lakini wapo vibaraka ambao wao maisha yao yanatunzwa, na kazi maalum wanazofanya ni hizi za kuharibu amani katika nchi.

Wapo, na hata tunavyoongea hivi wapo, wako kazini. Familia zao zinatunzwa kwa kufanya kazi hizo hizo za ukibaraka. Na wengine hupenya mpaka na kwenye mifumo, wanapenya.

Kila siku yuko kazini, unaweza ukadhani anafanya kazi ya taifa, kumbe ni kibaraka anatumika."
​
Mwigulu naye Jasusi? Si bora Yericko!
 
Muda huongea...
Mfano ni kama yule mwana ccm aliyenena kuhusu Chadema kwamba ishughulikiwe...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom