GE2025 Mwinyi awashauri wapinzani wake wajikite kwenye umakamu wa kwanza

GE2025 Mwinyi awashauri wapinzani wake wajikite kwenye umakamu wa kwanza

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewashauri baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kuendelea kushindana kwenye nafasi ya makamu wa kwanza wa rais badala ya kutumia kivuli cha kugombea urais bila malengo ya kweli.

Soma zaidi: Cheo cha Umakamu wa kwanza wa Rais Cleopa Msuya kuna wenzangu tulitatizika



Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu za kuomba uteuzi katika ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar baada ya kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu hizo, Dkt. Mwinyi amesema kauli za wagombea hao zinaashiria wazi kuwa dhamira yao si kuwania urais, bali nafasi ya umakamu.

Aidha, aliwashukuru wanachama wa CCM kwa kujitokeza kwa wingi kumdhamini, akisisitiza mshikamano huo ni ishara ya imani kubwa waliyonayo kwake kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom