Mwili wa dereva bodaboda Aron Enock Urio waokotwa shambani Arumeru, baada ya kupotea kwa siku kadhaa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwili wa kijana anayefahamika kwa jina la Aron Enock Urio, aliyekuwa akiendesha bodaboda eneo la Tengeru Kwa Fundi, umeokotwa katika shamba lililopo Kitongoji cha Madira, Kijiji cha Singisi, Kata ya Sela Singisi, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Aron alikuwa amepotea kwa siku kadhaa, hali iliyowafanya ndugu na marafiki kuanza kumtafuta. Mwili wake ulikutwa ukiwa na majeraha mbalimbali, ikiwemo kutobolewa macho.

Taarifa zinaeleza kuwa mwenye shamba hilo alikuwa akiweka mbolea kwenye mazao yake asubuhi alipokutana na mwili huo katikati ya shamba. Baada ya kukutana na mwili huo, alitoa taarifa kwa mamlaka za eneo hilo.

Jeshi la Polisi lilifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa Aron, kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya taratibu zaidi. Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwabaini waliohusika.

Soma Pia: Bodaboda auwawa na mwili wake kutupwa porini huko mkoani Morogoro

Attachments

  • IMG-20260827-WA0012.jpg
    IMG-20260827-WA0012.jpg
    22.3 KB · Views: 11
Mbona matendo ya ukatili yamekithiri sana kanda hiyo, Kuna shida gani hasa?

Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom