Mwigulu: Rais Samia ni nyota wa mchezo ukuaji sekta ya madini

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
IMG-20261010-WA0016.jpg

โ–ช๏ธ๐—”๐˜€๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚๐—ฎ ๐—ณ๐˜‚๐—ฟ๐˜€๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐˜‡๐—ฎ๐˜„๐—ฎ
โ–ช๏ธ๐—ช๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐—ถ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜„๐—ฎ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ๐˜๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ท๐—ถ

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko na ukuaji wa sekta ya madini nchini.

Amesema kwa maelekezo yake, Serikali imefanya mabadiliko makubwa ya sera ambayo yamewezesha wachimbaji na wachenjuaji wazawa wa madini kukua kiuchumi kwa kuwezeshwa kupata mitaji.

โ€œTumeona mchango mkubwa wa wachimbaji wazawa kwenye uchumi wa nchi yetu, tunathamini mchango wa wachimbaji wadogo pamoja na wawekezaji wengine ambao wamechangia kukuza uchumi wa nchi yetu,โ€ amesema

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na kampuni za uwekezaji katika sekta ya dhahabu za Gold World Council, Stone X na kampuni ya kizawa ya Geita Gold Refinery (GGR) inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Mama Sarah Masasi.

IMG-20261010-WA0030.jpg

Amesema dhahabu imeendelea kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kupitia DIRA 2050, Serikali imelenga kubadilisha uchumi na maisha ya Watanzania.

โ€œSerikali imeendelea kufanya mabadiliko katika sekta hii na kufanya maboresho ya kisera ili kukidhi mahitaji ya wachimbaji wadogo na wachenjuaji wa madini jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kupitia sekta hii. Tunatamani kuiona sekta hiyo ikiendelea kukua,โ€ amesema.

Pia, Waziri Mkuu amesifu ushirikiano wa kiuwekezaji uliopo baina ya wachimbaji na wachenjuaji wa dhahabu nchini ambao umeendelea kuongeza ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema sekta ya madini imeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na sasa inachangia asilimia 10 katika pato la Taifa.

IMG-20261010-WA0034.jpg

โ€œDhahabu imekuwa bidhaa adimu katika soko la fedha la kimataifa na inachangia zaidi ya asilimi 53 ya pato la fedha za kigeni na imekuwa bidhaa imara katika kukuza uchumi wetu, Tanzania tunazalisha zaidi ya tani 65 za dhahabu na mchango wa wachimbaji wadogo ni karibu aslimia 40,โ€ alisema.

Alisema kwamba Serikali sasa inatekeleza Sera ya Uchimbaji inayosema โ€œMadini kwa kesho iliyoboraโ€ yenye lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana, na sasa Serikali inafuta vibali ambavyo havijaendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo.

Naye, Mmiliki wa Kampuni ya Uchenjuaji ya GGR, Mama Sarah Masasi aliishukuru Serikali kwa kutoa fursa kwa wachimbaji wazawa kushirikiana na wawekezaji kutoka nje, jambo ambalo limechangia kuongeza mitaji na uwekezaji katika sekta ya madini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Stone X, Bw. Jonathan Kay alisema Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanya kazi ya kuipandisha thamani dhahabu ya Tanzania na kwa kushirikiana na kampuni kama GGR wamefanikiwa kukusanya kiwango kikubwa cha dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania na Benki Kuu ya Uingereza.

โ€œKuwekeza kwa wachimbaji wadogo, kuanzia ngazi ya chini, ya kati na ya juu kumekuwa na manufaa kwa nchi kama Tanzania. Kampuni kubwa sasa zinawaamini wazawa na zinawekeza mitaji mikubwa ili kuwawezesha kuongeza uchimbaji na ufanisi wa uchenjuaji wa dhahabu.โ€

IMG-20261010-WA0026.jpg

Alisema Tanzania sasa imekuwa kitovu cha uchimbaji wa dhahabu safi kazi ambayo inafanywa pia na wazawa. Aidha, aliahidi kuendelea kuongeza ushirikiano na uwekezaji zaidi kwa kampuni za wazawa kwa kuwa sera na sheria za sasa ni rafiki kwa wawekezaji wote.

IMG-20261010-WA0024.jpg
IMG-20261010-WA0032.jpg
IMG-20261010-WA0020.jpg
 
Attachments

  • IMG-20261010-WA0028.jpg
    IMG-20261010-WA0028.jpg
    486.6 KB · Views: 4
  • IMG-20261010-WA0022.jpg
    IMG-20261010-WA0022.jpg
    379.2 KB · Views: 7
๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ: ๐—ฅ๐—”๐—œ๐—ฆ ๐—ฆ๐—”๐— ๐—œ๐—” ๐—ก๐—œ ๐—ก๐—ฌ๐—ข๐—ง๐—” ๐—ช๐—” ๐— ๐—–๐—›๐—˜๐—ญ๐—ข ๐—จ๐—ž๐—จ๐—”๐—๐—œ ๐—ฆ๐—˜๐—ž๐—ง๐—” ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—”๐——๐—œ๐—ก๐—œ

โ–ช๏ธ๐—”๐˜€๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚๐—ฎ ๐—ณ๐˜‚๐—ฟ๐˜€๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐˜‡๐—ฎ๐˜„๐—ฎ
โ–ช๏ธ๐—ช๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐—ถ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜„๐—ฎ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ๐˜๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ท๐—ถ

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko na ukuaji wa sekta ya madini nchini.

