Mwigulu ni Daktari wa Uchumi, Inakuaje tatizo la ajira kwa vijana linamtoa jasho? Inakuwaje ugumu wa maisha mtaani unamtoa jasho?

Mwigulu ni Daktari wa Uchumi, Inakuaje tatizo la ajira kwa vijana linamtoa jasho? Inakuwaje ugumu wa maisha mtaani unamtoa jasho?

system hacker

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2022
Posts
426
Reaction score
709
Waziri wa Fedha Dr. Mwigulu Nchemba ni moja wa MaDr wakubwa wa uchumi tulio nao hapa nchini. Tunajivunia.

Bahati nzuri kwake yupo kabisa kwenye 'core system' yaani ni policy maker mwenyewe hivyo hana cha kusingizia.

Je, kwa uwezo wake wa kitaaluma kwenye masuala ya kiuchumi, imekuaje anashindwa kupiga kata funua tatizo dogo la ajira kwa vijana?

Au ndio hivyo tena darasani fresh lakini field ngumu?

Dr. Nchemba prove haters wrong!

Naomba nimpe heko Mh. Hussein Bashe kwa misimamo yake kuhusu mazao ya kilimo. Nakukubali sana, na watanzania wote tupo nyuma yako.

Reference:

Dr Jakaya Kikwete alikuwa mchumi wa kawaida tu lakini alimwaga ajira hadi zikamwagika.

Akaona haitoshi akawamwagia hadi wenye vyeti feki.

Akaona haitoshi ufisadi ukapigwa nje ndani laki sio pesa ilikuwa ni awamu yake.

Dr. Mwigulu unakwama wapi?

Hello Mh. Dr. JK pls mpe desa Mama na Mwigulu.
 
Atakwambia yeye sio Rais kama alivyokua JK
 
Mbona wewe linakushinda unamlilia Dr Mwigullu Nchemba PhD?
Mimi sio Taifa. Mimi ni individual a victim of sera mbovu za uchumi za kitaifa.

Siwezi kuishi nje ya mfumo wa sera za kiuchumi za kitaifa. Sera zikiwa mbovu hata matajiri wakubwa hukimbia ama hukwama sembuse mimi!

Anyway, sidhani kama una uelewa wowote wa masuala ya fedha na uchumi. Sidhani.

Na hapo tatizo lilipojikita zaidi kwa watu wengi.
 
Suala la ajira halijawahi kuwa kipengele muhimu kinachozingatiwa katika ukuaji au kuanguka kwa uchumi wa nchi hii. Ndiyo maana hata ajira unazoziongelea ni zile za serikalini wakati wote tunajua watanzania wengi wako nje ya mfumo wa ajira za serikali lakini hawatoagi taarifa zozote kuangalia hali ya ajira nje ya hizo za serikali.
 
Suala la ajira ni maamuzi ya watawala serikali aishindwi kuajiri wameamua tu kuwakomesha vijana wachakae na wadhalaulike mitaani, wawe wezi, wawe mashoga, wawe makahaba
 
Tunabana ili tuweze kurejesha mikopo na kupambana na hii kitu inaitwa debt stress, kwa hiyo tarajia hali ngumu zaidi kwa wadanganyika.
 
Tangu nijitambue sijawahi kuona serikali iliyopo madarakani kwa nchi ya Tanzania ikisifiwa. Huyo JK unayemsifia ndo alilaumiwa kiasi kwamba kuna picha ilitoka kwenye gazeti la mwanahalisi ya mtoto mwenye bango lililoandikwa kama kikwete ameshindwa kuongoza ampe yeye aongoze. Tatizo la ajira ni la dunia nzima.. ila kwa hapa Tanzania kuna unafuu. Na hizi juhudi za Bashe kwenye kilimo zitapunguza ukubwa wa tatizo. Serikali haiwezi kuajiri graduates wote. Cha muhimu itengeneze tu mazingira mazuri watu wajiajiri na kuajiriwa na sekta binafsi.
 
Jamani hata sasa hamjamjua Mwigulu. Huyu hata mjumb wa nyumba hamsini hafai. Kwa asili Mwigulu ni mkatili sana aliyefanya Mbunge Rwakatare wa Bukoba Mjini akae Lock up siku 136 kwa tuhuma za ugaidi, vijana wanne wa Chadema kufikishwa Mahakama Kuu kanda ya Tabora kwa tuhuma za ugaidi. Bahati yao Majaji wenye Hekima na Busara zao wakawaondolea tuhuma za ugaidi.
 
Waziri wa fedha anahusikaje na ajira , kuna viwanda na biashara , kilimo , nk ajira zipo nyingi mno shida yetu Tunashindwa kulaumu elimu yetu tunalaumu mtu baki kabisa
 
Back
Top Bottom