Mwili wa Rais wa Zamani wa Zambia, Edgar Lungu kuzikwa Afrika Kusini

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Familia ya aliyekuwa Rais wa Sita wa Zambia, Dkt. Edgar Lungu imetangaza kuwa mazishi yake yatafanyika nchini Afrika ya Kusini kwa ibada ya faragha

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Familia hiyo Mheshimiwa Makebi Zulu leo Juni 20 imeeleza kuwa nchini ya Afrika ya Kusini imeridhia kuipa familia hiyo uhuru wa kufanya ibada muhimu ya mazishi bila kuwaingilia

"Kwa niaba ya familia ya Lungu, tunapenda kutangaza kwamba mazishi na ibada ya mwisho ya mpendwa wetu, Dkt. Edgar Chagwa Lungu, yatafanyika hapa Afrika Kusini, kwa mujibu wa matakwa ya familia ya kuwa na ibada ya faragha." imesema taarifa

"Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini kwa msaada wao wa heshima na kwa kuheshimu uamuzi wa familia wa kufanya ibada ya faragha hapa Afrika Kusini." ameongeza Makebi

Hata hivyo taarifa imesema kuwa itaendelea kutafuta mshikamano na amani baina ya Wazambia katika kipindi hiki kigumu huku wakieleza kuwa hivi karibuni itatolewa taarifa juu ya siku ya mazishi na ibada ya mwisho ya Lungu.

Haya yanajiri baada ya jana Juni 19, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema kutangaza kuwa Hayati Lungu atazikwa nchini Zambia kwa heshima kiserikali na sio nchi nyingine yoyote

Soma pia: - Mazishi ya Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu kuleta utata baada ya serikali kusitisha
maombolezo
-Familia na Serikali zakubaliana Lungu kuzikwa Juni 22 Lusaka, Zambia

====
The family of the late President Edgar Chagwa Lungu has confirmed that the former head of state will be laid to rest in Johannesburg, South Africa, following a private family ceremony.

In a statement issued today, the family expressed deep appreciation for the support received from across Africa and commended the South African government for its non-interference and respect for their decision.

Family spokesperson Hon. Makebi Zulu noted that the family seeks peace and unity during this difficult period, and that further funeral details will be communicated in due course.

444.png

​

Source: SABC & LUSAKA TIMES​
 
Familia ya aliyekuwa Rais wa Sita wa Zambia, Dkt. Edgar Lungu imetangaza kuwa mazishi yake yatafanyika nchini Afrika ya Kusini kwa ibada ya faragha

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Familia hiyo Mheshimiwa Makebi Zulu leo Juni 20 imeeleza kuwa nchini ya Afrika ya Kusini imeridhia kuipa familia hiyo uhuru wa kufanya ibada muhimu ya mazishi bila kuwaingilia

"Kwa niaba ya familia ya Lungu, tunapenda kutangaza kwamba mazishi na ibada ya mwisho ya mpendwa wetu, Dkt. Edgar Chagwa Lungu, yatafanyika hapa Afrika Kusini, kwa mujibu wa matakwa ya familia ya kuwa na ibada ya faragha." imesema taarifa

"Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini kwa msaada wao wa heshima na kwa kuheshimu uamuzi wa familia wa kufanya ibada ya faragha hapa Afrika Kusini." ameongeza Makebi

Hata hivyo taarifa imesema kuwa itaendelea kutafuta mshikamano na amani baina ya Wazambia katika kipindi hiki kigumu huku wakieleza kuwa hivi karibuni itatolewa taarifa juu ya siku ya mazishi na ibada ya mwisho ya Lungu.

Haya yanajiri baada ya jana Juni 19, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema kutangaza kuwa Hayati Lungu atazikwa nchini Zambia kwa heshima kiserikali na sio nchi nyingine yoyote

====
The family of the late President Edgar Chagwa Lungu has confirmed that the former head of state will be laid to rest in Johannesburg, South Africa, following a private family ceremony.

In a statement issued today, the family expressed deep appreciation for the support received from across Africa and commended the South African government for its non-interference and respect for their decision.

Family spokesperson Hon. Makebi Zulu noted that the family seeks peace and unity during this difficult period, and that further funeral details will be communicated in due course.

Omba mod wakubadilishie iwe Zambia instead of Zimbabwe
 
HAITAWEZEKANA AZIKWE SOUTH AFRICA. ZAMBIA ITAKOSA KUMBUKUMBU YA MTU MUHIMU ALIEWAHI KUWA KIONGOZI WAO. LAZIMA AZIKWE ZAMBIA
 
Shughuli yake duniani ishakwisha, wazike popote tu...
 
Back
Top Bottom