Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Hivi tatizo la mzee Mengi ni nini? Kuwataja akina Rostam, Manji, Jeetu, Subash na Tanil kuwa ni mafisadi wakubwa? Amekosea wapi ktk hili? Namshangaa mwandishi mmoja ambae ni kijana kujiingiza ktk mkumbo huu. Hakuna hoja za kueleweka ulizozitoa ktk makala yako. Nakushauri achana na jambo hili, limekuzidi kimo. Kama bosi wako kakulazimisha kuandika, basi ukatafute hoja za kuandika, kile ulichokisema hakifanani na tunavyokujua. Njaa mbaya sana. Najuuuuuta kuisoma makala yako.
 
Hawa wanaowatetea watuhumiwa wa ufisadi waliotajwa na mzee Mengi wanataka kutuambia kuwa yale aliyoyasema ni uongo? Ni mtanzania gani asiyejua kuwa watu hao wanaiba hela za watanzania? Hivi ni biashara gani wanazifanya hata zikawaingizia hela kiasi hicho? Bahati mbaya, wote hao wana asili inayofanana.
Leo ametokea mtu anatutetea, tunasimama na kumtupia madogo... shame on us! When shall we wake up and stand for our rights?
 
Hivi ktk akili zako timamu unaamini kuwa Mengi ana shida hata akafikia kuiba Benz? Unajua mtu ukiwa muongo kwa nafsi yako, kamwe hutakuwa mkweli kwa mwenzio. Tuwe wakweli kwa nafsi zetu jamani. GT, vipi? Nawe ni miongoni mwao? Siku zenu zinakaribia, ni pale watanzania watakapoamua kuamua.
 
Mengi kusema kweli amekwenda mchomo ,ni kawaida kwa walioshitakiwa hutakiwi tena kuwataja taja ,aidha kama kuwataja wanaweza kuvuka basi mengi atakuwa amepoteza ushaidi au atakuwa amewasaidia kuvuka,inategemea na mawakili na naona serikali imelisitukia hilo ,na ndio pale niliposema hawa mafisadi wanajuana ila wanapokuwa mbele ya macho ya wananchi kila mmoja anamtolea mijicho mwenziwe na kurapu awezavyo isitoshe na kutoa hukumu kabisa ,Mengi ameyafanya hayo ,hivyo ,Wakili anaweza kuwatetea wateja wake kupitia kauli za Mengi si hasha wakashinda kesi na baadae wakamlipa mengi kwa mlango wa nyuma. Tunabaki hapa kucheza pachanga.
 
Mwiba, mzee Mengi hajatoa ushahidi hadharani. Huyo wakili ataanzia wapi? Kama angekuwa ametoa ushahidi, tena hadharani, basi hicho unachowaza kingeleta maana ktk hoja hii, lakini kwa pale alipoishia, bado anabaki ndani ya mstari. Alichokifanya ni kuwaumbua tu.
 
Katika hivi vita vinavyotukabili dhidi ya ufisadi, lazima tuwe tayari kuyapiga vita mafisadi kwa njia zozote zile zilizo ndani ya uwezo wetu. Kama wewe ni mwanasiasa, tumia uwanja wa siasa na hasa mikutano ya hadhara kuwaanika mafisadi kama alivyofanya Dr. Slaa Mwembe Yanga. Kama wewe ni mfanya biashara tumia vyombo vyako vya habari kuwaanika hadharani hawa wahujumu kama alivyofanya Mengi. Kama wewe ni kiongozi wa dini, tumia uwanja wako ndani ya kanisa au msikiti kulaani ufisadi unaoiathiri jamii. Kama wewe ni mwana JF, tumia hii forum kuwakandia wezi bila kuwaonea haya kama tunavyofanya wengi wetu hapa.

