Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tukiambiwa watanzania akili zetu kisoda huwa tunatokwa mapovuu kwelikweli..Mwijaku ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar es Salaam.
View attachment 2576622
Mtanzania maarufu wa Kituo Cha Redio kongwe nchini Clouds FM Mwemba Burton almaarufu kama Mwijaku ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar Es Salaam.
Katibu wa Chawa wa Mama Taifa Neema Karume amesema kuwa uteuzi huo umekuja baada ya Mwijaku kukidhi vigezo vya kuwa na nguvu ya uhamasishaji katika masuala ya Chama na Serikali na jamii nzima kwa ujumla.
Uteuzi huo umefanyika Aprili Mosi mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam.
"Tunamkaribisha sana ili tuungane kwa pamoja kuyasema yale yote mazuri anayoyafanya Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan hakika mama amefanya makubwa hatuna budi kumuunga mkono katika juhudi zake zote" amesema Katibu wa Chawa wa mama Taifa Neema Karume.
Katibu huyo wa Chawa Taifa Neema ameongeza kwa kusema kuwa kundi la Chawa wa Mama linaundwa na watu kutoka kada mbalimbali nchi nzima huku akiyataja baadhi yao makundi hayo kuwa ni Madereva wa Bodaboda, Madereva Taxi, Mabasi ya Abiria, Mama Lishe ,Wakulima, Wafugaji, Wafanyabiashara wakubwa na Wamachinga, Wasusi, Wavuvi, Wanasiasa, Wanafunzi wa Vyuo, Waalimu, Wakurugenzi katika taasisi mbalimbali Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi binafsi na Watanzani waliopo nje ya nchi ( DIASPORA).
Neema amesema kuwa lengo la kundi la Chawa wa Mama ni kuhakikisha wanakuwa Mabalozi wazuri ndani na nje ya nchi kwakuyasemea mazuri yanayotekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 wanaweka historia kwa Rais Dkt. Samia Hassan kuliongoza taifa katika awamu ya saba.
Chanzo: Haki Ngowi
Wewe endelea kukariri misemo ya wahenga wakati wenzio wanaendelea kusaka tongeWahenga waliposema "Kibaya chajiuza kizuri chajitembeza" hawakukosea kabisa.
Una maana chawa ni mashoga au ni sawa na mashoga au hawana tofautoi na mashoga!Kwa mwendo huu haishangazi vijana wengi wanakuwa mashoga. Mwanaume unakubali vipi kuitwa chawa wa mama?
Ipi akili safi, kisoda, kibia au ki"whiskey"Tukiambiwa watanzania akili zetu kisoda huwa tunatokwa mapovuu kwelikweli..
Hawana washauri jina linamchafua mama kuliko kum brand.Jina la Chawa sio jina zuri na halileti picha nzuri. Nawashauri watumie jina la "Vijana wa Mama" inaleta picha positive.