mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amesema kuwa hatoweza kurejea Bungeni iwapo Serikali haitachukua hatua za kutatua changamoto za migogoro ya wakulima na wafugaji, miradi ya maji isiyokamilika, na hali ya miundombinu ya barabara jimboni kwake. Hata hivyo, Waitara amesisitiza kuwa bado ana nia ya kurejea Bungeni na hana mpango wa kuachia jimbo lake.