John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Hadi kufikia asubuhi ya leo Ijumaa Februari 11, 2022 mwili wa aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Vincent Mbilinyi umeshindwa kutolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya mazishi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kuna deni la Sh milioni sita za matibabu yake.
Mbilinyi ambaye alifikwa na umauti juzi Februari 9, alfajiri akiwa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili akipatiwa matibabu kufuatia ajali ya bodaboda aliyopata Desemba 3, 2021.
Ndugu zake ambao walikuwa wakimuuguza muda mwingi wameshindwa kulipia gharama za matibabu aliyokuwa akipatiwa, ndiyo maana walifuatilia taratibu za kutoa mwili huo hospitali hapo kwa ajili ya mazishi lakini hawakufanikiwa.
Baadaye taarifa za mtandao wa @bongoboxingsafari ukaeleza kuwa kuna jitihada zinafanyika zikiongozwa na mwamuzi wa ndondi, Chaulembo Palasa na mwalimu wa mchezo huo, Super D lakini bado hakuna uhakika wa kuupata mwili.
Inaelezwa kuwa waliambiwa angalau wawe na Sh milioni mbili kisha ndiyo wapeleke maombi badala ya kwenda mikono mitupu, na tayari wameandika barua ya kupata msamaha wa deni hilo kwenda kwa mkurugenzi wa MOI.
------------------------
Ofisa Habari MOI, Parrick Mvungi alipoulizwa kuhusu hilo, alisema: “Ni kweli huo mwili upo, ndugu zake walikosea wakaenda kuomba katika uongozi wa Muhimbili, hivyo kukawa na mkanganyiko kidogo, lakini walielekezwa wakaja MOI.
“Jana nilionana nao wale viongozi wa ngumi na ndugu wa huyo bondia, nikawaelekeza utaratibu wanaotakiwa kuufanya, walikosea tu taratibu. Nafikiri wakikamilisha utaratibu watakabidhiwa, Serikali imeshasema hatutakiwi kuzuia mwili kisa mgonjwa alikuwa anadaiwa. Naamini wakikamilisha taratibu inavyotakiwa watakabidhiwa mwili wao."