Mwijaku anusurika kulipa TSh. milioni 500 baada ya Mahakama kufuta kesi ya Masoud Kipanya

Mwijaku anusurika kulipa TSh. milioni 500 baada ya Mahakama kufuta kesi ya Masoud Kipanya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama Kuu ya Tanzania (Masijala Ndogo ya Dar es Salaam) imeondoa kesi ya kashfa ya Ally Masoud Nyomwa maarufu Masoud Kipanya dhidi ya Burton Mwemba 'Mwijaku', kutokana na dosari za usajili.

Mheshimiwa Jaji David Ngunyale aliiondoa kesi hiyo mnamo tarehe 24 Oktoba 2024 kabla hajatoa uamuzi wa mapingamizi manne ya kisheria ya mdaiwa Mwijaku yaliyokwishasikilizwa kupitia Wakili wake, Gideon Opanda aliyepambana na jopo la mawakili wanne wa Kipanya wakiongozwa na Wakili Alloyce Komba.
IMG_0351.jpeg

Mahakama ilibaini yenyewe kwamba kesi iliyokuwa ikiiendesha ilisajiliwa kwa makosa kama kesi ya madai ya kawaida (normal civil suit) badala ya kuwa ni madai ya kashfa (defamation petition) kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Habari za Mwaka 2019. Hivyo, kutokana na dosari hiyo Mahakama ikasitisha kuendelea na kesi ya msingi na kuiondoa.

Kabla ya uamuzi huo, Jaji Ngunyale alitoa fursa kwa mawakili wa pande zote mbili kutoa maoni yao ya kisheria kuhusu dosari hiyo na nini kifanyike kuhusu kesi hiyo ambapo Wakili wa Kipanya, Wakili Komba alisema kesi iondolewe na kumpa fursa nyingine mteja wake kufungua tena kesi hiyo ikiwa ataamua kufanya hivyo. Wakili wa Mwijaku, Wakili Opanda aliomba kesi iondolewe kwa gharama kutokana usumbufu wa kushitakiwa mteja wake.

Soma Pia:
Mahakama ilitoa amri ya kuondoa kesi yenye dosari ya usajili bila gharama ya usumbufu ikisema hoja ya dosari ya usajili iliibuliwa na Mahakama yenyewe (the issue was raised suo motu) na siyo na Wakili wa Mwijaku hivyo hapaswi kunufaika nayo.
IMG_0352.jpeg

Katika kesi ya msingi Kipanya alimshitaki Mwijaku kwa kumkashifu kupitia akaunti yake ya Instagram kwamba anafanya biashara haramu ya kuharibu vijana na kupitia katuni zake huwa anahongwa ili kuwadhalilisha viongozi wa Serikali wakiwemo Rais wa nchi. Hivyo akadai fidia ya shilingi bilioni tano na milioni mia tano (5.5bn/-) kwa madhara ya kashfa ya kushushushiwa hadhi ambayo ameijenga katika jamii kwa zaidi ya miaka thelathini.
 
Kesi itafunguliwa upya yule chawa mshamba aliyevamia mji kwa pupa asifikiri ndiyo kashinda kesi.
 
Naye kipanya wivu tu alitaka kaghorofa kama ka mwijaku
 
"Wewe unatuchora kwenye vibonzo vyako kila siku tunakukaushia, inauwaje kijana mwenzanko mwijaku unamfungulia kesi. Bwana masudi hapa hakuna kesi, ndiyo inabidi ukubali tu. Kama sisi tunavyokukaushia na wewe utulie"
 
Back
Top Bottom