Mwinyi Zahera amkataa Kakolanya Yanga

Ila huyo benno anasema ela ya kusajiliwa alikuwa hajalipwa , kama ni kweli sidhani Kama kuna mchezani mungine yanga Anadai ela ya kusajiliwa isipokuwa yeye benno. Kama ni kweli iundwe Kamati ndogo ya kuchunguza ili suala lisawazishwe
Mpira ni ela ukiondoa Ameture league za mchangani, wachezaji wana sacrifice kwa asilimia kubwa kuliko kocha.Tatizo la wachezaji wa Tanzania nidhamu kwao ipo pembeni sana na hii inachangia kuporomoka kwa viwango. Ila kwa tamati kocha yupo sawa kusimamia nidhamu
 
Ni kweli Yanga ni zaidi ya Beno ila ujue mpira ni maisha yake.
Wewe uko kwako wanao wanakula kutokana na jasho lako ila jasho la beno unaona halina maana sio.
Mkuu Kocha Mwinyi zahera amemkataa Kokolanya kutokana na njia aliyotumia kudai maslahi yake. Maana aliondoka usiku wa manane huku kesho yake timu ikitakiwa kucheza mechi na yeye akiwa tegemeo namba 1 golini. Sasa huo ndio usaliti. Ingekuwa kwenye military adhabu yake ni kifo.
 
Kakolanya hana hisa Yanga, ni kama watumiaji wa mitandao ya simu. Mpira sio kuchumbia mke/mpenzi ni kazi kama kazi nyingine ndiyo maana mmeweka nae mkataba. Kinachohitajika ni commitment ya kazi. Ndiyo maana mchezaji anaweza kuipenda Simba lakini akachezea Yanga kwa nguvu na juhudi kwa kuwa ndiyo maisha. Hivi hawa wachezaji wa kigeni wanazipenda timu za Tanzania kama sio pesa?
Mpeni mapesa yake mishahara na pesa ya usajili. Huu ujinga ndiyo uliotufikisha hapa kama taifa sio tu kimichezo hata kisiasa na kiuchumi.
 
Baada ya mechi ya leo na mapumziko kesho Benno Kakolanya asiporudi Yanga itakuwa jambo la ajabu sana. Viongozi wa Yanga wanamsapoti na kocha atakula matapishi yake apende asipende.
Itatangazwa wamefikia makubaliano.
 
Mpira wa bongo bhana kwahiyo mchezaji akidai haki yake asipoipata afanyeje?? Kashatumia mbinu zote za ndani ya klabu zimeshindikana afanyeje?? Mbona mnaangalia upande mmoja tu.... Ndio maana soka la Tanzania haliendelei mmekalia maneno maneno matupu huku mpira umewashinda. Hyo Yanga unayoingelea humu utadhani imewahi beba CAF vile kumbe wasindikizaji tu.

Kama washabiki wote wa Yanga wana reason hivi basi mpira wetu una safari ndefu sana.
 
Ukiona wanajeshi wanaelekea vitani fahamu ela imeshaingia mfukoni .. hawaendi kutoa maisha yao lehani kukulinda wewe bure tu never.
Cha msingi wakae wayamalize..kama kocha kasimamia nidhamu sawa ila uongozi mzima wa Yanga usijifiche kwenye kivuli cha nidhamu wawajibike.
 
Beno alikera kila mtu Yanga. Je, mechi alizokacha kucheza kama timu ingefungwa hao mashabiki wako unaosema watasemaje?

Mashabiki wa Yanga wanafahamu kisa chote cha hali ya ukata kikosini Yanga ndiyo maana wanamshangaa Zahera anawezaje kupata matokeo haya inayopata Yanga. Hakuna shabiki atakayemnyooshere Zahera kidole cha ubaya timu ikifungwa kwa kukosekana Beno badala yake watajikita kwenye basic cause ya problem.
 
Isitoshe, huwezi kuwa na mchezaji tena kipa mwenye wakala mwenye kadi ya Simba. Siku Beno akifungwa hata kwa bahi mbaya kwenye mechi muhimu mashabiki watasema ameuza mechi kwa manufaa ya simba. Ni heri akwende akapunzikie kwingine na ikiwezekana hukohuko Simba japo atakwenda kugombania namba
 

Ni wazi hujui usemalo..Hapa nadhani ni suala la upeo na uelewa wa masuala ya kijamii...Hujaeleza hapa ni mbinu gani hizo ambazo Beno ametumia ndani ya klabu kudai haki zake...Yote kwa yote mbinu aliyoitumia kususia mazoezi na timu kwa ujumla ni ya kipuuzi kabisa...Na mtu anayeunga mkono mbinu aliyotumia Beno ya 'kususia' hapana shaka naye ana matatizo makubwa katika uelewa wake wa masuala ya kijamii...Hapa haina maana kuwa viongozi wa Yanga wako sahihi katika suala la Beno, La hasha...uongozi nao una matatizo yake, lakini solution kwa Beno siyo 'kususia'
 

Ni wazi hujui usemalo..Hapa nadhani ni suala la upeo na uelewa wa masuala ya kijamii...Hujaeleza hapa ni mbinu gani hizo ambazo Beno ametumia ndani ya klabu kudai haki zake...Yote kwa yote mbinu aliyoitumia kususia mazoezi na timu kwa ujumla ni ya kipuuzi kabisa...Na mtu anayeunga mkono mbinu aliyotumia Beno ya 'kususia' hapana shaka naye ana matatizo makubwa katika uelewa wake wa masuala ya kijamii...Hapa haina maana kuwa viongozi wa Yanga wako sahihi katika suala la Beno, La hasha...uongozi nao una matatizo yake, lakini solution kwa Beno siyo 'kususia'
 
Mkuu hili suala la Beno ni la muda mrefu sana sio la mwezi huu au uliopita amekuwa akilalamikia kuhusu pesa zake za usajili.... Keshaenda sana kwa uongozi kufuatilia ashafika kwa wadau kibao tu wa Yanga kuwaeleza suala lake lakini halijazaa matunda ndio mimi nauliza MLITAKA AFANYEJE?? Aendelee kulalamika tu mpaka lini??

Shida mkuu mnaangalia upande mmoja.... Mie sio shabiki wa mpira wa bongo kwa mambo kama haya sasa mtu anadai haki zake watu badala mumtafutie suluhu kama alivyofanya Musiba mmekalia kusema atimuliwe cjui hana nidhamu

Sasa ningeomba mkuu unieleze ingekuwa wwe ndio mshauri wa beno baada ya kukutaarifu kuwa kapita ngazi zote kama utaratibu unavyotaka ndani ya klabu na hajapata haki yake je ungemshauri afanyeje na hapo anavyoongea na wewe ana madeni na familia inamtegemea kwamba pesa inahitajika sana kwa wakati huu.

Nahitaji objective Situational analysis! Usiongozwe na mahaba ya Yanga.
 
Bongo bhana inaonekana hata basics za corporate management hatuna.... Yaani ndio nyie mliehoji kubenea anaishutumu vp serikali kumteka saanane ilihali gazeti lake la mwanahalisi limeripoti kuwa Saanane kaonekana kijiweni kwake!!

Jamani tutenganishe menejimenti na maisha binafsi ndio maana Courtois alipokuwa chelsea alipelekwa mkopo Atletico madrid na mechi ya Nusu fainali atletico walikutana na chelsea ila bado Atletico walimtumia Courtois golini na hakukuwa na hizi kelele kuwa atahujumu timu na mwishowe atletico wakaitoa chelsea!!

Sasa nyie bongo mngekubali kweli kipa mliyemtoa Simba kwa mkopo adake mechi ya yanga vs simba?? Ndio sembuse wakala mnaona big deal hivi

kwa aina hii ya mashabiki Mpira wa bongo kuendelea inahitaji muujiza
 


Unataka objective solution???!!!....Ok...utaipata hapa...Lakini awali ya yote ondoa fikra kwa kitu kinaitwa eti 'mpira wa bongo'...hoja hapa siyo 'mpira wa bongo'..suala hili linagusa mambo mbalimbali kiuongozi na kijamii...Halafu pengine let me declare my interset ...mimi nimecheza mpira na kubahatika kuongoza soka kwa ngazi za 'juu' kabisa.nchini...kwa hiyo suala la uendeshaji wa soka nchini lipo kiganjani mwangu...saikolojia ya wachezaji wa hapa kwetu naifahamu vizuri...uelewa wa wachezaji naufahamu sana...'umafia' katika soka nchini mwetu naufahamu sana...saikolojia ya mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania ...situation katika masuala ya uongozi wa soka Tanzania naifahamu fika...In short wachezaji wengi wa Tanzania hawana uelewa wala elimu ya kutosha ..uelewa wa masuala ya soka na elimu yao ni duni kwani wengi hawajasoma au kuingia darasani ...Kwa hiyo wachezaji wengi huburuzwa buruzwa tu..Beno yuko sahihi kudai kile ambacho hajapata...Lakini alichokosea ni kususia ...yeye ni mjinga na sisemi kuwa ni mpumbavu ..Hana uelewa wa masuala yake...anadanganywa na kudanganyika...Kama uongozi wa Yanga umeshindwa kutekeleza mkataba kwa mujibu wa maelewano alichopaswa kufanya ni 'kuushikisha adamu uongozi' kwa kuuburuza katika ngazi husika...iwe ni huko TFF au wizarani au Baraza la michezo kama linahusika na baadaye ikishindana anakwenda arbitration court ya FIFA au ngazi yoyote ile ya FIFA inayohusika...kususia kucheza mpira ni ujinga wa kiwango cha hali ya juu....kwanza anaua kipaji chake, pili anajenga maadui ndani ya Yanga, tatu kwa kususia fedha hizo hawezi kupata, nne akirudi Yanga hawezi kuaminika tena kutokana na mazingira yaliyopo, tano amemuweka wakala wake ambaye ni Simba katika hali ngumu kwani fikra zilizopo ni kuwa ameshinikizwa na wakala wake ingawa inawezekana siyo kweli..na kwa upande mwingine inawezekana ni kweli ikizingatiwa suala la 'umafia' wa soka nchini.

