The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali iko tayari kusonga mbele na inapokea maoni na kuyafanyia kazi, akisisitiza kuwa haitakuwa kikwazo katika juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania.
“La mwisho nimeyapokea niliyoyasikia kwa niaba ya Serikali, na bahati nzuri political will ipo. Mimi nimetumwa kusimamia, kwa hiyo niwahakikishie, kwa heshima ya Tanzania, mara zote tutakuwa nayo. Nimepokea, Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha nchi inakuwa moja na tunasonga mbele,” amesema Dkt. Mwigulu.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo Januari 24, 2026 nyumbani kwa hayati Mzee Edwin Mtei, Tengeru mkoani Arusha, akishiriki mazishi ya aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza baada ya kusikiliza maoni ya Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Bishop Simon Makundi, kuhusu umuhimu wa kutafuta suluhisho la kitaifa pale panapokuwepo tofauti, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imepokea wito huo na ina dhamira ya dhati ya kuutekele