Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
anko obama anaita hii ni 'distraction from real issues'. mnataka tuanze kujadili waandishi wameandikaje! the real issues ambazo zinatuathiri watz ni mafisadi, na wametajwa na mengi. mambo ya waandishi wa habari na uandishi mbaya sio issue.
Where are leaders like Edward Sokoine during times like this? I guess they are there kama wakina Dr. Slaa but we need a man like that who is within the government. Which leader within the government is going to stand up & say enough is enough. Nadhani neno "uzalendo" halipo kwenye vocabulary zetu tena.
Sasa kwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshatoa msimamo rasmi wa serikali na kusema kuwa Mengi ana haki ya kikatiba ya kujieleza, huyu Sofia Simba ana uchaguzi wa kufanya moja kati ya mawili haya.
1.Kukubali kwamba alikosea, kumuomba radhi Mengi, na kuchukua msimamo rasmi wa serikali yake.
2.Kukataa msimamo wa serikali yake uliotolewa na PM na kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri ili kuendana na misingi ya "collective responsibility"
Zaidi ya hapo atakuwa anathibitisha kwamba serikali ya Tanzania haina muelekeo na kila kiongozi anajisemea anachojua yeye mwenyewe bila kufuata miongozo ya serikali.
Wewe NIbo wacha ufezuli ,hivi unamjua Lipumba au unamsikia tu,eti wapo kwenye upinzani kwa kulisha familia zao,Lipumbwa analipwa dola ndugu kama huelewi kutokana na ile elimu aliyonayo ambayo inasemekana ni watu wachache sana hapa duniani wenye kuweza kufikia na kuwa na kipaji alicho nacho ,huu unaosema wewe si dharau bali ni uchafu ,Mengi nini Mengi nani Mengi anaishi kwa kuuza na yeye kujigamba na vyombo vyake vya redio shauri lake akiwasikiliza watu kama Nibo basi ajue hawamtakii mema ,hao wahindi haohao watamliza tu.
hizo dola analipwa na nani wewe, eti elimu aliyokuwa nayo ni ya watu wachache kwa nini alichokifanya, rekodi yake ni hipi kuna ma prof kibao duniani na rekodi zao zipo, lipumba amna mtu yeyote anayejua rekodi yake zaaidi ya porojo ni "mmoja ya watu wachache"Wewe NIbo wacha ufezuli ,hivi unamjua Lipumba au unamsikia tu,eti wapo kwenye upinzani kwa kulisha familia zao,Lipumbwa analipwa dola ndugu kama huelewi kutokana na ile elimu aliyonayo ambayo inasemekana ni watu wachache sana hapa duniani wenye kuweza kufikia na kuwa na kipaji alicho nacho ,huu unaosema wewe si dharau bali ni uchafu
.
MENGI NI WARREN BUFFET WA TZMengi nini Mengi nani Mengi anaishi kwa kuuza magazeti na kudanganya umma ,leo amepata ulua na kufadhiliwa na hao hao mafisadi wenzake ,leo amekuwa mtu kwa WaTz sababu anawakoromea wenzake kwa kutumia vyombo vya redio.
Leo JK, ktk hotuba yake ya Mei Mosi kwa wafanyakazi wa Tanzania kupitia kwa Dr Shein ametamka kuwa vita dhidi ya ufisadi ni lazima iendeshwe ki-maadili, bila kupakana matope.
Swali: Hivi wale waliofanya ufisadi ktk EPA, Radar, Deep Green walifanya hivyo kupitia maadili yepi? Walikuwa na nia njema kwa Watz? Huyu jamaa vipi?
Lakini nilifurahishwa na hotuba ya TUCTA, ambayo bila kigugumizi, iliwaponda wote wale wanaowatetea mafisadi kwa njia moja au nyingine, kwani wao ndiyo wanawafanya wafanyakazi wa nchi hii kuwa na kipato duni. Hongera TUCTA!!!!!
Sokoine was not a leader, he was an overrated tyrant, a populist apparatchik.
He would not survive in today's competitive free market accountable arena.
Nimekuwa nikifuatilia habari mbali mbali toka Mengi atoe tamko la "mafisadi papa". Nilicho gundua ni kwamba tokea atoe tamko hilo watu na hata makundi mbali mbali kila leo yanaitisha mikutano na vyombo vya habari. Wengi wao huongea pumba tupu na kuonekana ni kutaka tu umaarufu.
EVERYBODY IS SEEKING THEIR 15 MINUTES OF FAME!!!!!!
jE WOTE HAO WANA NIA NJEMA AU KITU CHA MAANA CHA KUSEMA? AU NI KUTAKA TU KUONEKANA NA KUSIKIKA?
