PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana Chaz Baba anadaiwa nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya kumpiga na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.
MANENO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo karibu na wanafamilia hao (jina limehifadhiwa), usiku wa Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar kilishuhudia ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia nani anamshushia kipondo mwenzake.
Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.
Dah! Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana, kilidai chanzo hicho.
MKE AFUNGUKA EI TU ZEDI
Baada ya taarifa hiyo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta mwanamke huyo ili aeleze nini kilitokea hadi mumewe kutaka kumkatishia maisha.Nakumbuka siku ya tukio nilikuwa supermarket maeneo ya Mwananyamala A (jijini Dar) nikinunua unga wa ulezi wa mtoto, ghafla Chaz alitokea, akaniamuru niingie kwenye gari alilokuwemo, tukaondoka kuelekea nyumbani.
Tulipofika maeneo ya Kinondoni, pale Meridian ndipo niliposhtukia naanza kupigwa. Nakumbuka nilipigwa hadi nikaishiwa nguvu mpaka akatokea rafiki wa Chaz, Hassan Kisanora na kuniokoa, nikakimbilia nyumbani, alisema mwanamke huyo.
CHAZ ATOWEKA, ARUDI NA SAMAKI MKUBWA
Akiendelea kuzungumza, mke huyo alisema: Siku hiyo Chaz aliondoka na hakurudi nyumbani mpaka alfajiri. Aliporudi aliniambia amekuja na samaki mkubwa, yuko kwenye friji huku akisahau kuwa amenikosea na anatakiwa kuniomba msamaha.
Sikumjibu, ndipo alipochukua kitu kizito na kunipiga nacho kichwani, baada ya hapo damu nyingi zikaanza kunitoka hadi puani, niliishiwa nguvu na kupoteza fahamu.
Nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali kwa Dk. Mvungi, Kinondoni. Licha ya kwamba nampenda sana lakini alitaka kuniua, hata sijui kisa.
MADAI YA KUSHANGAZA; NDANI YA MIEZI TISA KICHAPO MARA 16
Katika kuweka mambo zaidi hadharani, mwanamke huyo aliyebahatika kupata mtoto mmoja na mumewe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, tangu afunge ndoa na Chaz miezi tisa iliyopita, ameshachezea kichapo mara kumi na sita hivyo amechoka kufanywa ngoma.Nimechoka kufanywa ngoma na Chaz, ndoa ina miezi tisa tu nishapigwa mara kumi na sita kati ya hizo nimezimia mara saba kama vipi bora afanye utaratibu anirudishe kwetu, alimalizia kusema.
CHAZ BABA, IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kupata maelezo ya mke, Ijumaa Wikienda lilimsaka kwa njia ya simu Chaz mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ya mkewe kudai alimpiga ambapo alipopatikana alifunguka hivi:
Ni wivu tu kaka! Unajua mke wangu ana wivu mkali sana, alianza kunipiga yeye mimi ndiyo nikamrudishia, hakukuwa na sababu nyingine yoyote zaidi ya wivu, alisema Chaz bila kufafanua.
GP
Anangoja ufanywe utaratibu arudishwe kwao?! Amesahau njia kwani?
Labda anasubiri amaliziwe mahari yakeee...
Sikiliza, mama anaitwa Rehema Sospeter Marwa....akina Marwa nilipata kusikia hii kipigo ni mapenzi ya dhati....mweh!!Umepigwa mara kibao na ushazimia mara 7, but still upo tu umekomaa na ndoa. Una uhakika gani kama next time utakavyopigwa uta-survive? Hata kama wewe ndo umekosea labda, ndo upigwe hadi na kitu kizito kichwani? What if ungekufa? Hicho kichapo cha kwenye picha ni kwa ajili ya mke au mwizi?
Jamani wanawake tusilete utani na maisha. Usichukulie maisha kama ni kitu simple hivyo, kwamba utapigwa but utakuwa tu ok. Kesho utapigwa hadi ufe then tubaki tunalia tu afu tutakusahau tu baadaye. Na wewe charles kama mtu kakushinda si umuache tu. Utamuua mtoto wa watu afu uishie jela mfyuuuuuuuuu
Uvumilivu wa kichapo kwenye ndoa nimeapa sitakubali ukijaribu kunipiga hata kibao we loose each other kama unapesa jua natafuta namna ya kukufilisi ndiyo nisepe
Heaven Sent
Wewe huoni ni ujiko kuitwa mke wa Chalz Baba?
Halafu bado kuna mizembe inawasema wadada over 30 ambao hawajaolewa, sasa hii ni ndoa au gereza?
Sikiliza, mama anaitwa Rehema Sospeter Marwa....akina Marwa nilipata kusikia hii kipigo ni mapenzi ya dhati....mweh!!
Aisee ndio kupiga gani huko????mi naachika kabisaaa