Mwisho wa Diamond umekaribia, ilikuwa lazima aanguke

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,932
Reaction score
4,544
Kati ya mambo ya kijinga kabisa ambayo Diamond ameyafanya ktk maisha yake ni kumdharau baba yake mzazi eti kisa alimtelekeza kumlea na mama tu ndo akamlea,ni kweli baba yake alikosea sana,lakini ndugu zangu nataka mfahamu kuwa,mzazi wako ni mzazi wako tu,hata kama ni chizi,hata kama ni katili.

Diamond kazungukwa na kundi la watu wahuni wasiomshauri vyema, alimpatia marehemu Gurumo gari wakati baba yake hana hata baiskeli, huwezi kufanikiwa bila baraka za wazazi wote, kama Diamond anamdharau baba yake wa kumzaa,basi arudi tena kwenye udongo ili akazaliwe na baba atakayekuja kumheshimu. Sasa hivi ameandamwa na mikosi ya kila aina, wajinga wanalaumu watanzania wengine kwa matatizo ya Diamond, wamesahau kuwa kijana huyu kila uchao,baba yake mzazi anasononeka,akimuona mwanae anakula bata wakati yeye hata kula yake ya siku ni shida.

Anguko la Diamond limefika,hana baraka za baba, kwa hiyo hawezi kusonga mbele hata kama taifa zima litamuombea, DIAMOND KAMUANGUKIE BABA YAKO, OR ELSE YOU'RE GONE AWAY.
 
Oyaa wachie watu na maisha zao..kwanza huyo diamond wako wengne hatumfahamu
 

Usilolijua litakusumbua, Diamond na babake anayejua ni yeye na mama yake. Kama laana za baba yake asingefika alipo sasa. Diamond amefanikiwa sana, na pia kumbuka hamna kitu ambacho kitakuwa juu siku zote. Lazima ushuke siku moja. Wazungu wanasema, it's better to make hay while the sun shines. Nina uhakika Diamond kishafanya hicho kitu. Yaani ameshachuma. Hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Halafu nyie wanaume ma sperm donner,msifikirie kutoa mbegu ni kazi,kazi ipo kwenye kulea.Kama Diamond atashuka kimziki basi muda wake utakuwa umefika.Baba yake wala siyo sababu kabisa.Kama yeye hakumlea mwanae pindi alipomuhitaji iweje leo Diamond amlee.Hata Obama hakutoa chozi alipopigiwa simu baba yake mzazi kafa,ila kaja kuwa Raisi.Laana haipo kwa baba ambae hakukujali pindi ulipomuhitaji
 

Kama huyo baba yake anapenda damu yake kwa pesa tu ina maana hata huyo daimond akimsaidia kwa sasa na siku diamond akifirisika bado atawakana tu na kwanini huyo diamond alivyokuwa hajafanikiwa baba yake hakumuitaji?? Ebwanae hiyo laana itampata huyo mzee alieikana familia na sio diamond.kumbuka mzazi asieitunza familia ni mbaya kuliko SHETANI na laana ishaanza kumpata huyo mzee kwa ujinga wake alioufanya.Mzee nakushauri nenda itv kamwombe mwanao msamaha ili wazee wenye tabia mbaya kama yako wajifunze kupitia kwake.Hukutumwa na mtu kumtongoza huyo mama ukamzalisha kisha ukajifanya uko bize na wanawake wengine,haya endeleeni kupendana.Unakula ulichopanda mzee na wewe uliendika thread hii usikubali mtu akutumie vibaya bali uwe mshauri mzuri kwa kuwafanya watu wajutie makosa yao.
 

Unapojaza form za Immigration wakati unaingia ktk airpot ya Sudan..Khartoum(waliotua Sudan wanalijua hilo), swali mojawapo unaloulizwa ni jina la mama yako mzazi…hawaulizi jina la baba yako..Na inaleta maana labda sababu utakuaje na uhakika kuwa the so called your dad is really your biological dad?? lakini ni %100 kuwa that is your biological mother
 
Wewe mtoa mada ujui ulitendalo,wakati baba yake diamond tajiri na diamond akiwa anaishi chumba na mama yake uswahili hakuwa na msaada wowote kwa mtoto.

Kama wewe ni baba na umetelekeza mtoto siku mtoto maisha yakiwa mazuri usisogee kabisa.

Diamond yuko sawa.Malipo ya utelekezaji familia utalipwa umu umu duniani.
 

Mkuu kumbuka kuwa kuna akina mama wengine wanaiba watoto hivyo usiseme 100% ila sema kwa asilimia kubwa.
 
Kutoa mbegu sio kaz,apo ckubaliani na wewe hata kidogo!
Naona kama ww ulizaliwa bila bb
 

Sio kweli kuwa kutoa mbegu ni kirahic kiivyo ..lol
 

yaani hapo ndipo shida sana.
kiukweli kuzazi cha Leo kimeharibika sana.na hawa wenzetu wamagharibi ndio wametuharibu na kutupotosha kabisaaa.
kiukweli jamaa kafanya kosa kama kweli kamtelekeza baba yake.yaani hata PATA dhwawabu kwa mwenyezi mungu kwa kumhudumia mama yake Bali kwa babaye.
najua nivigum kunielewa Bali ukweli ndio huo.kitendo cha kumludia baba yake nakumpigia magoti kiukweli atakuwa kamludisha kondoo mpotevu bandani..
maana baba yake atatambua kosa atajuta na kuomba heri na msamaha kwa mwenyezi mungu.
na kwamwanae.

tatizo hili suala lipo kwenye vipengele kama v3 hv udini ,kiutandawazi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…