Kwa nchi kama Tanzania ambapo uhalifu unaoendeshwa na hawa mapapa unafumbiwa macho na mamlaka husika, ni ruksa kutumia silaha zozote - ziwe za jadi au za kisasa, kuyashambulia hawa manyang'au. Wanaweza wakawa na nguvu kuishinda dola lakini kamwe hawawezi kuwa na nguvu kuwashinda wananchi waliochoka kunyanyaswa. Wanaweza wakawa wameiweka serikali mfukoni, lakini kamwe hawawezi kuziba midomo ya wazalendo watakapoamua kulinda maslahi ya taifa lao. Wanaweza wakakiteka chama tawala kinachounda serikali lakini hawana ubavu wa kupambana na wananchi watakapochoka kuzugwa. Wanaweza kutamba kwa muda lakini lakini tambo zao zitafikia ukingoni siku uvumilivu wa wazalendo utakapofikia kikomo.
Kuna siku mafisadi na vikaragosi vyao
Ndani ya serikali
Ndani ya CCM
Ndani ya bunge
Ndani ya mahakama
Ndani ya vyombo vya dini
Ndani ya vyombo vya habari
Na ndani ya JF
Watapokea adhabu yao wanayostahili
Ya kuchomwa moto kama vibaka.​
 
Kinachonishangaza mimi ni kuona kuwa, waliotuhumiwa kuwa mafisadi ni wafanya biashara, lakini wanaojitokeza kuwatetea ni viongozi waandamizi Serikalini, kwani kuna uhusiano gani kati ya viongozi hao wa Serikali mafisadi? Alichokisema hadharani Mengi ndicho kilichopo ktk vichwa vya watanzania. Kipimo cha haya niyasemayo ni kidogo sana, mchukue Rostam au mwingine yeyote kati wale waliotajwa, mwambie atembee kw miguu mitaa ya Kariakoo kwa muda wa dakika 10, halafu mchukue mzee Mengi, nae afanye hivyo hivyo, matokeo yake kila mmmoja wetu anajua, Mengi atabebwa kwa kushangiliwa na hao mafisadi wataishia mikononi mwa wananchi.
 
Kama ni kweli Sofia Simba na George Mkuchika wametoa kauli hizo kama zilivyoandikwa ktk vyombo vya habari, basi wamejimaliza kisiasa. Wakitaka kujipima kwa kauli hizo, basi wafanye ziara sehemu wanazoishi walalahoi wenzangu, au wakahani msiba ktk maeneo hayo na watu wakawatambua...
 
Na Manyerere kaandika hivi:

Reginald Mengi ni msafi kiasi gani?

Na Manyerere Jackton

NILIANZA kumjua Reginald Mengi, mwanzoni mwa miaka ya 1990. Siku moja, tukiwa nyumbani Msasani, alifika getini. Akazungumza na walinzi. Akaangaza huku na kule kutazama mandhari ya mahali hapo ambako ni nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ili kuona vizuri, alizunguka hadi nyuma ya kibanda cha walinzi. Akarejea mbele ofisini. Akatikisa kichwa. Kwa sauti yake ya upole, akasema, “Baba wa Taifa hawezi kuishi katika mazingira kama haya. Naomba mfikishie ombi langu kwake. Nataka nimjengee fensi. Hii seng’enge haifai.”

Wale maofisa Usalama wa Taifa waliokuwapo, waliheshimu kauli hiyo. Wakati huo Mwalimu alikuwa Butiama. Baada ya siku chache, Mwalimu aliwasili Msasani. Mmoja wa viongozi wa Usalama akabeba msalaba wa kumweleza Mwalimu ofa aliyopewa na Mengi.

Mwalimu akabadilika. Uso ukawa mwekundu. Akatafuna midomo kama ilivyokuwa ada kwake baada ya kuguswa na jambo zito. Mwalimu akahoji, “Mengi nani? Katoa wapi utajiri wa kunijengea fensi? Huyu ni (akatukana). Kama ana hela akawajengee masikini; wapo wengi wanaohitaji msaada. Sitaki kusikia upumbavu wa kunijengea fensi, kwani ameona hii fensi (ya nyaya, tena zilizochakaa) hainitoshi? Mwambieni sitaki kabisa.”

