Mwina Kaduguda azua balaa uchaguzi klabu ya Simba

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ni baada ya wapiga kura tuliotangaziwa awali kuongezeka kutoka 1400 hadi 1728 , wamezaana lini haifahamiki ! ikumbukwe kwamba Mwina Kaduguda anagombea ujumbe.

Hii si mara ya kwanza kwa Mwina Kaduguda kupigania haki yake ndani ya simba , mara ya kwanza ilikuwa pale alipodai kurudishiwa hela ya chapati alizonunua kwa ajili ya kifungua kinywa cha wachezaji wa Simba.

....... Tutaendelea kuwajulisha yote yanayotokea kwenye uchaguzi huu , ikiwemo yale ya nyuma ya pazia .
 
"" mara ya kwanza ilikuwa pale alipodai kurudishiwa hela ya chapati alizonunua kwa ajili ya kifungua kinywa cha wachezaji wa Simba ""
Naomba kuuliza,hio sentensi ni kweli yalitokea au ni maneno code,yaani yana maana nyingine ?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakuna maana nyingine , Kaduguda akiwa kocha msaidizi wa simba alilazimika kununua chapati za chai kwa wachezaji baada ya viongozi kuchelewesha hela , hata hivyo alidai pesa zake na baada ya danadana akaamua kuripua kwenye vyombo vya habari .
 
Sasa nae anadai hela ya chai!!!? Ndio apewe ujumbe huyu.
Akafie mbele
 
Huyu Kadu nakumbuka kuna mechi Simba ilifungwa na Yanga, nilimuona analia uwanjani nilimuonea huruma sana. Ana uchungu sana na Simba, ila kitendo cha kudai fedha za chapati sio kizuri kwa mtu mwenye mapenzi na Timu. Si ajabu atashindwa hata kuwasaidia wachezaji punde wakimpiga mizinga ya shida.
 
Huyu ni Jipu pale Simbaa..
Watu kama hawa hatutakiwi kuwa nao
 
"" mara ya kwanza ilikuwa pale alipodai kurudishiwa hela ya chapati alizonunua kwa ajili ya kifungua kinywa cha wachezaji wa Simba ""
Naomba kuuliza,hio sentensi ni kweli yalitokea au ni maneno code,yaani yana maana nyingine ?[emoji23][emoji23][emoji23]
Ni kweli kabisa ilitokea wala si stori za kupotezea muda. Ilikuwa hivi:
Kaduguda wakati huo alikuwa kocha msaidizi wa Simba (nasema kocha msaidizi, pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Simba na TFF/FAT). Sasa baada ya mazoezi ya asubuhi, wachezaji wakapelekwa restaurant moja wakapate breakfast. Kutokana na wepesi wa kifungua kinywa kile kulinganisha na mazoezi, na viongozi hawakuwepo, Kaduguda akaamua kutingia mfukoni mwake na kununua chapati 60 na kuwapa wachezaji 30, yaani kila mmoja aongeze chapati mbili mbili, na kwa kuwa zilikuwa zinauzwa sh. 100/= each, ilimgharimu sh. 6,000/= (elfu sita tu) kwa chapati zote. Baada ya siku ile, Kaduguda akaanza kuudai uongozi umrudishie hela yake aliyojitolea. Uongozi ukawa unamzungusha siku hadi siku. Basi siku moja baada ya mazoezi ya timu, Kaduguda akaamua kuchukua mipira ya timu kama shinikizo la kulipwa elfu sita yake! Sijajua hatima yake ilikuwaje
 
Asee daah,soka oetu bado sana kumbe,
Na imagine team ndogo ndogo zilikua zina hali gani
 
Hakuna maana nyingine , Kaduguda akiwa kocha msaidizi wa simba alilazimika kununua chapati za chai kwa wachezaji baada ya viongozi kuchelewesha hela , hata hivyo alidai pesa zake na baada ya danadana akaamua kuripua kwenye vyombo vya habari .
Viongozi wa juu wangetumia akili kidogo,hii habari isingevuja,daah hadi aibu kusema kweli.
Wangempaga chake tu angemute,ila safi sana kwa alivyojitoleaga
 
"" mara ya kwanza ilikuwa pale alipodai kurudishiwa hela ya chapati alizonunua kwa ajili ya kifungua kinywa cha wachezaji wa Simba ""
Naomba kuuliza,hio sentensi ni kweli yalitokea au ni maneno code,yaani yana maana nyingine ?[emoji23][emoji23][emoji23]
Ni kweli kabisa hii
 
dah mkuu haya ya kweli nakumbuka ilitokea mwaka 2007
 
Ni kweli kabisa ilitokea wala si stori za kupotezea muda. Ilikuwa hivi:
Kaduguda wakati huo alikuwa kocha msaidizi wa Simba (nasema kocha msaidizi, pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Simba na TFF/FAT). Sasa baada ya mazoezi ya asubuhi, wachezaji wakapelekwa restaurant moja wakapate breakfast. Kutokana na wepesi wa kifungua kinywa kile kulinganisha na mazoezi, na viongozi hawakuwepo, Kaduguda akaamua kutingia mfukoni mwake na kununua chapati 60 na kuwapa wachezaji 30, yaani kila mmoja aongeze chapati mbili mbili, na kwa kuwa zilikuwa zinauzwa sh. 100/= each, ilimgharimu sh. 6,000/= (elfu sita tu) kwa chapati zote. Baada ya siku ile, Kaduguda akaanza kuudai uongozi umrudishie hela yake aliyojitolea. Uongozi ukawa unamzungusha siku hadi siku. Basi siku moja baada ya mazoezi ya timu, Kaduguda akaamua kuchukua mipira ya timu kama shinikizo la kulipwa elfu sita yake! Sijajua hatima yake ilikuwaje
Kwa hili namtetea Mwina, timu ilikuwa na bajeti yake. Ilikuwaje viongozi wakachelewa? Mwina alijua Kama akikaa kimya atakuwa kapigwa yeye hiyo hela, yaani kanunua kwa pesa zake huku kiongozi mmoja akilamba hizo pesa. Hoja sio kiadi Cha pesa, Bali Nani ananufaika nayo!!
 
Kwenye taasisi yoyote unapoamua kusaidia basi toa ukiwa unajua hakuna haja ya kurudishiwa endapo msaada wako ni hisani tu na hauna chanzo sahihi kinachoeleweka kupata hitaji husika. Mwina Kaduguda naamini hakuwa mjinga kudai hela yake ya chapati ukizingatia tabia za viongizi wengi wa vilabu hapa nchini. Simba kama taasisi, club kubwa, yenye mashabiki na wanachama wengi walishindwaje kuwanunulia chapati wachezaji, walishindwaje kumlipa mwina hela yake wanayoiita ndogo? Kwa nini walimzungusha huku timu ina budget yake. Ukiweza kudhibiti mazoea ya kutumia kidogo nje ya budget utazuia vikubwa pia. Kitendo cha mwina kinaashilia kuna wengine wengi huwa/walikuwa wanatoa fedha zao kidogo kidogo mifukoni mwao na hawalejeshewi ambapo mwisho wa siku bajeti ya timu inakuwa kubwa kwa vitu Vidogovidogo vingi, wanaolipa wengine, na viongozi inawezekana wakapiga kikubwa kilichotokana na vudogo vingi.......!!!!
 
Back
Top Bottom