Mwisho's Defeat in Big Brother: Nigerians are Money Mongers!!

Mwisho's Defeat in Big Brother: Nigerians are Money Mongers!!

Mbona Richard ni mtanzania na alishinda???

I dont remember, hivi Richard aliingia kwenye fainali na Mnigeria? Cheki hii story:

Global Publishers:

Nyeti zaidi, zinashushwa kuwa kwa vile Uti alikuwa na uhakika kuwa ujanja aliotumia hauna shaka, hakuwa na shaka yoyote kuhusu ushindi.
Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa mtandaoni, Uti kupitia timu aliyounda Nigeria, walitengeneza mtandao katika baadhi ya nchi hasa zile ambazo washiriki wake walitolewa mapema kwa lengo la kutafuta kura zaidi.
“Waafrika wanaweza wakawa hawajui ‘triki’ aliyotumia Uti kushinda, yule jamaa alienda kuhakikisha anashinda, kwahiyo alijipanga,” ilisema sehemu ya ujumbe huo na kuongeza:
“Nchi nyingine hawana elimu hii, mtu anakwenda kuwakilisha ili kubahatisha, Uti alikwenda kufanya kazi ya kutafuta fedha.”
Inachambuliwa kupitia ‘meseji’ hiyo kuwa kila timu iliyoundwa, ilitakiwa kufanya kazi ya kutuma ujumbe wenye kumpigia kura Uti kadiri walivyoweza na kufanya uenezi zaidi nchini humo na Afrika nzima.
Inaelezwa kuwa kufuatia maandalizi hayo, Uti alikuwa na kila kitu cha kumuwezesha kushinda na ndiyo maana hakuwa na shaka.
Mbali na Miji ya Nigeria, baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimetajwa kupelekwa mtandao wake kwa lengo la kukusanya kura ni Ghana, Malawi, Uganda, Angola, Ethiopia na Zambia.
SIRI NZITO YAVUJA - Global Publishers
 
Mi sikubaliani na wewe mia kwa mia sababu kama Mwisho angeshinda angeweza kutuletea sifa Tanzania hasa kwenye ramani ya Afrika. Mi naona celebrity community ya Tanzania wangefanya chochote kumuinua kidogo kimaisha kwani ingawa ana mapungufu yake, amejitahidi kutuletea sifa. Tuige mfano wa Zimbabwe:

Munya’s dream comes true
Herald Reporters

ZIMBABWE’S representative in the Big Brother All Stars reality television show, Munyaradzi Chidzonga, is probably the only person in the world who can say coming second beats coming first.
After missing out on the show’s US$200 000 prize, he returned home yesterday to be greeted with the news that a new bank account opened for him had the tidy balance of US$300 000.
On top of that, he fulfilled his childhood dream and met President Mugabe at State House in Harare.
Perhaps for Munya, the cherry on top of it all is that President Mugabe is the one who handed him the bank letter confirming the huge balance.
The money was sourced through a campaign spearheaded by businessman Mr Philip Chiyangwa and the National Indige-nisation and Economic Empowerment Boa-rd chaired by Mr David Chapfika.........

The Herald






'watanzania wenye moyo wamekaa wameamua kuaanda halfa ya kumsaidia ndugu yetu MWISHO MWAMPAMBA amabye baada ya kurudi safari yake ya south amekuta matatizo mengi hayaelezeki humu ni masha tu yamemgeukia kama mtanzania mwenzetu jamani tunaomba ushirikiano wenu kwa kumchangia chochote hata elfu 5 it will make a change in his life...habari mtaisikia hivi punde kwenye magazeti,radio na televisheni...tafadhali watanzania'
Nimeona mtu kaweka hiyo status facebook and I totally agree.kwa kweli watanzania tumchangieni mwisho kwa chochote tulichonacho tuonyeshe umoja, Mwisho ametuwakilisha vizuri sana kama nchi kwenye big brother Africa kwa mara ya pili sasa.
Na kama mlivyoona wenzetu wazimbabwe wamechangishana na wameweza kumpa mshiriki wao Munya dola 300,000 cash sababu wameamini Munya alionewa na kwamba yeye ndio alitakuwa kuwa mshindi.
Watanzania Mwisho anahitaji msaada wetu kwa kweli kapeperusha bendera yetu vyema na alifanikiwa kubaki ndani ya nyumba mpaka siku ya mwisho.
Chochote ulichonacho kitapokelewa hata mliopo nje mnaweza kutuma michango yenu.tumsupport kijana wetu Mwisho…

Stay tuned for more info on how to help Mwisho…

Tunapenda kuiga kweli haya mchangieni wenye nafasi nzuri kifedha mi bado nina majukumu ya kuukwamua ukoo wetu toka kwenye lindi kubwa la umasikini.
 
Back
Top Bottom