Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
"Semina, warsha sasa kwa kibali cha ofisi ya Waziri Mkuu
Na Habel Chidawali,Mpwapwa (Mwananchi)
Maoni yangu:
Mambo mengine yanashangaza sana lakini pia yanatuonesha kuwa jinsi "tulivyo". HIvi kabla ya agizo hili hii mikutano, warsha, na semina zilikuwa zinafanywa kwa taratibu gani hadi kusababisha watu kutumia mambo hayo kujitengenezea fedha? Angalau ni hatua muhimu.
Hata hivyo swali ni jinsi gani serikali itapima mafanikio ya maagizo haya? Vipi kama kila warsha na semina wanayoomba ina lengo zuri, jina zuri na inayohitajika kwa watumishi?
Ni vizuri kuweka vigezo wazi kabisa vya makongamano, semina na warsha; lakini wakati huo huo kutorudisha maamuzi muhimu kwenye idara na ofisi za sserikali mikononi mwa Waziri Mkuu kwani ni kurudisha ukiritimba usio wa lazima.
Na Habel Chidawali,Mpwapwa (Mwananchi)
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameingia kwenye orodha ya viongozi waliojaribu kupiga vita semina na warsha kwa taasisi za serikali baada ya kuzipiga marufuku kwa kile alichoeleza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Tamko kama hilo limeshawahi kutolewa na viongozi kadhaa wa juu wa serikali zilizopita bila ya kuwa na mafanikio, lakini Pinda amekwenda mbali zaidi kwa kuzitaka wizara zitakazotaka kuandaa semina, warsha au kongamano kuomba kibali kutoka ofisi yake.
Pinda alitoa tamko hilo juzi kwenye viwanja vya Mteteja wilayani Mpwapwa alipokuwa katika ziara ya siku ya tano mkoani Dodoma na akaweka msisitizo zaidi kwa kusema atalisimamia agizo hilo kwa nguvu zake zote.
Alisema kuwa kuanzia sasa hakuna wizara itakayofanya semina au warsha na makongamano bila ya kibali cha ofisi yake. Alisema ofisi yake itatoa kibali baada ya kupata maelezo sahihi kuwa semina au warsha inalenga nini na kwa faida ya nani.
Pinda alisema kuwa fedha zinazoteketezwa kwenye makongamano, semina na warsha hizo ni nyingi sana kiasi cha kuweza kusaidia katika miradi mingine yenye tija kwa wananchi wa Tanzania.
Alisema ameshaagiza wizara zote kumpa bajeti zao katika ofisi yake ili
aweze kuzipitia kabla ya kuruhusu makongamano hayo kufanyika popote na kama ataruhusu basi hiyo itaonekana kuwa ina faida kubwa wa wananchi.
Waziri Pinda aliendelea kueleza kuwa wizara nyingi hazijampa bajeti zao lakini akabainisha kuwa moja ya wizara iliyompa bajeti yake ilimstua sana kiasi cha kuwaagiza wasaidizi ake waagize bajeti za wizara zoe zinazolenga katika makongamano ili azipitie.
Alisema bajeti hiyo ya wizara hiyo ambayo hakuitaja ni Sh4 bilioni ambazo alisema hazitoshi kwa shughuli za wilaya kama zingetumika pia kwenye semina, warsha na kongamano zisingetosha na akaamua
kusimamisha mambo hayo hadi atakapotoa ushauri wake.
Unajua serikali yetu ni masikini sana lakini watu wanapanga kujinufaisha kwa kutumia makongamano na semina wao wenyewe. Sijui wakulima wa huku vijijini wanaufaikaje kama si kumuongezea mwenye nacho," alisema Waziri Mkuu na kuongeza:
"Walipoleta tu mimi niliangalia nikagundua kuwa wanataka kumaliza fedha bure hawa... nikasema NO, haiwezekani kabisa fedha nyingi kiasi hiki kutumika kwa ajli ya vitu vya namna hii wakati walipa kodi hawafaidi na kitu chochote."
Pinda alisema anafanya mpango wa kuwasiliana na rais ili kumweleza juu ya nia hiyo ya kuzuia mambo hayo na kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya mambo hayo, zitumike kununulia pembejeo za wakulima ili kuwapunguzia makali ya maisha.
Wakati huohuo, Waziri Pinda amemuagiza mkuu wa mkoa wa Dodoma kuwa mkali ili aweze kuwazuia madiwani wa mkoa huo wasiende kufanya ziara wanazosema kuwa ni za mafunzo na badala yake alisema wanatakiwa kujifunza wakiwa ndani ya halmashauri zao.
Alimweleza kuwa ni lazima ufike wakati mkuu huyo wa mkoa akaacha huruma kabisa na kutenda kazi aliyomtuma ili fedha zilizokuwa zikitumika katika ziara za mafunzo hayo, zitumike katika miradi ya maendeleo ya wananchi katika halmashauri zao.
Maoni yangu:
Mambo mengine yanashangaza sana lakini pia yanatuonesha kuwa jinsi "tulivyo". HIvi kabla ya agizo hili hii mikutano, warsha, na semina zilikuwa zinafanywa kwa taratibu gani hadi kusababisha watu kutumia mambo hayo kujitengenezea fedha? Angalau ni hatua muhimu.
Hata hivyo swali ni jinsi gani serikali itapima mafanikio ya maagizo haya? Vipi kama kila warsha na semina wanayoomba ina lengo zuri, jina zuri na inayohitajika kwa watumishi?
Ni vizuri kuweka vigezo wazi kabisa vya makongamano, semina na warsha; lakini wakati huo huo kutorudisha maamuzi muhimu kwenye idara na ofisi za sserikali mikononi mwa Waziri Mkuu kwani ni kurudisha ukiritimba usio wa lazima.