rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 456
Dk. Slaa awindwa bungeni
Waziri Kombani, Ghasia waongoza mkakati
Mmoja wa viongozi wa kambi ya upinzani aliyezungumza na gazeti hili na kutaka jina lake lihifadhiwe kwa sababu ameteuliwa kuongoza timu ya kuchunguza madai hayo dhidi ya Dk. Slaa, alisema kambi ya upinzani inazo taarifa hizo na inazifanyia kazi kwa siri, kwa sababu baadhi ya wabunge wa kambi hiyo wamenunuliwa ili kumuangamiza.
Bila shaka na Hamadi wa CUF ni miongoni mwao walionunuliwa maana swali alilomuuliza waziri mkuu bungeni linaashiria hivyo.
"Mheshimiwa waziri mkuu, naomba kuuliza. Katika kutekeleza sera ya utawala bora, je ni halali kwa mmiliki wa chombo cha habari kutumia chombo chake kwa ajili ya kuwashutumu watu wengine, aliuliza Rashidi na kutaka kujua msimamo wa serikali (Source= Mwananchi).
Mi naona CUF wamenunuliwa akiwemo Lipumba mwenyewe. Mtakumbuka Lipumba alikuwa pia anaunga mkono ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans. Mpo hapo wana JF? Hii vita dhidi ya ufisadi ndugu zangu kwa kibinadamu ni ngumu mno lakini hakuna kisichowezekana kwa MUNGU. MUNGU ameshaona mateso yetu na hakika sasa yuko kazini kuwasambaratisha hawa wanaosababisha wananchi wateseke huku wao wakilundika mipesa kwenye akaunti zao zikiwa hazina hata kazi ya kufanya huku wenzao wakiamka hawajui hata kama watapata mlo siku hiyo.