Maana sawa ni vyema tamko la Mengi lime hamasisha watu kuongea iwe wana kubaliana na Mengi au la. Lakini. unakuta kuna watu wana jitokeza wanaongelea yale yale yaliyosha semwa na wengine au wana jitokeza na kuongea pumba tupu.
nimeona thread kuhusu wazee wa Yanga kumtetea Manji. Sawa kila mtu ana haki na mawazo yake lakini je ilikua na ulazima wao kutoka kwenye vyombo vya habari na kuongea?
Mara una sikia vikundi mbali mbali vya CCM. Leo sijui umoja wa vijana wa wapi kesho sijui kiongozi wa kundi gani. Jamani kuna ulazima wote mtokee muongee? Si muunde kauli moja kama chama badala ya kila mmoja kuji tokeza?
Katika hali yote hii nimeona kuna kupendelea kwenye tamko la watu wengi. Kuna BIAS kubwa sana. Leo wazee wa Yanga wanao fadhiliwa na Manji watokee kumtetea Mengi tena kwa kujiamini ina maanisha nini? Au kufanyika survey na kituo kinacho milikiwa na IPP na kuonyesha kwenye tv yao watu wote wakimsupport Mengi. Yote haya yana changia kupungu a kwa credibility.
NI WAKATI MUAFAKA WA KUSIKIA WATU AMBAO HAWA TETEI MASILIHI YAO WALA UPANDE WOWOTE ULE. MAANA WENGI TUNAO WASIKIA NI WATU WANAO JULIKANA MOJA KWA MOJA KUWA WATA TETEA UPANDE FULANI.
Jamani waTAnzania tuache kutafuta umaarufu wa kipuuzi. Tuache ushabiki tu. Haswa hawa wanaoji tokeza kwenye vyombo vya habari ongeeni kwa kutumia akili maana ukishaenda wazi kwenye umma unaweza kunakiriwa na unacho ongea wewe kika tumika dhidi yako baadae.
TUACHE UPAMBE NA KUJI PENDEKEZA. KAMA UTATETEA UPANDE MMOJA AU KUPONDA UPANDE MWINGINE FANYA HIVYO KWA KUTUMIA FACTS. KAMA UNA TOA PERSONAL OPINION BASI ISIWE YA KUPENDELEA(BIAS) AU ANGALAU IWE NA MISINGI
Tatizo ni kwamba kwenye matatizo kama haya ya kinchi kuna makundi mawili:
1.Wenye nia ya kweli na nchi(wachache sana)
2.Wanao tetea maslahi yao kwa kujidai wana tetea maslahi ya nchi(wengi sana)
Haya maoni yangu tu wana JF sijui nyie maoni yenu nini.
Are you DOING THE SAME????? By the way Kila mtu ana haki ya KUONGEA hata huyo Mengi alichokiongea au wahindi aliowataja hakuna jipya.
Ningefurahi kuonga upepo wa mafisadi unageuka tuwaongelee na nyie wafanya kazi MNAOTUSALITI kwani nyie ndio mnashiriki moja kwa moja kusogeza hayo mafile ya UFISADI. SHAME ON YOU NA mEI MOSI YENU.
Zak Malang said:Leo JK, ktk hotuba yake ya Mei Mosi kwa wafanyakazi wa Tanzania kupitia kwa Dr Shein ametamka kuwa vita dhidi ya ufisadi ni lazima iendeshwe ki-maadili, bila kupakana matope.
Swali: Hivi wale waliofanya ufisadi ktk EPA, Radar, Deep Green walifanya hivyo kupitia maadili yepi? Walikuwa na nia njema kwa Watz? Huyu jamaa vipi?
Lakini nilifurahishwa na hotuba ya TUCTA, ambayo bila kigugumizi, iliwaponda wote wale wanaowatetea mafisadi kwa njia moja au nyingine, kwani wao ndiyo wanawafanya wafanyakazi wa nchi hii kuwa na kipato duni. Hongera
Kwa maneno mengine Kikwete anachosema Vita dhidi ya mafisadi lazima iendeshwe KISANII bila kufanya lolote lile dhidi ya mafisadi ili waendelee kupeta. Ni lipi kubwa alilolifanya Kikwete katika vita hii dhidi ya mafisadi zaidi ya USANII!? Mafisadi wanatufisadi Watanzania kwa karibu trillioni moja halafu tusiwapake matope!!!!? Duh! huyu jamaa ni msanii wa kutupa!!!
EPA 133 billioni
Meremeta 155 billioni
Rada 40 billioni
Richmond/Dowand 200 Billioni
Nyumba za serikali 200 billioni
Twin Towers zaidi ya 200 billioni
Mapesa yote haya karibu Shilingi Trillioni 1 yaliyofisadiwa na mafisadi halafu tusiwapake matope!!!!