Amesema kwa maelekezo yake, Serikali imefanya mabadiliko makubwa ya sera ambayo yamewezesha wachimbaji na wachenjuaji wazawa wa madini kukua kiuchumi kwa kuwezeshwa kupata mitaji.

โ€œTumeona mchango mkubwa wa wachimbaji wazawa kwenye uchumi wa nchi yetu, tunathamini mchango wa wachimbaji wadogo pamoja na wawekezaji wengine ambao wamechangia kukuza uchumi wa nchi yetu,โ€ amesema

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na kampuni za uwekezaji katika sekta ya dhahabu za Gold World Council, Stone X na kampuni ya kizawa ya Geita Gold Refinery (GGR) inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Mama Sarah Masasi.

Amesema dhahabu imeendelea kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kupitia DIRA 2050, Serikali imelenga kubadilisha uchumi na maisha ya Watanzania.

โ€œSerikali imeendelea kufanya mabadiliko katika sekta hii na kufanya maboresho ya kisera ili kukidhi mahitaji ya wachimbaji wadogo na wachenjuaji wa madini jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kupitia sekta hii. Tunatamani kuiona sekta hiyo ikiendelea kukua,โ€ amesema.

Pia, Waziri Mkuu amesifu ushirikiano wa kiuwekezaji uliopo baina ya wachimbaji na wachenjuaji wa dhahabu nchini ambao umeendelea kuongeza ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema sekta ya madini imeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na sasa inachangia asilimia 10 katika pato la Taifa.

โ€œDhahabu imekuwa bidhaa adimu katika soko la fedha la kimataifa na inachangia zaidi ya asilimi 53 ya pato la fedha za kigeni na imekuwa bidhaa imara katika kukuza uchumi wetu, Tanzania tunazalisha zaidi ya tani 65 za dhahabu na mchango wa wachimbaji wadogo ni karibu aslimia 40,โ€ alisema.

Alisema kwamba Serikali sasa inatekeleza Sera ya Uchimbaji inayosema โ€œMadini kwa kesho iliyoboraโ€ yenye lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana, na sasa Serikali inafuta vibali ambavyo havijaendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo.

Naye, Mmiliki wa Kampuni ya Uchenjuaji ya GGR, Mama Sarah Masasi aliishukuru Serikali kwa kutoa fursa kwa wachimbaji wazawa kushirikiana na wawekezaji kutoka nje, jambo ambalo limechangia kuongeza mitaji na uwekezaji katika sekta ya madini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Stone X, Bw. Jonathan Kay alisema Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanya kazi ya kuipandisha thamani dhahabu ya Tanzania na kwa kushirikiana na kampuni kama GGR wamefanikiwa kukusanya kiwango kikubwa cha dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania na Benki Kuu ya Uingereza.

โ€œKuwekeza kwa wachimbaji wadogo, kuanzia ngazi ya chini, ya kati na ya juu kumekuwa na manufaa kwa nchi kama Tanzania. Kampuni kubwa sasa zinawaamini wazawa na zinawekeza mitaji mikubwa ili kuwawezesha kuongeza uchimbaji na ufanisi wa uchenjuaji wa dhahabu.โ€

Alisema Tanzania sasa imekuwa kitovu cha uchimbaji wa dhahabu safi kazi ambayo inafanywa pia na wazawa. Aidha, aliahidi kuendelea kuongeza ushirikiano na uwekezaji zaidi kwa kampuni za wazawa kwa kuwa sera na sheria za sasa ni rafiki kwa wawekezaji wote.
sahihi 100% :KasugaYeah:
 
Anasifia mchango wa wachinbaji wazawa, ili hali hiyo picha ya pamoja inasema tofauti

Huko pori Wachina wanatindua miamba kinoma noma! Haijawahi tokea
 
Wapi hiyo?
Mchina akishaiona mali ni kama ruba, hang'oki.
 
Chawa wa Zanzibar, wajinga waliisha huo upuuzi haufanyi kazi 2026 .

Stay guided.
 
Mchimbaji mdogo hasa dhahabu Tanzania ni mtu wa kutangatanga.......
Hana vifaa wala technology...
Ni mtu anayejaribu kuchimba kwa kubahatisha......
Katika kubahatisha hukohuko, siku atakayofumania mzigo.....katika eneo ambalo wenye technology hawatarajii.
Atapewa saa 24 kuondoka hapo mara moja?
Ataambiwa hilo eneo kapatikana mwekezaji mwenye leseni.
Atafurumushwa kwa mtutu.
Baada ya hapo huyo mwezezaji muhuni ata enclose hilo eneo bila maendelezo.
Shughuli imeishia hapo...
Na hutasikia uwekezaji wowote kwa eneo hilo.
Mchimbaji atabaki mzululaji kwenye nchi yake.
Leo utamsikia yupo Singida, kesho yupo Simiyu, kesho kutwa yupo Biharamulo, mara utamsikia kakimbilia Chunya,
Wiki jana karudi tena Geita.