Kweli, Mengi hakuonekana tena kwa Mwalimu, labda wakati wa msiba. Tangu siku hiyo, nikawa nataka kujua sababu za mtu huyu kuchukiwa na Mwalimu. Mwalimu alikuwa “kiona mbali”. Pengine alijua kwamba akiruhusu Mengi amjengee hiyo fensi, baadaye yangekuwa matangazo kuanzia kwenye televisheni, redio hadi magazeti anayoanzisha kama uyoga.

Mwalimu alipofoka kuhusu msaada wa Mengi, alifoka kwa sababu alijua Mengi si msafi kama anavyotaka jamii imtambue. Alijua Mengi jinsi alivyofaidi fedha kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mali ya wananchi, lakini akawa anakwepa kulipa kwa kutumia wanasheria. Hadi leo bado Mengi anakabiliwa na utata mkubwa kuhusu mabilioni aliyokopa yeye au familia yake.

Mwaka 1996 aligombana na viongozi wa Habari Corporation Limited, iliyokuwa ikiongozwa na magwiji wa habari, kina Jenerali Ulimwengu, Johnson Mbwambo, Salva Rweyemamu, Dk. Gideon Shoo na wengine. Chanzo cha ugomvi kilitokana na kuandikwa kwamba anadaiwa mamilioni ya NBC.

Juzi, Mengi ameibuka kwenye vyombo vya habari. Akawa mlalamikaji. Akawa mwendesha mashitaka. Akawa jaji. Akatoa hukumu. Alifanya kile alichofanya kwa kigezo kwamba anapambana na mafisadi. Hivi kina Edward Sokoine, ambao ndiyo wanaoheshimika katika vita hiyo, wangetumia staili hii, nchi ingekuwaje? Mengi ni nani wa kuwahukumu wengine?

Kama ilivyotarajiwa, baada ya kubwabwaja, akawageukia wananchi. Akataka wamuunge mkono. Tena akasema anajua maisha yake yake yako hatarini! Hizi ni propaganda tu. Nani ambaye maisha yake hayako hatarini, hasa wakati huu ambao hata bajaj zinaua?

Akianzisha ugomvi, anataka wananchi wote wamuunge mkono. Wampigie makofi. Akilia, tulie naye. Akicheka, tucheke sote. Mengi anaweza kuanzisha ugomvi kisha akawataka Watanzania wote wamtetee. Akikosa biashara, basi huyo aliyemshinda kwenye biashara hiyo, ni fisadi. Atahamishia ugomvi kwenye televisheni yake.

Amegombana na kila kundi katika jamii. Amegombana kuanzia kwa maaskofu hadi kwenye kundi la Ze Comedy. Fikiria. Kama mtu anaweza kugombana hata na viongozi wa kiroho, huyo lazima atakuwa na matatizo.

Yeyote anayemwangalia vema Mengi kwenye televisheni, atagundua kuwa huyu Mtanzania mwenzetu anaelekea kuchanganyikiwa. Inawezekana kabisa akili ya leo ya Mengi si akili ile aliyokuwa nayo alipoanza harakati za kujikomboa kiuchumi. Amejisahau mno kwa kudhani kwamba wananchi wote ni wajinga.

Mengi wa leo amekuwa wa kukomoa wenzake kwa kivuli cha kupambana na mafisadi. Yeye ana usafi gani? Hivi kweli katika kundi la watoa rushwa, Mengi ataponea tundu gani? Juzi alipotaja hao anaowaita “mapapa wa ufisadi”, aligawa shilingi ngapi kwa kila mwanahabari? Mimi najua alitoa kiasi gani. Aseme usafi wake uko wapi?

Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kujiweka nyuma katika mapambano dhidi ya ufisadi. Mara zote tumekemea na hata kuibua ufisadi katika wizara, idara na kila mahali katika jamii yetu. Ushahidi wa ushindi tulioupata upo.

Lakini vita dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi yetu tumeiendesha kwa misingi ya haki na kwa utu. Wapiganaji wa kweli hawawezi kutumia nafasi ya vyombo vyao vya habari, kuwadhalilisha watu wengine.

Mengi anawatukana wenzake kwa sababu anajua kwamba ana vyombo vya habari vinavyotazamwa, kusikilizwa na kusomwa na wananchi wengi-ndani na nje ya nchi. Anajua masikini hawa wenye rangi nyeupe wataonekana wa ajabu wakianzisha televisheni maalumu ya kumshughulikia Mengi.

Kama tunaweza kulaani matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi na watumishi wa Serikali, kwa nini Mengi asilaaniwe kwa matumizi mabaya ya vyombo vyake vya habari?

Hivi, tajiri Teddy Tunner, ambaye ni mmiliki wa kituo cha televisheni cha CNN, akiamua kufanya kama haya yanayofanywa na Mengi, mambo yatakuwaje? Lakini tofauti na Ulaya na Marekani, hapa Tanzania kuna kina Mengi wanaosimama na kutukana wengine, kisha wakaachwa hivi hivi. Sana sana mtukanaji eti anamweleza anayetukanwa, “ukitaka nenda mahakamani”.

Mengi amefika mahali amejisahau. Ameona anaweza kutumia silaha yoyote kufanikisha malengo yake anayoyajua yeye mwenyewe. Mengi anajua kwamba nchi yetu inafuata misingi ya kisheria. Tuna Mahakama, Bunge na Serikali. Kila chombo kinawajibu wake. Tuna Takukuru na vyombo vingine vingi tu. Kama ushahidi anao, kashindwa nini kuupeleka katika vyombo hivyo? Kama ameupeleka, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, wa kulaumiwa ni mtuhumiwa au anayestahili kuwashitaki? Kwa nini mtuhumiwa atukanwe na kudhalilishwa?

Anajua fika kwamba baadhi ya watu anaowashambulia hadharani wana kesi mahakamani. Anajua kuwa Mahakama inapokuwa kwenye shughuli zake, inapaswa iheshimiwe. Ipewe wigo wa kupitia mashitaka na utetezi ili ifikie hatua ya kutoa hukumu ya haki. Je, katika mazingira ya aina hii, mazingira ya kutukanana, kubezana, kusemana ovyo, mahakama itakuwa na kazi gani?

Kama kweli Mengi alikusudia kuwataja mapapa wa rushwa, basi angewataja hata wale wenye rangi nyeusi! Kama hawa weupe wamechukua fedha, nani kawapa huko BoT. Je, BoT kuna gavana Mhindi au Mzungu? Yeye alipochukua fedha NBC, kulikuwa na mkurugenzi Mhindi au Mzungu? Je, mawaziri wanaoidhinisha, ni wa kutoka nchi gani? Hawa kwa nini asiwaunganishe? Kwa nini achague hawa wenye rangi tofauti tu?

Angewataja na kina Manyerere wenye ngozi nyeusi ili walau watu wajue kwamba anachofanya anakifanya kwa misingi ya haki. Lakini kutamka wazi kwamba hawa “wenye asili ya Kiasia” ndiyo watu hatari, ndiyo wanaoimaliza nchi, ni kutafuta tu kuungwa mkono na jamii ya watu masikini. Kuna Wahindi na wazungu waliofanya mambo mengi mazuri katika nchi hii. Kina Dereck Brycson, Alnoor Kassum, Amir Habib Jamal, Shamim Khan, Joan Wicken na wengine wengi.

