Mwijaku,"Mke wa Alikiba amekula maisha mazuri, mumewe hajatelekeza ndoa"

Mwijaku,"Mke wa Alikiba amekula maisha mazuri, mumewe hajatelekeza ndoa"

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mtangazaji na muigizaji, Mwijaku amefunguka sakata la Alikiba na mke wake Amina, akisema kuwa Alikiba hajaitelekeza ndoa yake.

Mwijaku amesema hayo Jumamosi Februari 19, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kutumwa na Alikiba kumuwakilisha kwenye mkutano huo ambao ulikuwa wa kuzungumzia ujio wa msanii Maher Zain kutoka nchini Sweden, ambaye atakuja Tanzania kufanya shoo na Alikiba Machi 21, 2022.

Wakati akimuwakilisha Alikiba, Mwijaku aliulizwa taarifa zilizosambaa zikidai kuwa mke wa Alikiba ameomba talaka akasema:

“Alikiba hajatelekeza ndoa yake, Ali ni miongoni mwa watu wanaojua kujali familia yake, kinachotokea hapendi kuweka mambo yake mitandaoni, ila tu watu wa pembeni ndiyo wamechangia bi Amina kuwa hivyo alivyo.

“Mimi nimeshafika kwenye familia ya Alikiba najua kinachoendelea, bi Amina amepata bahati ya kuwa na Maisha mazuri.”
 
Bi Amina akauliza huyo ndio nani?, wakamwambia huyo ndio Mganga wa Ally a.k.a sangoma, akaguna na kuachia kicheko cha kebehi.... akaambiwa katokea Kigoma huyo, macho yakamtoka akasema "are you serious".
 
Vitu vyengine vya hovyo tokee apewe bichwa na sifa za kipuuzi za kuitwa DC wa Insta naona anataka kujipa uchambuzi wa maswala ya familia za watu.
 
[emoji23]jamaa linakula maisha,yani hapo limetumwa na Ally kumuongelea.hii nchi mpaka ujiongeze,lingetumia masters sijui ni bachelor yake ile lisingekuwa na pesa za kila siku hizi
Mkuu pesa zipo nyingi sana kwenye mifuko ya watu unatakiwa uwe na akili tu ya kufanya hao watu watoe pesa zao mfukoni kukupa wewe.

Dunia ya leo vyeti vina matumizi madogo sana kukufanya uishi decent life.
 
Umesema vyema kabisa Mkuu, haya maisha yana mengi sana. ndio kuna member fulani alisema january sio ngumu akatoa mfano tutazame Bar watu wanavokunywa pombe kila siku
 
😂jamaa linakula maisha,yani hapo limetumwa na Ally kumuongelea.hii nchi mpaka ujiongeze,lingetumia masters sijui ni bachelor yake ile lisingekuwa na pesa za kila siku hizi
Kabisa. Anajua kujiongeza huyu.
Mi namuelewa anachofanya.
Sio mjinga yule.
 
😂jamaa linakula maisha,yani hapo limetumwa na Ally kumuongelea.hii nchi mpaka ujiongeze,lingetumia masters sijui ni bachelor yake ile lisingekuwa na pesa za kila siku hizi

Mwijaku ana degree ya sanaa kutoka department ya creative arts ya university of dar es salaam.

Digrii yake imemfundisha drama na ubunifu
 
😂jamaa linakula maisha,yani hapo limetumwa na Ally kumuongelea.hii nchi mpaka ujiongeze,lingetumia masters sijui ni bachelor yake ile lisingekuwa na pesa za kila siku hizi
Hapo limejiongeza,nadhani alitumwa akaongelee ujio wa show hiyo!Akakutana ghafla na swali!
Ally Kwa jinsi alivyo,hawezi kumtuma mtu akazungumzie maisha yake ya ndoa!Hilo nakataa!
 
Back
Top Bottom