Huyu mchimbaji akiwa anachimba bila kupata mzigo hakuna mwenye habari naye.....Ila siku akiotea chochote.
Yatatokea mafuriko ya watu eneo hilo ndani ya nusu saa.
Utamuona mkuu wa wilaya kaja.
Mkuu wa mkoa naye kaja.
OCD yupo
Afisa madini kaja.
Mtendaji huyo hapo.
Mavunde yupo njiani.
Ni msururu wa Magari ya gharama....
Lakini source ya utambuzi ni mchimbaji asiye na vifaa wala teknolojia.
Sasa Kwann hao wenye mitaji, vifaa na technology kama wanavyoonekana kwenye picha wameshindwa kujua location ya dhahabu?
 
View attachment 3688095

โ–ช๏ธ๐—”๐˜€๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚๐—ฎ ๐—ณ๐˜‚๐—ฟ๐˜€๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐˜‡๐—ฎ๐˜„๐—ฎ
โ–ช๏ธ๐—ช๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐—ถ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜„๐—ฎ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ๐˜๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ท๐—ถ

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko na ukuaji wa sekta ya madini nchini.

Amesema kwa maelekezo yake, Serikali imefanya mabadiliko makubwa ya sera ambayo yamewezesha wachimbaji na wachenjuaji wazawa wa madini kukua kiuchumi kwa kuwezeshwa kupata mitaji.

โ€œTumeona mchango mkubwa wa wachimbaji wazawa kwenye uchumi wa nchi yetu, tunathamini mchango wa wachimbaji wadogo pamoja na wawekezaji wengine ambao wamechangia kukuza uchumi wa nchi yetu,โ€ amesema

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na kampuni za uwekezaji katika sekta ya dhahabu za Gold World Council, Stone X na kampuni ya kizawa ya Geita Gold Refinery (GGR) inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Mama Sarah Masasi.

View attachment 3688096

Amesema dhahabu imeendelea kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kupitia DIRA 2050, Serikali imelenga kubadilisha uchumi na maisha ya Watanzania.

โ€œSerikali imeendelea kufanya mabadiliko katika sekta hii na kufanya maboresho ya kisera ili kukidhi mahitaji ya wachimbaji wadogo na wachenjuaji wa madini jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kupitia sekta hii. Tunatamani kuiona sekta hiyo ikiendelea kukua,โ€ amesema.

Pia, Waziri Mkuu amesifu ushirikiano wa kiuwekezaji uliopo baina ya wachimbaji na wachenjuaji wa dhahabu nchini ambao umeendelea kuongeza ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema sekta ya madini imeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na sasa inachangia asilimia 10 katika pato la Taifa.

View attachment 3688097

โ€œDhahabu imekuwa bidhaa adimu katika soko la fedha la kimataifa na inachangia zaidi ya asilimi 53 ya pato la fedha za kigeni na imekuwa bidhaa imara katika kukuza uchumi wetu, Tanzania tunazalisha zaidi ya tani 65 za dhahabu na mchango wa wachimbaji wadogo ni karibu aslimia 40,โ€ alisema.

Alisema kwamba Serikali sasa inatekeleza Sera ya Uchimbaji inayosema โ€œMadini kwa kesho iliyoboraโ€ yenye lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana, na sasa Serikali inafuta vibali ambavyo havijaendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo.

Naye, Mmiliki wa Kampuni ya Uchenjuaji ya GGR, Mama Sarah Masasi aliishukuru Serikali kwa kutoa fursa kwa wachimbaji wazawa kushirikiana na wawekezaji kutoka nje, jambo ambalo limechangia kuongeza mitaji na uwekezaji katika sekta ya madini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Stone X, Bw. Jonathan Kay alisema Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanya kazi ya kuipandisha thamani dhahabu ya Tanzania na kwa kushirikiana na kampuni kama GGR wamefanikiwa kukusanya kiwango kikubwa cha dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania na Benki Kuu ya Uingereza.

โ€œKuwekeza kwa wachimbaji wadogo, kuanzia ngazi ya chini, ya kati na ya juu kumekuwa na manufaa kwa nchi kama Tanzania. Kampuni kubwa sasa zinawaamini wazawa na zinawekeza mitaji mikubwa ili kuwawezesha kuongeza uchimbaji na ufanisi wa uchenjuaji wa dhahabu.โ€

View attachment 3688098

Alisema Tanzania sasa imekuwa kitovu cha uchimbaji wa dhahabu safi kazi ambayo inafanywa pia na wazawa. Aidha, aliahidi kuendelea kuongeza ushirikiano na uwekezaji zaidi kwa kampuni za wazawa kwa kuwa sera na sheria za sasa ni rafiki kwa wawekezaji wote.

View attachment 3688099View attachment 3688103View attachment 3688104
Ni aibu mtu anayeitwa dokta au profesa kujigeuza au kugeuzwa chawa.
 
Back
Top Bottom