Mwili wa kijana wakutwa vichakani huku ukiwa na majeraha ya kitu chenye ncha kali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
MWILI wa kijana mmoja alietambulikana kwa jina la Noel Jengeni Mlilo (27), mkazi wa Wawi wilaya ya Chake Chake ambae ni mwenyeji wa mkoa wa Songwe Tanzania Bara, umepatikana umetelekezwa vichakani katika kijiji cha Mtuhaliwa, wilaya ya Mkoani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kaka wa marehemu, Devista Jengeni Mlilo (30), alisema marehemu aliondoka nyumbani tokea Oktoba 12, na hakurudi ndipo walipoomba msaada wa polisi kwa ajili ya kumtafuta.

Alisema marehemu hakuwa na kawaida ya kutorejea nyumbani na ndio sababu walipoona amechelewa kurudi wakaamua kumtafuta.

Aidha alisema, hakuwa na matatizo yoyote ya akili wala kiafya na alikuwa akifanya biashara zake katika maeneo ya Mkoani.

Mashuhuda wa tukio hilo, Zakaria Mgeni na Omar Shoka, walisema wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida, waliuona mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa karibu ya shina la muembe.

Waliseka eneo hilo ambapo marehemu alikuwepo ni karibu na kitalu cha miti cha wananchi wa shehia ya Mtuhaliwa, ambapo baadae waliamua kutoa taarifa kwa wananchi wengine.

Alisema upande wa pili wa barabara waliona mizigo ya vyombo ambavyo waliamini vilikuwa ni sehemu ya bidhaa za marehemu.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Dk. Mohamed Faki Saleh, marehemu alikuwa na majeraha madogo sehemu ya mbele ya mwili na mgongoni alikuwa na jeraha ambalo linaonesha kusababishwa na kitu chenye ncha kali.

Alisema hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kifo cha marehemu, na nyingine ni kukosa hewa na kuachana kwa mifupa ambayo yalisababishwa na mkabo uliokusudiwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

“Marehemu ana ishara ya kukabwa na inaonekana waliofanya hivyo, walikuwa na lengo la kutenganisha kichwa na kiwiliwili, kwani ana alama kubwa, lakini hawakufanikiwa, ingawa walimkosesha hewa na kisha kufariki,”alifafanua.

Sheha wa shehia ya Mkanyageni, Iddi Mohamed Kombo, alisema tukio hilo amelipokea kwa masikitiko na kuiasa jamii kuacha kujichukulia sheria mikononi.

Mkuu wa wilaya ya Mkoani, Issa Juma Ali, alisema taarifa ya kuonekana kwa mwili wa kijana huyo waliipokea saa 3:00 asubuhi.

Alisema tukio hilo ni lakusikitisha na wamelipokea kwa huzuni na kwamba haliwezi kuvumilika huku akiliomba jeshi la polisi kuwasaka wahusika.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, Kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba, Hassan Nassir Ali, alithibitisha taarifa hizo na wameanza uchunguzi.

Baadae mwili wa marehemu, ulikabidhiwa kwa ndungu zake kwa ajili ya mazishi.

Hili ni tukio la pili kwa mwaka huu kwa mkoa wa kusini Pemba, kuokotwa mtu akiwa amefariki, ambapo la kwanza lilitokea Agosti 1, ambapo maiti ikiwa imeshaoza iliokotwa katika shehia ya Wawi wilaya ya Chake Chake.
 
Polisi kikosi maalum kiende huko hawa wauaji wanalengo baya kwa taifa letu..
hawa watakuwa na ajenda ya siri ya kuwasha moto mkubwa baina ya watanzania,upelelezi ufanyike wapatikane ikibidi wapotezwe moja kwa moja..!
 
Binadamu tumekosa utu na tumefikia hatua ya kukatisha uhai wa wengingine hizi roho zitawalilia .
 
Basi usikute huyo dogo alikuwa anakula tu kwa raha zake watu wakakasirika na kutoa roho yake.
 
Hayo mauaji yana maswali mengi nyuma ya pazia

Wazee wa kazi mngelifanyia uchunguzi tukio hili mjue Chanzo chake

Isije ikawa jina lake Ndio limemponza
Polisi waanzie hapo.Isije kuwa labda Kama alikuwa muislamu kubadili dini Kama alikuwa muislamu kukawa sababu ya wenye siasa Kali kumtenda hivyo
 
huyu dada tokea nimeanza kumjua yeye huwa anaandika thread za vifo vifo tu
 
Back
Top Bottom