Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema uchumi wa Tanzania unaendelea kukua akibainisha kuwa kasi ya ukuaji wa kitaifa imepaa hadi kufikia 6.0% licha ya mtikisiko uliosababishwa na janga la Uviko-19.
Mwigulu ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma leo, Aprili 1, 2026, wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (2026-2027).
Mwigulu amehusisha maendeleo haya na uwekezaji mkubwa wa kimkakati katika sekta za msingi kama vile nishati, usafirishaji, na huduma za kijamii. Jambo kuu la fahari ni ziada ya umeme (electricity surplus) ambayo haijawahi kutokea nchini, hali inayoiweka Tanzania kama kiongozi wa kikanda katika usalama wa nishati ndani ya Afrika Mashariki na Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).