Mengi amekuwa makini sana kutafuta “sympathy” kutoka jamii. Mara zote anatafuta mambo ambayo anajua akiyateremsha kwenye jamii, ataungwa mkono. Akishawaandalia chakula walemavu na watu wengine masikini, hazitopita siku nyingi, ataibua “bomu”.

Haya tumeyaona mwaka 1994 aliponunua ugomvi kwa nguvu kutoka kwa Watanzania wenye asili ya Kiasia, hata akafika hatua akadai kwamba kulikuwa na mpango wa kumtoa roho.

Rais wa wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, akapata habari hizo. Mengi akapewa ulinzi wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU). Tena wengine walikuwa wakilinda kwa Mwalimu Nyerere. Wakatolewa ili wamlinde Mengi. Hakuna aliyelalamika maana Katiba ya nchi inazungumzia haki ya kila mwananchi kupewa ulinzi na hifadhi ya maisha yake.

Baadaye ikaja kubainika kuwa ugomvi ule ulitengenezwa na Mengi mwenyewe, akitaka wananchi wamwonee huruma. Hata alipokuwa akiuhadaa umma wa Watanzania kwamba matangazo ya mpira au ngumi yalikuwa yakiletwa moja kwa moja kutoka Ulaya na Marekani, akasema anasakamwa na wabaya wake. Ukweli ulikuwa kwamba badala ya matangazo yale kuwa yanatoka moja kwa moja Ulaya, yalikuwa yanatoka moja kwa moja Mikocheni!

Mengi, kama nilivyosema hapo awali, aligombana na maaskofu na wapinga matumizi ya kondomu. Yeye anajua wazi kwamba makanisa yana miiko. Hayaongozwi na utashi wa wamiliki au wenye hisa kwenye viwanda na biashara za kondomu. Akatetea kondomu hadi akaitwa “nabii wa kondomu”.

Bwana mkubwa huyu huyu aligombana na Wilson Masilingi baada ya kunyimwa umiliki wa hoteli ya Kilimanjaro. Hatuna hakika kama hoteli hiyo angepewa Mengi, ingekuwa na mwonekano mzuri na wa maana kama huu uliowekwa na mwekezaji aliyepewa.

Alishagombana na Shamin Khan, wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Mengi akawa anawanywesha watu maji ya kisima, lakini akitangaza kuwa ni ya chemchem kutoka mlimani. Waligombana wee, hadi Khan akaibuka mshindi. Maneno ya udanganyifu yakafutwa kwenye chupa za maji. Udanganyifu nao ni ufisadi.

Huyu huyu Mengi amegombana na Yusuf Manji. Amemtukana kadri alivyoweza. Akawaingiza hata baadhi ya wanasiasa mamluki ili wamtukane. Hapa naomba wasomaji watambue kuwa simtetei Manji au hao aliowabatiza kuwa ni “mapapa wa ufisadi”. Ninachotetea hapa ni maadili na namna ya kuwasilisha jambo. Kumparamia mtu na kuanza kumtukana kwa sababu tu mmenyang’anyana michezo ya bahati na nasibu na kamari, si jambo la kiungwana.

Wiki kadhaa zilizopita alimvaa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha. Kila aliyefuatilia ugomvi ule kwa makini, alimshangaa Mengi. Mtu mzima kubishana, kutukanana na mtu mwenye hadhi ya “mwanao”, ni aibu.

Kutoka kwa Masha ameingia kwa wahariri kadhaa wa vyombo vya habari. Yeye kila siku anasimama kudai kwamba mafisadi wanaanzisha magazeti kumshambulia. Lakini anapuuza upande wake. Yeye kila anapokabiliana na mtu au kikundi cha watu, si ajabu tukaona gazeti maalumu kwa ajili ya kukabiliana na mtu au kundi alilokorofishana nalo.

Ni wapi ambako yeye anapata fedha safi za kuanzisha magazeti ambako wengine hawawezi kuzipata? Kuna vijana wamejiunga. Wameanzisha magazeti kwa nia njema, lakini ameingilia kati na kusema wamefadhiliwa na mafisadi.

