Mwili unakuwa katika hali ya kupatwa na shocks za umeme

kilama

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
2,824
Reaction score
2,199
Habari za muda wakuu.

Naomba msaada wa hii ninayopitia ya mwili unakuwa katika hali ya kupatwa na shock kama ya umeme hasa nikiinamisha kichwa. Hospitali wameniambia wakati mwingine h-pyori huwa anasababisha hiyo lakini kwa muda ambao nimetumia dawa za h-pyori hiyo hali bado ipo.
 
Mkuu hauna deficiency ya vitamin fulani?, check hospital kwanza.

ila mara nyingi case ni hiyo kwa mwanzoni, ikikomaa wana jua cha kufanya.
 
Jaribu kupay attention katika mwili wako na utajia nini kinasababisha hayo yote. Kila kitu kina chanzo na matokeo. Kwaiyo jaribu kutaka kujua chanzo nini na katika hicho chanzo utaweza kubadili matokeo
 
Huenda ni upungufu wa uwiano wa virutubisho vya mwili, vinavyo julikana kama metabolites.
Ngoja nikujibu kikemia na kifizikia zaidi kuliko kibaolojia....

Ukichukua chumvi ya kupikia, ambayo inaitwa( Sodium Chloride), majina yasikushtue kama hujasemea, weka makini ninavyoelezea, .....
Ukachanganya na maji inakuwa (inageuza Sodium na Chloride kuwa Ionic solution, ........
Halafu ukichukua waya ukaunganisha na glopu, na kutumbukiza ndani ya hayo maji ya chumvi, inawaka!..

Sasa fikiria chakula unachokula kina virutubisho vya Sodium, Calcium, Potassium, na hizi zote zikiungana na Chlorine zinatengeza aina ya chumvi....
Na hivi vyote vinahitajika na kila seli ya mwili ili iweze kuishi, sasa kwa kuwa viko ndani ya mwili, vinageuka kuwa ni Ionic compound, yaani zinabadilishana nguvu ya kielectroniki zinapokuwa katika hali ya ute ute(majimaji), na kufua umeme wa mwili.
Kila kirutubusho kinaingia na kutoka kwenye seli kumpisha mwenzake, katika huu utaratibu, kila wanabodadilisha zamu, ni kama wanatengeneza cheche ndani ya mwili ambao ni umeme wa mwili.....

Sasa kama lishe yako haizingatii mlo kamili na wenye virutubisho vyote, unatengeneza uwiano usio sawa na kusababisha mwili kuwa unazungikwa na chaji ya umeme ambayo inahitaji kutoroka kama ukisalimia na watu au ukijigusa sehemu za mwili.
Nasubiri mtanange na wanasayansi na madaktari nijipatie mada ya kulalia........................
 
Nilijaribu kuulizia sehemu tofauti tofauti inaonekana hii hali inachagizwa na ukosefu wa vitamini B12 na hata nilipokwenda kwenye pharmacy jamaa alishauri nitumie aidha dawa za TB kwa kufikiri kwamba hizi dawa zina mchanganyiko mwingi au nitumie dawa za Vitamini B12. Hivyo, nilichagua dawa za Vitamini B12 inayoitwa CYANOCOBALAMIN ndiyo ninayoendelea nayo na siku ya 4.
 
Huenda ni upungufu wa uwiano wa virutubisho vya mwili, vinavyo julikana kama metabolites.
Ngoja nikujibu kikemia na kifizikia zaidi kuliko kibaolojia....

Ukichukua chumvi ya kupikia, ambayo inaitwa( Sodium Chloride), majina yasikushtue kama hujasemea, weka makini ninavyoelezea, .....
Ukachanganya na maji inakuwa (inageuza Sodium na Chloride kuwa Ionic solution, ........
Halafu ukichukua waya ukaunganisha na glopu, na kutumbukiza ndani ya hayo maji ya chumvi, inawaka!..

Sasa fikiria chakula unachokula kina virutubisho vya Sodium, Calcium, Potassium, na hizi zote zikiungana na Chlorine zinatengeza aina ya chumvi....
Na hivi vyote vinahitajika na kila seli ya mwili ili iweze kuishi, sasa kwa kuwa viko ndani ya mwili, vinageuka kuwa ni Ionic compound, yaani zinabadilishana nguvu ya kielectroniki zinapokuwa katika hali ya ute ute(majimaji), na kufua umeme wa mwili.
Kila kirutubusho kinaingia na kutoka kwenye seli kumpisha mwenzake, katika huu utaratibu, kila wanabodadilisha zamu, ni kama wanatengeneza cheche ndani ya mwili ambao ni umeme wa mwili.....

