Mwina Kaduguda: Nipo tayari kufa ili Simba Sc ifanikiwe

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mwina Kaduguda amesema kuwa wapo tayari kufa ila Simba ifanikiwe na kufikia malengo yao kwa msimu huu.
.
“Tunaziona timu zilizofanikiwa Afrika kuwa na uwekezaji mkubwa. Simba pia tupo kwenye njia hiyo kwa msimu wa tano sasa kwanini tusifanikiwe kubeba mataji makubwa Afrika?” amesema mwenyekiti huyo wa zamani wa Simba na kuongeza:
.
“Tunaamini tunaweza kumfunga yeyote na kutwaa mataji kama ilivyo lengo letu na nipo tayari KUFA ili kuhakikisha Simba inafikia malengo na kutwa mataji makubwa makubwa Afrika.” amesema Kaduguda.

My Take
Nami nipo tayari kufa ili Simba ifanikiwe. Simba Nguvu Moja
 
Bila shaka hiki ni kile kibwagizo kinachotumika efm kipindi cha sports hq ,bwana simba wa yuda aipenda simba kwelikweli
 
Acheni kukufuru Mungu nyie

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Wewe sema upo tayari kufa kwa ajili ya Mwamedi na si Simba
 
Mwache afe sisi turithi mali zake, mke na watoto
 
Chapati zako ulishalipwa,Mzee wa litochi?
 
Acha makasiriko ya kijinga na kuishia kutukana watu hovyoo!! Nani kakwambia Kila kinachoandikwa humu ni uhalisia??. Tumia hata akili za visigino kujibu na sio kuja na makasiriko ya kipuuzi wakati watu hutania!!
 
Aliwahi kudai hela zake alizonunua Chapati kwenye kambi ya Simba. Tena alizidai kwa lugha mbaya sana
 
Mtu anayeweza kudai elf 5 ya chapati hana hasara ya kufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…