PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Rwanda, Gloriose Musabyimana, maarufu kama Gogo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 36 nchini Uganda.
Taarifa zinasema alifariki usiku wa Septemba 3, baada ya kuugua kwa muda mfupi alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini Kampala. Ingawa sababu kamili ya kifo chake haijathibitishwa, lakini katika moja ya mahojiano yake aliwahi kueleza kuhusu changamoto za kiafya ikiwemo matatizo ya moyo.
Gogo alikuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda na Uganda, ambako alifanya matamasha kadhaa yenye mafanikio, hasa jijini Kampala yaliyovuta maelfu ya watu
Umaarufu wake uliongezeka kupitia mitandao ya kijamii kama YouTube na TikTok, ambapo nyimbo zake maarufu “Everyday, I Need Blood of Jesus” zilisambaa sana mitandaoni na baadaye kuachia nyimbo nyingine ikiwemo ya Krismasi “Uwo Mwana.”