Mwili wa marehemu Tabia Mwanjelwa wawasili Dar, mazishi kufanyika kesho Kiwira, Mbeya

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Mwili wa mwanamuziki mkongwe, Bi. Tabia Shabani Mwanjelwa, aliyefariki Januari 25, 2025, huko Saarbrücken, Ujerumani, umewasili nchini leo na unatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwao Kiwira, wilayani Rungwe, Mbeya.

Binti wa marehemu, Jane Jackson, alisema mwili wa mama yake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Ethiopian Airlines, ukiambatana na mume wa marehemu, Bw. Elmar Moessner, na mtoto wake wa kiume, Moses.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, alikuwepo kuongoza mapokezi ya mwili huo.

Hata hivyo, wanamuziki na wadau wa muziki na hata wanahabari hawakujitokeza kwa wingi kama ilivyotarajiwa, hali iliyozua maswali mengi.

Marehemu atakumbukwa kwa vibao maarufu kama "Jane Mimi Nahangaika" na "Kweli Maisha ni Safari Ndefu", alizoimba na Maquis du Zaire miaka ya 1980.

Licha ya kuishi Ujerumani kwa zaidi ya miaka 40, alikuwa akirejea Tanzania mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Jane, mama yake alisumbuliwa na uvimbe kooni kwa muda mrefu, na wosia wake ulikuwa azikwe Kiwira alikozaliwa.

Jane, ambaye ndiye aliyeimbwa na mama yake katika kibao cha “Jane Mimi Nahangaika” amesema kwamba mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho saa saba mchana.

Mola ailaze pema roho ya marehemu
- AMINA
 
RIP legend Tabia Mwanjelwa.
 
Hapakuwa pazuri pa kuishi miaka 40 lakini pazuri pa kutupa maiti kwa mujibu wa wosia. Tumekubali, tufanyeje.

RIP japo wengine hatujawahi kumsikia. Nashangaa Waziri amepoteza mafuta ya serikali kwenda eti kuongoza mapokezi ya mwili. Sijui alikuwa anaelekeza jinsi ya kubeba jeneza kwenye ngazi za ndege ?

Wanatuteka akili kwa vitu vidogo vidogoooo, na wanatuona mabwege! Hatuhitaji uongozi wa serikali mpaka kwenye misiba. Ingekuwa familia imelosti kaa yangu tungesema wanahitaji mchango wa serikali wa ubwawa wa shuguli. Mmekaa Ujerumani miaka 40, take care of your own damn funeral.
 
Hapakuwa pazuri pa kuishi miaka 40 lakini pazuri pa kutupa maiti kwa mujibu wa wosia. Tumekubali, tufanyeje.

RIP japo wengine hatujawahi kumsikia. Nashangaa Waziri amepoteza mafuta ya serikali kwenda eti kuongoza mapokezi ya mwili. Sijui alikuwa anaelekeza jinsi ya kubeba jeneza kwenye ngazi za ndege ?

Wanatuteka akili kwa vitu vidogo vidogoooo, na wanatuona mabwege! Hatuhitaji uongozi wa serikali mpaka kwenye misiba. Ingekuwa familia imelosti kaa yangu mimi tungesema wanahitaji mchango wa serikali wa ubwawa wa shuguli. Mmekaa Ujerumani miaka 40, take care of your own damn funeral.
Mbona jiwe alizungushwa nchini akiwa maiti hukusema.... Halafu maiti ya jiwe haikupelekwa Kanda ya kaskazini
 
Mwili wa mwanamuziki mkongwe, Bi. Tabia Shabani Mwanjelwa, aliyefariki Januari 25, 2025, huko Saarbrücken, Ujerumani, umewasili nchini leo na unatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwao Kiwira, wilayani Rungwe, Mbeya.
Hivi ni ndugu na yule aliyekuwa mbunge na waziri aliyedukuliwa akisambaza rushwa Mbeya 2020?
 
Poleni wana familia,ndugu jamaa na ma rafiki na wana kiwira kwa msiba huu, RIP Tabia Mwanjelwa . Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe Amen
 
Hapakuwa pazuri pa kuishi miaka 40 lakini pazuri pa kutupa maiti kwa mujibu wa wosia. Tumekubali, tufanyeje.

RIP japo wengine hatujawahi kumsikia. Nashangaa Waziri amepoteza mafuta ya serikali kwenda eti kuongoza mapokezi ya mwili. Sijui alikuwa anaelekeza jinsi ya kubeba jeneza kwenye ngazi za ndege ?

Wanatuteka akili kwa vitu vidogo vidogoooo, na wanatuona mabwege! Hatuhitaji uongozi wa serikali mpaka kwenye misiba. Ingekuwa familia imelosti kaa yangu mimi tungesema wanahitaji mchango wa serikali wa ubwawa wa shuguli. Mmekaa Ujerumani miaka 40, take care of your own damn funeral.
Nyimbo zake zilikuwa maarufu sana Enzi za radio za 277.
 
Back
Top Bottom