Ila huyo benno anasema ela ya kusajiliwa alikuwa hajalipwa , kama ni kweli sidhani Kama kuna mchezani mungine yanga Anadai ela ya kusajiliwa isipokuwa yeye benno. Kama ni kweli iundwe Kamati ndogo ya kuchunguza ili suala lisawazishweKwa upande mwingine uko sahihi kwamba matokeo yakianza kuwa hasi kwa Yanga upepo utabadilika...lakini hii ni kwa dunia nzima kwani hii ndiyo saikolojia ya mashabiki wote wa soka duniani..lakini kwa ujumla wake kocha Zahera yuko sahihi kabisa.Huwezi kumkaribisha mchezaji aliyegoma..kwani mwenye matatizo ya kucheleweshewa malipo siyo Beno peke yake...wachezaji kadhaa wa Yanga wana madai yao...sasa Beno alifanya hivyo kwa kuwa alivimbishwa kichwa yeye ndiye kipa bora kwa Yanga na kwamba ni lazima atingishe kiberiti kwa kugoma...ni jambo baya sana...yaani waandishi wa habari wanaowadai mishahara kadhaa waajiri wao wagome kwenda kazini!!! Halafu wafanyakazi wa taasisi za ummawenye madai yao wagome kwenda kazini...haiwezekani...alichofanya Kakolanya ni upuuzi wa kiwango cha juu...hisia zangu zinanituma niamini kuwa Beno alishawishiwa afanye hivyo na meneja wake ambaye ni kiongozi wa Simba kwa lengo la kuihujumu Yanga...Yanga kamwe wasikubali Beno arudi Yanga, aende huko huko ikibidi aende Simba...Yanga mwaka 1976 iliwahi kufukuza wachezaji wote wa kikosi cha kwanza na kuanza upya, mwaka 1977 ilifunggwa 6-0 na Simba lakini Yanga haikufa moyo....iliendelea kujijenga na mwaka 1981 Yanga ikajikomboa kwa kuichapa Simba goli 1-0 kwa bao la Juma Mkambi.....
Mpira ni ela ukiondoa Ameture league za mchangani, wachezaji wana sacrifice kwa asilimia kubwa kuliko kocha.Tatizo la wachezaji wa Tanzania nidhamu kwao ipo pembeni sana na hii inachangia kuporomoka kwa viwango. Ila kwa tamati kocha yupo sawa kusimamia nidhamu