Ndugu yetu Musiba hajafanya jambo jema kumpa pesa huyo Beno..kwa kufanya hivyo amechochea mgawanyiko ndani ya timu kwani wapo wachezaji ambao wana madai yao kama Beno...Huyo Beno akirudi kwenye timu wachezaji wengine wanaweza wakacheza chini ya kiwango ili Beno afungwe mabao mengi na aonekane kuwa hafai...Nina hakika kabisa wako wachezaji wa Yanga ambao wanamuona Beno hana maana kwa uamuzi aliouchukua
 


Unataka objective solution???!!!....Ok...utaipata hapa...Lakini awali ya yote ondoa fikra kwa kitu kinaitwa eti 'mpira wa bongo'...hoja hapa siyo 'mpira wa bongo'..suala hili linagusa mambo mbalimbali kiuongozi na kijamii...Halafu pengine let me declare my interset ...mimi nimecheza mpira na kubahatika kuongoza soka kwa ngazi za 'juu' kabisa.nchini...kwa hiyo suala la uendeshaji wa soka nchini lipo kiganjani mwangu...saikolojia ya wachezaji wa hapa kwetu naifahamu vizuri...uelewa wa wachezaji naufahamu sana...'umafia' katika soka nchini mwetu naufahamu sana...saikolojia ya mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania ...situation katika masuala ya uongozi wa soka Tanzania naifahamu fika...In short wachezaji wengi wa Tanzania hawana uelewa wala elimu ya kutosha ..uelewa wa masuala ya soka na elimu yao ni duni kwani wengi hawajasoma au kuingia darasani ...Kwa hiyo wachezaji wengi huburuzwa buruzwa tu..Beno yuko sahihi kudai kile ambacho hajapata...Lakini alichokosea ni kususia ...yeye ni mjinga na sisemi kuwa ni mpumbavu ..Hana uelewa wa masuala yake...anadanganywa na kudanganyika...Kama uongozi wa Yanga umeshindwa kutekeleza mkataba kwa mujibu wa maelewano alichopaswa kufanya ni 'kuushikisha adamu uongozi' kwa kuuburuza katika ngazi husika...iwe ni huko TFF au wizarani au Baraza la michezo kama linahusika na baadaye ikishindana anakwenda arbitration court ya FIFA au ngazi yoyote ile ya FIFA inayohusika...kususia kucheza mpira ni ujinga wa kiwango cha hali ya juu....kwanza anaua kipaji chake, pili anajenga maadui ndani ya Yanga, tatu kwa kususia fedha hizo hawezi kupata, nne akirudi Yanga hawezi kuaminika tena kutokana na mazingira yaliyopo, tano amemuweka wakala wake ambaye ni Simba katika hali ngumu kwani fikra zilizopo ni kuwa ameshinikizwa na wakala wake ingawa inawezekana siyo kweli..na kwa upande mwingine inawezekana ni kweli ikizingatiwa suala la 'umafia' wa soka nchini....Halafu hivi unadhani kwenye mkataba wa Beno kuna kipengere kinasema asipolipwa eti anaruhusiwa kugoma au kususia???!!!

Ndugu yetu Musiba hajafanya jambo jema kumpa pesa huyo Beno..kwa kufanya hivyo amechochea mgawanyiko ndani ya timu kwani wapo wachezaji ambao wana madai yao kama Beno...Huyo Beno akirudi kwenye timu wachezaji wengine wanaweza wakacheza chini ya kiwango ili Beno afungwe mabao mengi na aonekane kuwa hafai...Nina hakika kabisa wako wachezaji wa Yanga ambao wanamuona Beno hana maana kwa uamuzi aliouchukua
 
Zahera aache umama..yeye analipwa na Congo DRC faranga za kutosha...Beno ana mtoto,mama yake amestaafu kazi...hao wote wakale wapi??Nampenda Chief Coach Zahera ila hapa kachemka mbaya...mrudishe Benno au siku zako za kukaa Jangwani zinahesabika...huyo Kabwili magoli mengi anayofungwa Beno hafungwi....mtoto akinyea mkono...........
 
Beno kakosea Sana kwenye hili, kwani anaijuwa thamani ya kukosa kucheza mechi moja bila ridhaa ya kocha wake? Anafahamu hizo mechi alizogomea kucheza zinapunguza kiasi gani kwenye hela anayoidai Yanga? Huwezi kuacha kucheza mechi bila ruhusa ya kocha halafu pesa yako ulipwe yote bila kupungua. Jee, club imepata hasara kiasi gani Kwa Beno kugomea mechi? Je Yanga ingepata hasara kiasi gaini kama wachezaji wote wanaodai wangefuata nyao za Beno kususia mechi?
 
Sasa alivyogomea mechi kama timu ingefungwa kwaajili yake ungesema nn? Kila mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…