Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu na ustawi wa wananchi wa Unguja na Pemba, kwa misingi ya umoja, mshikamano na maendeleo endelevu.
Amesema kuwa katika kufanikisha malengo hayo, Serikali itaendelea kuwawezesha wananchi kupitia mikopo isiyo na riba, mafunzo ya ujasiriamali, na kuendeleza maeneo ya michezo ili kuongeza fursa za ajira na kuinua kipato cha wananchi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Oktoba 6, 2025 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwale, Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni kisiwani humo.