Mwinyi Zahera ni kocha bomu

Mwinyi Zahera ni kocha bomu

weka thamani ya kikosi cha zesco kisha weka thamani ya kikosi cha yanga... ukiongezea na mishahara wanaolipwa wachezaji wote ..

kisha weka gharama za kikosi cha timu za Tanzania simba na azam na mishahara wanayolipwa...kisha weka na yanga..

tutajua kocha bomu ni nani
Kwa hiyo guardiola ni kocha bomu kwakuwa kafungwa na kocha wa norchwich yenye bajeti ndogo??
 
Weka na kikosi cha Ud songo au kikosi cha mashujaa
 
Kwa hiyo guardiola ni kocha bomu kwakuwa kafungwa na kocha wa norchwich yenye bajeti ndogo??

guardiola hafungwi kila siku..

kwa timu yenye kikosi cha bei nafuu.. mishahara ya wachezaj nafuu na hawalipwi kwa wakati... kocha aliyeweza kuifanya timu maskini kumaliza ligi ya pili ni kocha mzuri.. kocha alieifanya yanga mpaka leo bado inacheza champions league ni kocha bora.. timu kibao zimetolewa wakiwemo wenye kikosi cha mabilioni
 
Kwa

Kwa hiyo zahera ni bora kuliko kocha wa mabilioni???
 
Yanga kombe letu ni klabu bingwa afrika au shirikisho afrika, hilo kombe la mchangani vodacom simba tangazeni ubingwa hata mwezi huu sisi yanga hatulitaki tumeshachoka kulichukua
Nimekuelewa...kwa hio unasubiri mbeleko tena mwaka huu ili mwakani ucheze klabu bingwa. Akili nyingine buana
 
Ila tumpe muda Zahera kama Simba walivyoitengeneza timu kwa miaka 5 then baadae wakabeba ubingwa na kufika robo fainali ya CAF.
Kama Simba walitengeneza timu mbona sasa ni watazamaji tu? Uzuri wao uliishia wapi? Mi nawashauri Simba wanunue sana mechi ili mwakani warudi, au wajitahidi kwenye FA, wajihadhari na Green Worriors na Mashujaa.
 
Nimekuwa nikimfuatilia Kocha Mwinyi Zahera tangia ajiunge na Timu ya Yanga Mwishoni mwa msimu wa 2017/18. unaweza kusema amepata mafanikio kiasi ikiwemo kuifanya Timu yake kushika nafasi ya Pili mara mbili mfululizo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na ikiwemo kuwa Kocha Bora wa Mwezi Desemba 2018 na Januari 2019.

Hata hivyo Kocha huyu ana tatizo katika mbinu zake. Ni muumini sana wa mtindo wa kujilinda. Tuliona mechi dhidi ya Simba kwenye Ligi Kuu msimu uliopita. Mechi ya kwanza walifanikiwa kulinda ipasavyo na mechi kuisha 0-0 na kwenye mechi ya Pili walilinda vyema kabla ya kuruhusu goli dakika ya 70 na kuishia kufungwa 1-0 na Simba.

Leo tarehe 14 Septemba 2019, ameiongoza Yanga katika mechi ya Tatu Kimataifa kwa kucheza mechi ya Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ZESCO United ya Zambia. Katika Mechi hii Zahera ameonyesha wazi alivyo muoga. Amechezesha mfumo wa 4-5-1 huku akiwa na mabeki asilia 3, Yondani, Moro na Ally Sonso japo alikuwepo Mapinduzi Balama ila huyu ni Kiungo. Akachezesha wachezaji 5 wa Viungo na Fowadi mmoja Sadney Khotage Urkob peke yake.Huu ni woga mkubwa aliounyesha. Nina imani angecheza na Washambuliaji wawili au watatu pengine timu yake ingepata matokeo yaliyo tofauti na waliyopata leo.

Mchezaji kama Sibomana alikuwa out of form kabisa leo. Ukiachana na lile goli la penati hakuwa na mchango wowotw wa maana. Nilidhani angeweza kutoka Sibomana akaingia Ngasa huku pia ukiwa na Kalengo pamoja na JUma Balinyya au Sadney ili kuimarisha pacha ya Usshambuliaji.

Mashabiki wa Yanga wanaweza kuamua wenyewe hata hivyo, sisi kazi yetu ni kutoa tathmini tuu.
TEAM YAKO IMETOLEWA NA UD SONGO ...UD SONGO team mbovu umetolewa ...yanga ipo ipo sana ...huo ushauri ungempa kocha wenu wa simba ...kutwa kumuwaza zahera na yanga .............UD SONGO amewatia kiwewe
 
Back
Top Bottom