Mwili wa Rais wa Zamani wa Zambia, Edgar Lungu kuzikwa Afrika Kusini

Hata kizmkazi atazikwa Omani
 
Pesa alizoiba huyo Lungu aliziweka Africa kusini na kawekeza hasa Africa ya kusini
Anazikwa mali zake ziliko
 
Inawezekana jamaa hakuwa mzambia,kwa Nini gvt isitishe maombolezo!?



Levy mwanawasa pia Kuna story alikuwa mnyamwanga wa Tanzania


🤔🤔
 
Familia ya rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu, imetangaza kuwa kiongozi huyo wa zamani atazikwa Afrika kusini. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa zamani wa nchi nyengine kuzikwa nchini humo.

Uamuzi wa familia umejiri baada ya mvutano na serikali ya Zambia kuhusu mipango ya maziko ya kitaifa ya Hayati Lungu. Familia yake ilizuwia mwili wake kusafirishwa Zambia kutoka Afrika Kusini, alikokuwa anapokea matibabu, baada ya kugundulika kuwa rais wa sasa Hakainde Hichilema, alipanga kuupokea mwili huo hatua ambayo ni kinyume na alivyotaka Lungu.

Msemaji wa Familia ya Edgar Lungu, Makebi Zulu, alithibitisha maziko ya kiongozi huyo wa zamani aliyefariki dunia Juni 5 yatafanyika Afrika Kusini. Amesema familia yake inaomba amani na mshikamano wakati huu mgumu.

Lungu alichaguliwa mwaka 2015 kuiongoza Zambia iliyotajiri kwa madini ya shaba. Miaka sita baadae nafasi yake ikachukuliwa na Hichilema baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu 2021. Tangu wakati huo mkewe na watoto wake wameshitakiwa kwa rushwa na uhalifu, mashitaka ambayo familia imeyakanusha na kudai yamechochewa kisiasa.
 
Atakuwa sio wa kwanza.
Mobutu tseseko alifia nje na kuzikwa hukohuko...Amini wa uganda pia.

Nawasiwasi hata obote hakuzikwa Uganda.

Mbunge Nimrod mkono yeye sijui alizikwa wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…