PreGE2025 Mwisho wake ni nini. Maana CCM na vyama vingine vinasema tuanaendelea na uchaguzi CHADEMA pekee inasema no reform no election

PreGE2025 Mwisho wake ni nini. Maana CCM na vyama vingine vinasema tuanaendelea na uchaguzi CHADEMA pekee inasema no reform no election

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wananchi wakiendelea kuielewa hoja ya chadema kama ilivyo sasa,hakika wanaweza kususia uchaguzi.Je hizo zitakuwa ndio fujo na furugu za chadema?Bali ni watu walioelimishwa.Mimi ningetamani serkali ikubali reforms kwa faida ya wote.Na hii haina maana kushindwa kwa ccm ktk uchaguzi.Na kama ikishindwa yatakuwa ni maamuzi ya wananchi
 
Sijajua mwisho wake nini Maana CCM na vyama vingine vinasema tuanaendelea na uchaguzi ,CHADEMA pekee inasema no reform no election.

Kibaya zaidi CHADEMA iko disquualified kushiriki uchaguzi.lakini wanaendelea na campain yao kwamba no reform no election.kwa maana hiyo siku tume huru ya uchaguzi itakapotangaza tarehe ya kapeni za uchaguzi chadema watafanya nini? vurugu? watazuia watu kwenda kupiga kura?

We need to sit down kuelewa mstakanbali wa taifa letu .hapo mbele kuna hataari ya vurugu kama za Kenya.ni vyema CHADEMA iitwe na msajili wa vyama vya siasa wapigwe marufuku kuendelea na kampain yao ya no reform no elections,au utafutwe mwafaka wa jambo hili kabla ya damu kumwagika.

Solution nyengine kama hizo mbili hazifai ,basi serikali ipi marufuku mikutano ya vyama vya siasa mpaka tarehe ya kuanza kampeni za uchaguzi ,na chadema au chama ambacho kiko disqualified kisipewe kibari cha mikutano yoyote mpaka baada ya uchaguzi

The solution would be : njoo usaini kanuni za uchaguzi ,kama hutaki kwanzia sasa hutapewa kibari chochote cha mikutano ya kisiasa .
Mkuu umeangazia tatizo badala ya chanzo cha tatizo

Pata picha
Unakwenda kwenye uchaguzi form zinatolewa J tano zinarudishwa Ijumaa...... kuanzia Alhamisi mahakimu wote hawapo ofisini kusaini form za wagombea ila CCM wanajua watapata vipi mahakimu.

Wagombea wako 80% watakao rudisha form wanaenguliwa kihuni tu kisa eti wamekosea kujaza form wakati wa CCM 100% form zipo sawa

Na katika hao 20% wataka bahatisha kupitishwa kugombea 50% watawekewa mapingamizi ya kiboya tu ili mradi

Vituo vya kupigia kura ndio balaa
Kura bandia zinaingizwa kinyemela
Mawakala wanawekewa mapingamizi kusimamia
Na bado ukishinda upinzani anatangazwa CCM kwasababu wasimamizi wa uchaguzi ni MAKADA wa CCM
Ukienda mahakamani unaangukia pua

Haya ndio mambo tunapaswa kukadili badala ya kuwalaumu wapinzani wanaopigania uwanja sawa wa uchaguzi

Tatizo ni kwamba tunadhania hilo ni tatizo la CDM
Ila ukweli hili ni tatizo zaidi kwetu wapiga kura
Kwanini kura zetu HAZIHESHIMIWI?
Kwanini tumchague Ali tukubali atangazwe John?....... hichi ndicho CDM wanapita kuwaambia wananchi kwamba kama hakuna badiliko ya uchaguzi huru nabhaki kwanini uchaguzi uwepo wa mkimchagua Ali anatangazwa John?

FUNGUA AKILI MKUU
 
kumbuka Bunge la Ulaya limewaelekeza wawakilishi wake wafuatilie hatua kwa hatua No Reforms No Election

Angalieni msijichanganye, baadae muanze kuja kulia lia misaada mnayoendaga kuomba huko ikizimwa
Akili yako yote imeishia ulaya kumbuka kuna korea kwa kiduku pia urusi
 
Wananchi wakiendelea kuielewa hoja ya chadema kama ilivyo sasa,hakika wanaweza kususia uchaguzi.Je hizo zitakuwa ndio fujo na furugu za chadema?Bali ni watu walioelimishwa.Mimi ningetamani serkali ikubali reforms kwa faida ya wote.Na hii haina maana kushindwa kwa ccm ktk uchaguzi.Na kama ikishindwa yatakuwa ni maamuzi ya wananchi
No reform ,No election mi sioni kama kuna chochote kitatokea sababu Chadema watawashawishije wananchi waelewe hoja yao ili wasusie uchaguzi
 
Back
Top Bottom