Mwimbaji Chaz Baba nusura amuue mkewe, ampiga na kitu kizito kichwani mpaka mke kuzimia

Mwimbaji Chaz Baba nusura amuue mkewe, ampiga na kitu kizito kichwani mpaka mke kuzimia

Huyo Dada jina lake la mwisho ni 'marwa' wengi wao wanaamini wasipopigwahawapendwi!!!!
 
He must be crazy lolz

Imebidi ni ka google picha za harusi yake.

Kweli mahaba niue..mweeee
 
Anangoja ufanywe utaratibu arudishwe kwao?! Amesahau njia kwani?
 






PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’ anadaiwa nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya kumpiga na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.

MANENO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo karibu na wanafamilia hao (jina limehifadhiwa), usiku wa Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar kilishuhudia ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia nani anamshushia kipondo mwenzake.

Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.

“Dah! Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana,” kilidai chanzo hicho.

MKE AFUNGUKA ‘EI TU ZEDI’
Baada ya taarifa hiyo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta mwanamke huyo ili aeleze nini kilitokea hadi mumewe kutaka kumkatishia maisha.“Nakumbuka siku ya tukio nilikuwa supermarket maeneo ya Mwananyamala A (jijini Dar) nikinunua unga wa ulezi wa mtoto, ghafla Chaz alitokea, akaniamuru niingie kwenye gari alilokuwemo, tukaondoka kuelekea nyumbani.

“Tulipofika maeneo ya Kinondoni, pale Meridian ndipo niliposhtukia naanza kupigwa. Nakumbuka nilipigwa hadi nikaishiwa nguvu mpaka akatokea rafiki wa Chaz, Hassan Kisanora na kuniokoa, nikakimbilia nyumbani,” alisema mwanamke huyo.

CHAZ ATOWEKA, ARUDI NA SAMAKI MKUBWA
Akiendelea kuzungumza, mke huyo alisema: “Siku hiyo Chaz aliondoka na hakurudi nyumbani mpaka alfajiri. Aliporudi aliniambia amekuja na samaki mkubwa, yuko kwenye friji huku akisahau kuwa amenikosea na anatakiwa kuniomba msamaha.

“Sikumjibu, ndipo alipochukua kitu kizito na kunipiga nacho kichwani, baada ya hapo damu nyingi zikaanza kunitoka hadi puani, niliishiwa nguvu na kupoteza fahamu.”
“Nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali kwa Dk. Mvungi, Kinondoni. Licha ya kwamba nampenda sana lakini alitaka kuniua, hata sijui kisa.”

MADAI YA KUSHANGAZA; NDANI YA MIEZI TISA KICHAPO MARA 16
Katika kuweka mambo zaidi hadharani, mwanamke huyo aliyebahatika kupata mtoto mmoja na mumewe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, tangu afunge ndoa na Chaz miezi tisa iliyopita, ameshachezea kichapo mara kumi na sita hivyo amechoka kufanywa ngoma.“Nimechoka kufanywa ngoma na Chaz, ndoa ina miezi tisa tu nishapigwa mara kumi na sita kati ya hizo nimezimia mara saba kama vipi bora afanye utaratibu anirudishe kwetu,” alimalizia kusema.

CHAZ BABA, IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kupata maelezo ya mke, Ijumaa Wikienda lilimsaka kwa njia ya simu Chaz mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ya mkewe kudai alimpiga ambapo alipopatikana alifunguka hivi:

“Ni wivu tu kaka! Unajua mke wangu ana wivu mkali sana, alianza kunipiga yeye mimi ndiyo nikamrudishia, hakukuwa na sababu nyingine yoyote zaidi ya wivu,” alisema Chaz bila kufafanua.
GP


Du! Chalz hafai kabisa. Tena afadhali hakumuoa byutiful Onyinye mtoto wa Sepetunga. Manake kwa hicho kipondo anachotoa mpka mtu kushonwa sijui Wema angekuwaje maana na huo mkorogo wake sijui kama angeshoneka. Bora wali date tu then wakaachana.
 
JOE THOMAS-"I Understand"

I understand [x 4]
Girl I understand, I understand,
See I understand,

You used to be the life of the party
But now you walk with head hung low
Cause he ride your nerves like a harley
And it's obvious that wasn't there before
Now you taken to wearing make up
To hide the marks that wasn't there before
In your heart you wanna break up
Can't find the nerve to walk out the door

Why don't you take those chains and break those chains
No love should cause you so much pain
Why don't you walk away before it gets too late
Leave him now
(see I understand)
Love should never hurt

You should have left the first time that he hit you
But instead you just stead and cried
Your friends and family tried to tell you
But you told them to mind their B.I
A career girl with a bright future
You had so much going on in your life
Since that man came along and abused you
Bour life has been everything but right
Two babies at home, can't pay the damn loan
Girl it's all wrong, you gotta move on
You say you really love him, I understand lady but tell me

Why don't you leave that man, go on your own
You're so fine, you are strong
Spread your wings, fly away
Girl don't cry another day
Don't give up, take a chance
Find your way, take a stand
You'll find that there's a better plan out there for you
 
Zilipendwa
 

Attachments

  • 1410860141402.jpg
    1410860141402.jpg
    43.3 KB · Views: 228
Kwa msio elewa english,na maneno ya kimarekani .....mnakosa elimu kubwa sana ya kigentlemen kutoka kwa huyo msanii hapo juu.
 
Umepigwa mara kibao na ushazimia mara 7, but still upo tu umekomaa na ndoa. Una uhakika gani kama next time utakavyopigwa uta-survive? Hata kama wewe ndo umekosea labda, ndo upigwe hadi na kitu kizito kichwani? What if ungekufa? Hicho kichapo cha kwenye picha ni kwa ajili ya mke au mwizi?
Jamani wanawake tusilete utani na maisha. Usichukulie maisha kama ni kitu simple hivyo, kwamba utapigwa but utakuwa tu ok. Kesho utapigwa hadi ufe then tubaki tunalia tu afu tutakusahau tu baadaye. Na wewe charles kama mtu kakushinda si umuache tu. Utamuua mtoto wa watu afu uishie jela mfyuuuuuuuuu
Sikiliza, mama anaitwa Rehema Sospeter Marwa....akina Marwa nilipata kusikia hii kipigo ni mapenzi ya dhati....mweh!!
 
Uvumilivu wa kichapo kwenye ndoa nimeapa sitakubali ukijaribu kunipiga hata kibao we loose each other kama unapesa jua natafuta namna ya kukufilisi ndiyo nisepe

Haha siku izi wanaume wanaoa kijanja wewe, ingekua kufilisi rahisi kiivo wengi wangekua matajiri....kuna kitu inaitwa Exemption Clause....nenda kahugo upate madini zaidi
 
Heaven Sent
Wewe huoni ni ujiko kuitwa mke wa Chalz Baba?

Halafu bado kuna mizembe inawasema wadada over 30 ambao hawajaolewa, sasa hii ni ndoa au gereza?




Ukitaka kuwa na ndoa ngumu sana, basi ingia na msanii.
Na ndoa hizo zisitumike kama reference kwa ndoa zote.
 
Back
Top Bottom