Mwigulu amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Singida kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho, Novemba 27, 2024.
Akizungumza katika Mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi uliofanyika leo, Novemba 26, 2024, katika Kata ya Puma, Wilaya ya Ikungi, Dkt. Nchemba amewasihi wananchi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu, huku akisisitiza wachague CCM.
"Tufanye uchaguzi wa amani na utulivu. Waambieni vijana wenu wasikubali kushawishiwa au kuchochewa kugombana. Vyama vingi vipo kikatiba kwa ajili ya kukuza demokrasia, siyo kuleta migogoro. Mgombea anayeheshimika na sera bora hatakiwi kutumia fujo kushinda. Umoja wetu na amani yetu ndio msingi wa utaifa wetu,"
PIA SOMA
- LGE2024 - Polisi: Tusiwape nafasi wanaotaka kuvuruga amani ya Uchaguzi wa kesho Novemba 27, 2024