Baadhi ya waombelezaji wakiaga mwili wa mtunzi na mwimbaji wa nyimbo za hamasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), George Mwingira aliyetamba na wimbo wa 'No reforms no election.'
Waombolezaji hao wameaga mwili wa Mwingira leo Jumamosi, Agosti 16, 2025 nyumbani kwao Matarawe, Songea, Mkoa wa Ruvuma. Mwingira maarufu 'MC Mwingira' alifariki dunia baada basi alilokuwa akisafiria kupata ajali maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro, Jumapili Agosti 10, 2025.
Inaelezwa MC Mwingira alikuwa akitoka Songea kwenda Dar es Salaam, kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anayekabiliwa na mashtaka ya uhaini.
Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema (Bara), John Heche baada ya msiba huo, akizungumza na Mwananchi alisema chama hicho, kimepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Mwingira aliyekuwa msanii kiongozi kwa kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali.
Chanzo: Mwananchi_official