PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Julai 2, 2026, Waziri Mkuu Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na wananchi wa Shirati wilayani Rorya mkoani Mara, ametangaza kuwa serikali inaenda kufuta rasmi sheria ya kutaifisha mifugo katika kikao cha Bunge la mwezi wa Tisa kinachoanza Agosti mwaka huu.
Nchemba alieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya serikali kubaini mapungufu mengi katika sheria hiyo, ikiwemo baadhi ya watu kuitumia kujitofautisha na kujitajirisha kibinafsi kwa kufanya ujanja wa kutaifisha na kuuza makundi ya ng'ombe siku hiyo hiyo asubuhi bila kufuata taratibu za kisheria, jambo ambalo limekuwa likikiuka haki na kuwanyonya wafugaji nchini.