Mwisho Mwampamba kufukuzwa Namibia

Ruzibiza

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
563
Reaction score
123


STAA wa Shindano la Big Brother, Mwisho Mwampamba, amesikitishwa na vitendo vya ubaguzi alivyofanyiwa na Polisi wa nchini Namibia, anakoishi na mkewe, Meryl Shikwambane, ambapo walimfuata kwenye nyumba yake na kumtaka aondoke nchini humo.

Mwisho ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akisema nchi hiyo sasa hivi imekuwa kama Afrika Kusini, ambako wageni, hasa wenye ngozi ya Kiafrika, hupata shida ya kuishi kutokana na kubaguliwa.
"Mimi nimeoa mtu wao na nimezaa naye mtoto, nashangaa kubaguliwa na polisi hao, pia inashangaza kuona
wakiwahudumia vyema wageni kutoka barani Ulaya, lakini sisi Waafrika wenzao tunabaguliwa," alisema Mwampamba.

Mkali huyo ameshangazwa kupewa hati ya kuishi nchini humo kwa miezi miwili pekee, wakati ameoa mwanamke wa
nchi hiyo, huku akipata shida hiyo hata mipakani.
 
Isije ikawa kwa ajili ya bwax aka Gambe maana huyo ndugu mzuri kwa ku pombeka!
 
Huenda Mwisho mwenyewe ndio matatizo, mbona huko kuna wabongo kibao na hawabaguliwa,ila huko ni kawaida kwa machotara kudhauriwa na wale wasio machotara kwani mbele ya jamii ya Kinamibia,machotara ni watu wasio na asili,na wapo machotara wengi sana huko Namibia
 
Hahaaa si Ana ngozi nyeupe huyoo au mixed sasa shida ni nini? Aache Kulia lia na mibange yake
 
Operation kimbunga hiyo. When you live in glass houses.....
 
Njoo TZ na mkeo huyo kama kweli mna ndoa halali kisheria. Isije ni kuzaa naye tu ndo anatumia kama kigezo cha kuishi kwa watu. anaweza kuwa mhamiaji haramu huko.
 
toka ukweni uko urud kwenu. ata tz imefukuza wahamiaj haramu.
inasikitisha mtu kama mwisho kuishi ukweni bila vibali
 
Mwisho ndio alimfanya ray C abwie unga. na haoni tatizo kuwaharibu watoto wa watu. kufukuzwa huko kuna jambo sema hawezi jiongelea mapungufu yake. mia
 
Operation kimbunga hiyo. When you live in glass houses.....
Nilishajua kuletwa post hii hapa jamvini kuna lengo fulani - birds of a feather...., hii inadhilisha kwamba Operation Kimbunga iliwashika pabaya waliokuwa na ajenda zao. Bravo JK na wana usalama wetu kwa kazi yenu iliyo tukuka, sina shaka wahamiaji haramu watafikilia mara mbili kabla hawaja tia mguu tena Tanzania, fuateni taratibu na sheria za uhamiaji kama mna nia nzuri ya kuomba uraia/hamia Tanzania - lakini mkileta mambo ya kugehuza nchi za wenzenu shamba la bibi mtapata fundisho la mwaka. Kumbuka zoezi hili ni endelevu, tumekwisha washtukia.
 

Kama kazi utakuwa nayo, shamba utakuwa nalo, pesa utakuwa nayo sina shaka.. ila umekosa kitu kimoja nacho ni zaidi ya pesa, shamba nk....kitu hicho si kingine ni ......AKILI

Hivi wahamiaji walikufanya nini?mbona unakuwa na chuki za ajabu ajabu?una bahati hujawahi kutoka nje ya bukoba/muleba.....waulize walokwisha toka nje ya nchi wakueleze kubaguliwa ni nini?
 
Mkuu nilisha eleza mara nyingi humu kwamba sisi hatuna chuki na kabila lolote kutoka Rwanda, mbona walianza kuhamia mkoani Kagera kama wakimbizi tangu miaka ya hamsini wakaishi na wenyeji bila labsha, tatizo limekuja kuhibuka miaka ya hivi karibuni katika current Administration ya nchini mwenu, mtu ukiangalia jinsi mnavyo ji-conduct mnapo kuwa ugenini ni majanga kabisa kuanzia kwenye: Uharibifu wa mazingira with impunity, kuteka magari na kuuwa raia wasio na hatia, kujaribu kuhodhi/pora aridhi za majirani zenu by hooks&crooks nk - ni binadamu gani mwenye akili timamu anaweza kuvumilia vitimbwi vyenu 4ever! Nani, tell me? Yaani mnataka ku-emulate adithi za Mwarabu mwenye hema na Ngamia wake. MKuu kumbuka kinacho zungumzwa hapa ni uhamiaji HARAMU repeat HARAMU na si kitu kingine, tatizo lenu mko mahiri sana kugeuza maneno na kurudia rudia adithi hizo hizo miaka nenda rudi - dunia imekwisha shitukia/choshwa na mbinu zenu zilizo kwisha pitwa na wakati !! Nimalizie kwa kusema kwamba nimeona hapa umejaribu kutusema mambo mengi -ve, lakini inapokuja kwenye Dept ya AKILI nataka kukuhakikishia kwamba Watanzania tuna akili nyingi ndio maana tuliweza kuwa-nip in the bud i.e timely wahamiaji wote haramu kabla hawaja import vurugu zao ndani ya Taifa letu. Mwisho, wewe unajuaje kama sijawahi kutembelea mkoa wowote zaidi ya Bukoba mjini na vijijini, unajuaje kama sijawahi ku-encounter RACISM katika maisha yangu, mkuu hakuna binadamu anayependa kubaguliwa, vile vile hakuna Taifa lolote linaweza kuruhusu wageni waishi nchini mwake bila kibali, alafu wakihojiwa wanaleta mambo ya kutishia maisha, dharau, viburi na kufokea watu wazima kama watoto.
 
Njoo TZ na mkeo huyo kama kweli mna ndoa halali kisheria. Isije ni kuzaa naye tu ndo anatumia kama kigezo cha kuishi kwa watu. anaweza kuwa mhamiaji haramu huko.

Kwani yuko Jf nae?
 
Kweli ukiwa nchi za watu ukajifanya wewe mtoto wa mjini mvunja sheria lazima wakumind tu hata ikiwezekana kuwa deported, uwe umeoa ama la!

Am 98% sure huyu Mwisho ana tatizo ndio maana wamemkomalia, arudi tu
 
hizo ndo taabu za kupenda vya mteremko, hangaikeni vijana mpate vyenu siyo mnapenda kuhudumiwa
 

Mwambie huyo maana kauli yake ni km mtu mwenye jiografia ya kuku,atembee aone,aende hata msumbiji tu.
 

Haaa haaaa inauma eeh...! AKILI ya kuishi kiharamu nchi za watu?
 

wewe humuwakilishi mtu yeyote hapa kwenye mjadala nadhani unakosea kusema "ninawaita" u'd rather stand on your feet....
CHUKI SI DHAMBI YA ASILI UNAWEZA KUITENGENEZA WAKATI WOWOTE SIYO LAZIMA KUZALIWA NAYO....maumivu nayopata Mwisho ungekuwa wewe chuki zako hizo zingeisha...it is apparent hujatoka nje ya BK,maana hakuna mtu mwenyeuzoefu wa kukaa kwa watu atashadadia upuuzi kama huo....Go to Spain and see what is happening....siku moja inatosha tu kujifunza.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…