Mwigulu: Wanaosusia vikao vya Bunge wana mpango wa kushusha uchumi wa nchi

Mwigulu: Wanaosusia vikao vya Bunge wana mpango wa kushusha uchumi wa nchi

1734444bfad5bb46afc8da7c9b1a1b74

WAZIRI wa Katiba na sheria, Mwigulu Nchemba amesema kitendo cha baadhi ya Wabunge wa Upinzani kususia vikao vya Bunge kwa kuogopa Corona ni ishara ya kutengeneza madaraja na mpango wa kushusha uchumi wa nchi.

Waziri Nchemba amesema hayo jana Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya wizara ya Viwanda na Biashara ya makadirio na matumizi kwa mwaka wa fedha,2020/2021 ambapo amewataka Watanzania kuacha kusikiliza miluzi ambayo inapotosha taifa.

Waziri Nchemba amesema Maisha ya Watanzania mara nyingi hayana akiba hivyo kitendo cha watanzania kujifungia ndani bila kufanya kazi kwa tahadhari ya Corona kama wanavyoshauri baadhi ya wabunge wa Upinzani panaweza kutengeneza majanga mengine hivyo wanatakiwa kufuata ushauri uliotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuchapa kazi na kuondoa hofu juu ya Corona na kubainisha kuwa janga halikimbiwi.

Waziri Nchemba ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni kuiongoza Wizara ya Katiba na Sheria tukio lililofanyika Mjini Chato mkoani Geita baada ya aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo Dkt. Balozi Augustine Mahiga kufariki Dunia.
Uchumi wa jimbo la N.Mkono na S. Mhongo umeimarika kiasi gani tangu wawe watoro wazuri?
 
Eeh kama yule aliyekamatwa kwa tuhuma ya ujangiri na kumiliki silaha likuki kinyume na sheria
 
Uchumi utaanguka vipi na kuna mbunge munamrejesha bungeni Cecil mwambe akaongeze hoja za nguvu
 
Naye ameshakula shavu atulie sasa,haoni mawaziri wenzake?Ukishabwabwaja ukaonekana na kupewa shavu tulia,porojo waachie akina kibajaji!

Au umesahau ulivyochekwa ulipotumbuliwa mara ya kwanza,tulia ule matunda ya mdomo wako!Ukishupaza sana shingo,siku yakikukuta utapata aibu na kuchekwa sana!

Wewe ni waziri sasa,hebu shughulika na wizara yako!Kupiga domo kunaweza kukawa kumekupa uteuzi,ila kupiga domo hakutakubakisha kwenye nafasi hiyo!Period!
Huyu dogo ameenda shule lakini hayaelimika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom