Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Vyovyote vile, lakini hii haibatilishi kwamba alio wataja ni mafisadi papa na ushahidi upo hata humu JF umeanikwa nje nje. They have to face it regardless of their race, they are thieves! We cant let them kwa kutafuta vijisababu kwamba hoo tunabaguliwa, nooo, kwani wako wahindi wangapi mbona wao hawajatajwa?
 
Wewe NIbo wacha ufezuli ,hivi unamjua Lipumba au unamsikia tu,eti wapo kwenye upinzani kwa kulisha familia zao,Lipumbwa analipwa dola ndugu kama huelewi kutokana na ile elimu aliyonayo ambayo inasemekana ni watu wachache sana hapa duniani wenye kuweza kufikia na kuwa na kipaji alicho nacho ,huu unaosema wewe si dharau bali ni uchafu ,Mengi nini Mengi nani Mengi anaishi kwa kuuza magazeti na kudanganya umma ,leo amepata ulua na kufadhiliwa na hao hao mafisadi wenzake ,leo amekuwa mtu kwa WaTz sababu anawakoromea wenzake kwa kutumia vyombo vya redio.

Mengi na hao wahindi na wengine ambao ameogopa kuwataja wote ni chungu kimoja,Mengi anatumia umasikini wa WaTanzania kuwadhalilisha kwa kuwagaia vijipesa na kutaka kuwatawala akili zao ,Mengi hana lolote zaidi ya kutaka kujionyesha msafi kwa kuwageukia wenziwe ,wote ni nzige ndani ya Tanzania , mengi amezidiwa kete ndio anageuka ili tumuone ni bora na mtetezi lakini ukweli amekoseshwa tonge ndio hasira zake,Mengi kawataja watu watano tena kutoka upande wa wenye asili ya kiasia ,hivi alishindwa nini kuwataja wenye asili ya Congo ,Mengi ametafuta ubaguzi kwa kugawa weusi na weupe .kwa ufupi anawalinda mafisadi weusi na kuwakandamiza weupe ,hili si la kuachiwa hata sekunde moja Mengi ni mbaguzi kwa kitendo hiki anatumia dau la mafisadi kutaka kuwagawa WaTanzania ambao ni watu kutoka mataifa mbalimbali,kama Mengi haelewi Tanganyika ilikuwa ni mbuga tu iliyotawaliwa na wanyama wakali na ukiitafuta historia ya wapi waTanganyika walitokea utafungua akili yako na kuondokana na tabia chafu ya ubaguzi tabia ambayo ilimuondoa Salim Ahmed mtu ambae alishika nyadhifa nyingi tena nyeti katika nchi hii ,ubaguzi ndio uliomhuzunisha na kumfadhaisha na kuwafanya waTz wote kuonekana hatuna maana ,Mengi ni adui wa Taifa hili ambae anataka kutumia rangi kutugawa na kututawala na vipesa vyake vya kuuzia magazeti sie walala hoi kwa nini asiwe kama mwenziwe muuza Icecream ambae ametulia ,Mengi baada ya kukusanya vipesa vya magazeti sasa anataka kufanya jeuri ,amewatenga watu weusi ili awavutie kwake na kuanza kuwanyanyasa na kuwatumia kutokana na umasikini wao,Mengi anataka kutumia vipesa vyake vya kuuza magazeti kuwarubuni wale aliowaacha kuwataja ili waweko upande wake ,kwa ufupi amezidi kuwagawa mafisadi ,yaani amewatenga mafisadi weupe na kuwalinda mafisadi weusi ,mengi mwoga amewataja hawa wahindi mavi kitambaani je angewataja na weusi si angekuwa ameshakamatwa na kuwekwa jela kwa kuvunja sheria ,Mengi amevunja sheria hilo halina mjadala mtajaribu kulikoroga na kulipamba lakini wahindi wameshaliona na wameshapata information za juu kabisa kuwa wakienda mahakamni basi Mengi hatoki ,endeleeni kumpa kichwa Mengi kama hakuuza makaratasi yake yote na fedha yake ikawa fedheha. Jamaa kadai shilingi tu,hivyo weka akili zenu vizuri sio mnamtomeza na yeye kujigamba na vyombo vyake vya redio shauri lake akiwasikiliza watu kama Nibo basi ajue hawamtakii mema ,hao wahindi haohao watamliza tu.

Labda wewe ndiye..
 
WADAU , THIS IS A BURNING ISSSUE.LETS NOT WATER IT DOWN:
-Wajanja wachache wanapo suka mtandao wa kuiba milioni 152 kwa siku kwa miaka miwili-Richmond
Rostam at el

-Wajanja wanaoopoa Bilioni 40 BOT-Kagoda
Rostam at el
-Mjumba ya thamani ya millioni500-800 yanapouzwa kwa Nssf kwa bilion 48
Manji at el

-Radar inapoongezwa bei ili wajanja wakate chao cha juu bil 40
Jeetu
-Ndege ya Rais inaponunuliwa kwa mabilioni harafu hairuki
Jeetu
Sasa mkuu ukikwazwa na hilo utaniita natafuta umaarufu?
Ni heri sasa watu wanapoongea maana wakiamua kutenda kama Anna Kilango alivyosema "patakuwa hapakaliki hapa"
-

Hawa walikuwa wanajulikana kabla hata ya Mengi kuwarusha hewani,
wanaotafuta umaarufu ni wakina Lipumba kwa kupinga ukweli unaojulikana ili mradi aonekane nae amezungumza
 
Hawa walikuwa wanajulikana kabla hata ya Mengi kuwarusha hewani,
wanaotafuta umaarufu ni wakina Lipumba kwa kupinga ukweli unaojulikana ili mradi aonekane nae amezungumza

Kumbe Mengi nae kadandia!

Mangi Mengi hajatulia kabsaaaa, anahitaji kupepewa. Asipoonekana ITV kwa muda hajisikii visuri aisee. Msee misifa achia fijana mbeee.
 
Kweli usilojua ni kama usiku wa giza nene inanikumbusha mwaka fulani watamzamia tuliandamana kupongeza ufaransa kwa kukataa kuwauzia makaburu nyambizi tuliipongeza ufaransa ni kitendo cha kishujaa.lakini ukweli ufaransa ilikuwa inawaadhifu makuburu kwa kuwauzia wamarekani dhahabu.mgogoro huu ulimfanya dr kissinger kutembelea tz, hatimaye afrika ya kusini.sasa vita hivi mengi vs rostam na wengine havina tafauti na hivyo nilivyovieleza.wa tz wepesi kushawisha kwa muhubiri ya askofu yeyote hata kama hajui maandiko matakatifu.matokeo yake tuna dini zaidi ya elfu tatu hapa nchini
 
Mwezi uliopita kuna msamaria mwema alitoa taarifa kwa mamlaka ya chakula na madawa kuhusu uwepo wa dawa feki za malaria.
Mtu huyo alizawadiwa na serikali ikazi burn dawa hizo.

Mbona kwenye hili la Mengi kuna kigugumizi na matokeo yake mawaziri wanawatetea watuhumiwa????

Mzee wa Upako (Mch Lusekelo) jana nae alihoji, " iliyetoa taarifa za DECI alizawadiwa na Deci ikashughulikiwa, iwaje Mengi atoe taarifa halafu ashughulikiwe yeye???
 
Tafadhali Mode futa hii topic haina tija kwa taifa.
 
Wahenga walisema " Amlipaji wa mpiga zumari ndie atakae chagua wimbo..." acheni ITV na Nipashe wa dance ngoma ya boss wao...
 
Hoja ni moJa tu... UFISADI-PAPA!!!.

Hao Vijana wa CCM- Tabora, kusafiri all the way from Tabora hadi Dar kwaajili ya kumtetea fisadi ni jambo la hatari sana....!

Mmepewa nauli na nani? Mmefikia wapi? Mnakula nini hapo Dar?.. Just for that goal? Tabora kuna hospitali ngapi, shule ngapi, na barabara ngapi, mkaacha kuongelea matatizo hayo, mnantetea FISADI PAPA, ANAYEPELEKA HELA ZENU INDIA???

Vijana...!! Are you Vijana... Na sio Wazee!!! Kweli nyie vijana, whom i officially call you VIBARAKA, mnatuachia mzigo mkubwa sana sisi wapenda Utawala Bora!
 
Vyovyote vile, lakini hii haibatilishi kwamba alio wataja ni mafisadi papa na ushahidi upo hata humu JF umeanikwa nje nje. They have to face it regardless of their race, they are thieves! We cant let them kwa kutafuta vijisababu kwamba hoo tunabaguliwa, nooo, kwani wako wahindi wangapi mbona wao hawajatajwa?

Anayeingiza habari za uhindi ndiye anaye water down hii issue na kuwapa msemo. Kulikuwa hamna haja ya kuingiza uhindi, hawa ni mafisadi na waandamwe kama mafisadi, mkiingiza uhindi mnawapa msemo kwamba wanaandamwa kwa sababu wao ni wahindi.
 
Granted, Nipashe si New York Times (ambao nao hukosea pia, lakini husahihisha) lakini hili wamezidisha.

Waliotajwa na Mengi hawakutajwa kwa sababu ya "uTanzania wao wa asili ya Asia" hasha.

Wametajwa kwa sababu ya ufisadi.Kwa hiyo kama wametokea kuwa Watanzania wenye asili ya Asia, hii haimaanishi wamekuwa mafisadi kwa sababu wao ni Watanzania wenye Asili ya Asia, tuna mafisadi wengi Watanzania weusi, na watanzania wenye asili ya Asia wengi ambao si mafisadi.

Kwa hiyo hilo andiko la Nipashe, ambalo linaweza kutafsirika kuwa "Mengi kawatolea uvivu watanzania wenye asili ya Asia" lina mislead kwa kuonyesha tatizo kuwa ni utanzania wenye asili ya Asia, badala ya kusisitiza vita dhidi ya ufisadi.

Mengi naye analeta maswali mengi kwa kutaja Watanzania wenye asili ya Asia tu, ina maana wao tu ndio mafisadi?

Kwahiyo unapendekeza angechomeka mtanzania asiye na asili ya kiasia kwenye top 5 yake kwa lengo la kuepuka maswali mengi tu?

Kama unahisi wapo watanzania wasio na sili ya kiasia ambao walistahili kuwa kwenye top 5 yake, jisikie huru kupendekeza top 5 yako mbadala
 
Last edited:
Nia yetu wote ni kuhakikisha mafisadi wanachukuliwa hatua, lakini walichoandika Nipashe inamaanisha watanzania wote wenye asili ya kiasia ni mafisadi papa kitu ambacho si kweli. Kitu kama hiki kingeandikwa huko kwa Obama unapopasema ingekua bonge la soo. Nipashe wamechemsha.

Mpendwa, hiyo maana sipati picha umeifikiaje. Wengine uelewa wetu mdogo, labda utusaidie kuelewa ni vipi hicho ndio kilichomaanishwa.

Kwa uelewa wangu mdogo, kusema Zitto ni mwizi hakuwezi kamwe kumaanisha wabunge wote ni wezi. (Of coz siamini kwamba Zitto ni mwizi; huo ni mfao tu. Na hata kama ningekuwa naamini hivyo, vile vile hakuwezi kuamaanisha kwamba Zitto ni mwizi; mantiki101).
 
kutoka nipashe nimemalizia sentensi ambayo dikteta alikuwa hataki kumalizia

Pia, hafla hiyo licha ya kumpongeza Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kwa ujasiri wa kutaja Watanzania wenye asili ya kiasia na madhara yao hadharani, wabunge waliwataka mawaziri kufuatilia kero za wananchi badala ya kutumwa na mafisadi kuwasafisha.

hao jamaa ni top five kwa wizi na wote ni wa asia....
ni ukweli wa asia wengi TZ ni mafisadi, kila kitu wao ni short cut tuu
wao ndio kiini cha rushwa africa......

watu msitake kutafuta political correctness mkabadilisha ukweli na ukweli ni indians are thieves and not patriotic
 
Mwezi uliopita kuna msamaria mwema alitoa taarifa kwa mamlaka ya chakula na madawa kuhusu uwepo wa dawa feki za malaria.
Mtu huyo alizawadiwa na serikali ikazi burn dawa hizo.

Mbona kwenye hili la Mengi kuna kigugumizi na matokeo yake mawaziri wanawatetea watuhumiwa????

Mzee wa Upako (Mch Lusekelo) jana nae alihoji, " iliyetoa taarifa za DECI alizawadiwa na Deci ikashughulikiwa, iwaje Mengi atoe taarifa halafu ashughulikiwe yeye???

Mengi hawezi kupewa zawadi kwa vile hana moral authority ya kutaja wafanyabiashara wa kiasia kuwa ni mafisadi papa wakati yeye ni fisadi mzawa aliyejivisha ngozi ya malaika. 'Conflict of interest'.


Na kama ni kupewa zawadi, wangepewa kina Slaa, walitaja mafisadi miaka kadhaa iliyopita. Tena kupitia mkutano wa hadhara sio press conference.
 
Sasa mbona haisemwi nini kimepotoshwa?wengine hatukuona hiyo habari tungependa kujua nini kilionyeshwa ....
 
Wadau hivi huyu Sofia Simba nyuma yake kuna akina nani? Binafsi siamini ni mafisadi pekee wako nyuma yake inaonekana huwa anatumwa specifically kutoa matamko yenye utata ili kutokana na haiba yake ya mtu wa hovyo hovyo basi watu makini wa-assume ni kauli yake tu sio ya serikali. Nakumbuka alivyo-comment baada ya Kitine kuongelea mambo muhimu ya nchi, leo tena anajiunga kuwatetea wafanyabiashara badala ya kuongelea matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi. Kauli zake hizi za ajabu ajabu nafikiri angeongea waziri makini kama Mama Sitta au Shamsa Mwangunga kila mtu angeshtuka, lakini kwa vile kaongea kilaza ndio maana watu wanapuuza! Hivi CV yake ikoje, embu wadau iwekeni hapa tumjadili!

Umenena mdau, sitashangaa kama MC wa chama tawala pamoja na mafisadi wenyewe ndo wamemtuma.
Tukumbuke kuwa RA aliwahi kuwa mweka hazina wa chama tawala, CV ya RA kali sana
 
Kanisa lamtetea Reginald Mengi
Saturday, 02 May 2009 09:38
Na Said Mwishehe
Majira

KIONGOZI wa Kanisa Kipentekoste la Gospal Rivival Centre( GRC) Mchungaji Anton Lusekelo amemtetea Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi kwa kauli yake ya kutaja majina ya watu alidai ni mafisadi papa na kutaka Serikali impe ushirikiano katika mapambano hayo.

Mchungaji amewashangaa watu wanaodai Bw.Mengi anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kubainisha kwamba 'ni bora kujipendekeza kwa Rais kuliko kwa mafisadi papa.'

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, jana Mchungaji Lusekelo alisema, tuhuma alizozitoa Bw. Mengi kwa kutaja majina ya mafisadi papa ni nzito hivyo Serikali haipaswi kupuuza bali kushirikiana naye kuhakikisha watuhumiwa wanachunguzwa na hatimaye kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Alisema haoni sababu baadhi ya watu kuaza kupuuza kauli ya Bw. Mengi kwa sababu ni mtoa taarifa mwema ambaye ameamua kuanika uhalifu hadharani hivyo ni jukumu la Serikali kumlinda mtoa taarifa kwa mujibu wa taratibu za utawala bora .

"Kwa sasa Serikali inachotakiwa kufanya ni kuona jinsi gani inashughulikia majina ya mafisadi papa ambao wametajwa na Bw.Mengi. Naamini Serikali imekuwa mstari wa mbele kushughulikia mafisadi,"alisisitiza Mchungaji Lusekelo.

Alidai anashangazwa kuona wakati Bw.Mengi anatekeleza kazi ya kupambana na mafisadi inayosimamiwa na Serikali, baadhi ya mawaziri akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bi.Sofia Simba na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. George Mkuchika wanamshambulia badala ya kumpongeza.

"Tulitegemea Serikali kuyafanyia kazi maneno ya Mengi dhidi ya mafisadi papa ambao wanaweza kumdhuru wakati wowote baada ya kuanikwa hadharani,"alisema.

Aliongeza kuwa Bw. Mengi alishasema ana vielelezo vyote vya ushahidi wa tuhuma alizotoa dhidi ya watu hao, hivyo ni jukumu la Serikali kuwasiliana naye ili kuchukua hatua zaidi kisheria.

Alitoa mfano kuwa Jeshi la Polisi kwa sasa linahimiza programu ya Polisi Jamii na Bw. Mengi ni miongoni mwa Watanzania walioamua kutumia fursa hiyo kama raia kutaja watu anawatuhumu kwa ufisadi.

Alitoa rai kwa viongozi wa dini, washirikiane na wanasiasa wachache ambao wamejitokeza hadharani kupiga vita ufisadi.

Pia ametoa mwito kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua hatua ya kumfukuza uanachama Bw. Rostam Azizi ambaye ni Mbunge wa Igunga (CCM) ili kulinda heshima ya chama hicho.

Alisema tuhuma zinazomkabili Mbunge huyo ni nzito na zinaligawa Taifa , jamii na Bunge.

Aliongeza ripoti ya REDET ya hivi karibuni inaonesha wananchi bado wanaimani na CCM na vyama vya upinzani havina uwezo wa kushika hatamu, wanachama wanaoandamwa na kashfa mbalimbali kama Bw. Rostam wanaweza kukiathiri chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

"Mwalimu Nyerere aliwafukuza akina Juma Duni , Sharif Hamad, Shabani Mloo na wenzake ili kuimarisha chama. Alitoa mfano Malikia aliyetuhumiwa kwa ukahaba na kuachwa na Mfalme,"alisema Mchungaji Lusekelo kwa lengo la kuitaka CCM kuchukua hatua dhidi ya wanachama wote wanaohusishwa na tuhuma mbalimbali.

Mchungaji huyo alimpongezi Rais Kikwete kwa juhudi zake za kusimama kidete kupinga ufisadi na kuhimiza uwajibikaji.

Aliwapongeza baadhi ya wanasiasa wakiwemo wabunge waliojitokeza na kuamua kupambana na ufisadi.
 
Ni lazima Pinda amtetee Mengi. Atamtetea nani. Hana political weight Tanzania. Ni lazima ajitengenezee mkakati wa kubakia kwenye nafasi hiyo hata baada ya uchaguzi ujao. Mtaona mwaka huu na mwaka ujao kila mwenye uwezo atakayejitokeza atamtetea ili mradi naye atengeneze force kwa maandalizi ya uchaguzi ujao na kurtetea nafasi yake ya uwaziri mkuu. Vinginevyo mtamlaumu akianza tena kulia hadharani.

Sidhani kama kwa kumtetea Mengi ndio anajitengezea mkakati wa kubaki... unless there is something missing!!!

His response was spot-on!!!
 
watu wanaodai Bw.Mengi anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kubainisha kwamba 'ni bora kujipendekeza kwa Rais kuliko kwa mafisadi papa.'

kwa maana hiyo lipumba, sofia s, mkuchika wanajipendekeza kwa ma papa.....
 
Back
Top Bottom