Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nimeamka nikiwa na matumaini makubwa ya mwaka mpya na mojawapo ya mambo ambayo ka'nzi' kamenibrief ni mabadiliko ya ndani ambayo yametokea Idara yetu ya Usalama wa Taifa mabadiliko ambayo kama ilivyotarajiwa yanaendeleza kufahamianization. Mmoja wa wakurungezi amestaafu na kuagwa rasmi huko Mbweni, Bagamoyo.
Mojawapo ya mambo ambayo tutayadokeza zaidi mwaka huu ni ulazima wa mabadiliko ya Idara ya usalama wa taifa kama nilivyodokeza kwenye Unleashed-Vol.1 Licha ya manung'uniko ya hapa na pale dhidi ya RO ndani ya idara hiyo bado mgawanyo wa maslahi unazidi kujaa na hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu.
Mmojawapo ya vyanzo vya kuaminika vinadokeza nia na kusudio la idara hiyo na wapambe wake kuhakikisha kuwa vyovyote itakavyokuwa hakuna challenge ya maana ambayo Rais JK ataipata toka ndani ya CCM kwani taarifa zimeshakusanywa za kutosha dhidi ya wale wote wanaotaka nafasi hiyo kupitia CCM na "mafaili" yao yatavutwa pale ambapo watajionesha wanakusudia kweli kweli kumpa changamoto JK.
Natumaini Enigma na wenzake wakimaliza ripoti yao ya Silaha Haramu tutapata update ya uhakika ya nini kinaendelea ndani ya idara hii.
Kwa mara nyingine, tunatoa shukrani kwa niaba ya taifa kwa mzee wetu wa TISS aliyestaafu kwa kulitumikia taifa kwa muda wote huu na kama ada na sheria Jina lake haliwezi kutajwa kumlinda yeye na familia yake. Huyo aliyeingia toka Ubalozini ameshazua manung'uniko kwani wapo ndani ya Idara watu wanaolalamika kurukwa tena vyeo hivyo kama ilivyotokea alipoteuliwa RO mwenyewe..