Mwili wangu unatoa umeme?

Mosahe

Member
Joined
Feb 22, 2017
Posts
67
Reaction score
33
Nashindwa kuelewa niniaumwa au ni hali ya kawaida, huwa napigwa shock kama ya umeme nikigusa vitu kama meza, mlango, kiti na baadhi ya nguo ninapokuwa ninagusa kwa mara ya kwanza ila nikishashika kwa muda vitu hivyo hali huwa shwari.
 
Na Mimi ni tatizo hilo ngoja nisubiri majibu huwa mara nyingi nikifungua mlango wa gari au nikimshika mtu nampiga shoti ya umeme.
 
Huo ni upako umekujaa...jitahidi ufanye makuu, watu adimu sana ninyi
 
Umenikumbusha wakati naishi Namibia hiyo hali inakua ni kawaida na kila raia hua ana experience kutokana na kua na jua kali sana ,joto hivyo hupelekea ngozi kua kavu na ku produce hizo electrons (static electricity)
 
Nawezaje kuikabiri hali hii
je kila mtu anayo hali hii na madhara yake ni yapi.
 
Hatimaye Tanzania Yagundua "umeme utokanao na mwili wa binadamu"

Ndugu yangu hilo ni bonge la dili, wala usiwe na wasiwasi
 
MNANISHAURI NIJIFUNGE KATRANSIFOMA KADOGO NIWE NACHAKI W3 YA GU?
 
Nashindwa kuelewa niniaumwa au ni hali ya kawaida, huwa napigwa shock kama ya umeme nikigusa vitu kama meza, mlango, kiti na baadhi ya nguo ninapokuwa ninagusa kwa mara ya kwanza ila nikishashika kwa muda vitu hivyo hali huwa shwari.
ongea na tanesco wakuunganishe kwenye gridi ya Taifa mkuu
 
Ila tuacha jokes basi mkanisaidia maana sasa hata wanakijiji wenzangu wanahisi nina majini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…