Sasa kama lishe yako haizingatii mlo kamili na wenye virutubisho vyote, unatengeneza uwiano usio sawa na kusababisha mwili kuwa unazungikwa na chaji ya umeme ambayo inahitaji kutoroka kama ukisalimia na watu au ukijigusa sehemu za mwili.
Nasubiri mtanange na wanasayansi na madaktari nijipatie mada ya kulalia........................
Asante kiongozi kwa ufafanuzi
 
Mkuu hauna deficiency ya vitamin fulani?, check hospital kwanza.

ila mara nyingi case ni hiyo kwa mwanzoni, ikikomaa wana jua cha kufanya.
Nilipokwenda hospitali daktari amekuja na hilo hitimisho/conclusion kwamba ni h-pyori japo sikuridhika moja kwa moja na maelezo yake. Kuna hali alionyesha ya wasiwasi wa ufahamu wa hicho kitu lakini basi imenibidi nipotezee.
 
Habari za muda wakuu.

Naomba msaada wa hii ninayopitia ya mwili unakuwa katika hali ya kupatwa na shock kama ya umeme hasa nikiinamisha kichwa. Hospitali wameniambia wakati mwingine h-pyori huwa anasababisha hiyo lakini kwa muda ambao nimetumia dawa za h-pyori hiyo hali bado ipo.
Tatizo uloambiwa linaweza kuwa ni ndiyo lakini linaweza kuwa hapana..
you need kufanya vipimo zaidi kwa changamoto uliyosema!

tuanze na tatizo la H-pylori na nikucorrect kidogo sio h-pyori ni H-pylori kwenye medical PYO ina maana nyingine kabisa so ukisema Pyori na Pylori ni tofauti (utani kidogo)

aliyesema kuwa PUD (ulcers disease ya Peptic) inaweza kusababisha anaweza kuwa sahihi to some extent ila kitaalamu Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya bakteria wa H. pylori (wanaosababisha vidonda vya tumbo) na dalili hii ya kushtuliwa na umeme unapoinamisha kichwa.

Nikubakiana na yeye kuwa kweli kwamba H. pylori ya muda mrefu inaweza kuzuia unyonyaji mzuri wa Vitamin B12 tumboni (na upungufu wa Vitamin B12 huweza kusababisha matatizo ya neva), lakini hata kama ni hivyo, tatizo kuu sasa hivi liko kwenye mfumo wa neva na uti wa mgongo, na sio tumboni tena. Ndio maana pamoja na kumaliza dozi ya H. pylori, hali hiyo haijaisha.

dalili uliyonayo na uliyotaja kitaalamu linaitwa Lhermitte's sign au Lhermitte's phenomenon...
au kwa lugha ya utani tunaita barber chair phenomenon..

mzee hiyo ni kiashiria cha hatri sana na ulipaswa kuwa MOI sasa hivi kwa ajili ya vipimo zaidi na sio kunywa dawa za PUD;;..
kwanini..?
kwa sababu hutokea wakati kuna mkandamizo, msuguano, au uharibifu wa neva (nerve irritation/demyelination) katika uti wa mgongo wa shingoni (Cervical Spinal Cord).

Wakati kichwa kinapoinamishwa, uti wa mgongo unajivuta kidogo; ikiwa kuna tatizo kwenye eneo hilo, basi mishipa ya neva zinasisimka na kutoa hiyo hisia ya "shock."..

inaweza ikawa ni Disc herniation (cervical disc herniation) au inaweza kuwa ni cervvical spondiliosis,au Matatizo ya Mfumo Mkuu wa Neva Kama vile Multiple Sclerosis (MS) au majeraha ya zamani ya shingo (whiplash),,

usizembee muone daktari wa Mishipa ya fahamu haraka kwa ajili ya evaluation na check up vinginevyo kuna hatari ya total paralysis
 
Asante sana mkuu nitafanya hivyo japo safari ya MOI ni mbali kidogo labda nijaribu hapa Bugando iliyopo karibu, sijajua kuhusu Chato kama naweza kupata huduma kwa usahihi.
 
Back
Top Bottom