DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mwili wa Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mzee Edwin Mtei (94), unatarajiwa kuwasili nyumbani kwake Tengeru, nje kidogo ya Jiji la Arusha, leo saa 11:00 jioni.
Shughuli za mapokezi ya mwili huo, zitaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, baada ya kuchukuliwa Hospitali Teule ya Selian majira ya saa 10:00 jioni na kupitishwa barabara kuu ya Arusha/Moshi.
Msemaji wa familia ya Mtei, Freeman Mbowe, amesema mwili huo utachukuliwa leo kwa kufuata itifaki za CHADEMA katika Hospitali Teule ya Selian iliyopo Jijini Arusha na baadae kutakuwa mkesha hadi siku ya kesho asubuhi Januari 24, ambako ratiba ya shughuli za kichama itaanza saa 3:00 asubuhi.
"Tumejaribu kutafuta njia ili kila kundi lipate nafasi ya kutoa salamu zake na liweze kushiriki kadri linavyoweza. Yako makundi ya kisiasa, vyama vya siasa vyote vimetupa taarifa ya kufika.
"Chama kiongozi katika jambo hili ni CHADEMA, ambapo CHADEMA huyu ni mwasisi wa chama chetu. Kwa hiyo nafasi kubwa itatolewa kwa CHADEMA, kwa sababu baba ni mwasisi wa chama chetu lakini baada ya hapo yatafuata makundi mbalimbali."
"Chama cha ACT Wazalendo, tumepokea taarifa za kushiriki kwao, viongozi wa serikali vilevile wametoa taarifa za kushiriki kwao, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Gavana nimemuona hapa wametoa taarifa ya kushiriki kwao na taasisi nyingine mbalimbali, Jumuiya ya Afrika ya Afrika ya Mashariki wamesema watatoa taarifa yao." amesema Mbowe.
Chanzo: Nipashe