WAATHIRIKA wa mabomu Mbagala Kuu yaliyopelekea kubomoka kwa nyumba zao kutokana na mabomu yaliyosababishwa na kambi ya Jeshi watoa siku tatu kwa serikali la sivyo wataandamana kushinikiza kutimiziwa madai yao.
Waathirika hao wametoa muda huo kwa serikali kwa kuchoshwa na ahadi hewa kutoka serikali inayowafanya waishi maisha ya kutangatanga kama hawakuwa na makazi.
Hatua hiyo ya kuandamana imekuja baada ya serikali kutotoa kauli iliyo thabiti juu ya wahanga hao na kuwapa ahadi hewa ambazo zimewachosha na kuchukua uamuzi huo ili waweze kutimiziwa mahitaji yao.
Akizungumza kwa jazba Makamu Mwenyekiti wa wahanga hao, Bw. Nicklaus Ngaloma amesema kuwa, wanawapa Serikali siku tatu kuanzia jana ili waweze kutimiza ahadi wanazowapa wakazi hao na kama hawatatimiza wataandamana hadi Ikulu kushinikiza kupatiwa fidia za nyumba zao zilizobomoka kufuatia mabomu hayo.
Amesema serikali imekuwa ikitoa ahadi hewa zinazowafanya kucheleweshwa kwa kupewa fidia na kujengewa nyumba hali inayofanya waendelea kuteseka kwenye mahema ambayo wamelundikana zaidi ya familia zaidi ya tano kwenye hema moja.
Amesema serikali inachelewesha mchakato mzima wa kutoa fidia ama kujenga nyumba hizo hali inayowafanya wachoshwe na hali wanayoendelea kuwa nayo sasa.
Hivyo wameamua kufanya hivyo endapo serikali haitaanza mchakato mzima wa nyumba hizo ili warudi katika hali zao za kuishi kama wengine na si kuteseka kulundikana kwenye mahema hayo.
Yaani sisi unavotuaona hatuogopi mabomu endapo watakataza maandamano hayo kama mabomu tulishapigwa nayo sasa ni mabomu gani tutakayoogopa ni lazima tuandamane hayo mabomu ya machozi hayatatutisha walilalama
Wakazi hao wamekuwa wakiishi kwenye mahema hayo ni zaidi ya miezi minne sasa.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2751258&&Cat=1