nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 820
- 2,896
Muda huu ninaoandika taarifa hii, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Mwita Mwikabe Waitara akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM Tarime, Ndugu Daudi Marwa Ngicho wamewaita viongozi wa kata ambao ni Mwenyekiti, Katibu na Mwenezi na wanafanya kikao kijiji cha Kangariani, ambako ndiko nyumbani kwao na Waitara.
Waiatara amekuwa akikiuka waziwazi makatazo yote yanayofanywa na Chama kwa kusema yeye anajiamini sababu ametumwa na Mh. Rais Magufuli kugombea.
Jambo hili linaondoa USAWA wa ushindani na watia nia wengine ambao wameamua kuheshimu maagizo na taratibu za Chama.
Viongozi walioitwa wanatoka kata zote za Bwiregi na baadhi ya kata walizochagua.
Tunaomba uongozi wa juu ufuatilie mambo anayofanya Waitara Tarime Vijijini, na matukio yote nitayaweka hapa.
Nuni, ilitara kimura.
Venance Omona wa Marwa