Makala hii itazua mjadala. Nitafurahi sana mjadala huu ukiendelea. Mengi ameshapeleka uwongo hadi Ikulu akiwasingizia waandishi wa habari kwamba wameunda umoja kumchafua Rais Kikwete. Sina hakika, lakini inawezekana ndiyo mbinu yake ya kujipendekeza ili awe karibu na Rais Kikwete. Anajua hakumuunga mkono Kikwete wakati wa mchakato, sasa kufukia hayo, anafanya kila awezalo ili awe karibu naye. Lakini wenye akili wanajua hakuna kiongozi makini anaweza kufunga pingu za urafiki na Mengi. Hana uadilifu huo.

Ataibuka na kusema nimetumwa na mafisadi. Atasema nimelipwa ili nimwandike. Bora aseme uwongo huo, lakini nimeshindwa kuvumilia usanii huu anaoufanya sasa. Tumefanya kazi Habari Corporation kwa miaka mingi kabla ya kampuni hii kupata wamiliki wengine. Leo hatuwezi kukosa amani kwa sababu Mengi anatusema kwamba tumeajiriwa na mafisadi. Yeye ameuza kampuni ngapi? Siwezi kuendelea kukaa kimya na kumpa heshima haramu.

Mengi hana usafi huu ambao anataka watu waamini kuwa anao. Hana. Anapoamua kuwatukana wengine, lazima ajiridhishe kwanza kwamba yeye ni msafi. Hata Biblia inasema usikazane kukinyooshea kidole kibanzi kilicho kwenye jicho la mwenzio wakati lako lina boriti!

Lakini hatari kubwa ni hii ya kuanza kuhubiri maneno yanayoweza kuibua chuki kubwa miongoni mwa wananchi. Hakika, kwa maneno ya kusema Wahindi ndiyo waporaji wakuu wa uchumi wa nchi hii, anataka kuwaeleza wananchi kwamba sasa waanze kuwachukia. Kwa nini udhaifu wa Waafrika kuongoza nchi na kumiliki uchumi wanasukumiwa Wahindi na Wazungu? Tangu Uhuru mwaka 1961, tumekuwa na rais yeyote Mhindi au Mzungu? Udhaifu ni wetu wenyewe.

Kwa maneno yake, sijui itakuwaje Watanzania wenye asili ya Kiasia wakiharibikiwa gari Manzese au Mwanjelwa. Je, hawatashambuliwa? Je, wakishambuliwa, kitu gani kitazima mwendelezo huo? Mengi anaipeleka wapi Tanzania? Yeye amezeeka. Amekula chumvi ya kutosha. Awaache vijana wadogo nao wawe wazee kama yeye.

Mengi ni mtuhumiwa wa ufisadi kama watuhumiwa wengine. Bahati yake ni kwamba hakuchota fedha za EPA. Tofauti na hapo, ni fisadi tu hata kama si wa fedha, basi wa tabia.

Wakati sasa dunia ikiwa kwenye mtikisiko wa uchumi, Mengi yeye yuko kwenye mtikisiko wa akili. Amekosa busara! Angekuwa na busara, vita dhidi ya mafisadi angeishiriki kiungwana kama wanavyofanya wenzake.

Kama nilivyosema, huu ndiyo mwanzo wa mjadala. Kama yeye amekuwa mbele kuwasema wenzake, naye avumilie kusemwa. Kama kutukana watu wengine ni ushujaa, ipo siku naye atakutana na vichaa watakaomtukana.

Kuendelea kumnyamazia Mengi ni kuitoa rehani amani ya nchi yetu. Kumwogopa hakuwezi kusaidia kumrejesha kwenye mstari. Leo anatangaza hatari kama hii kupitia vyombo vyake vya habari, kesho kitu gani kitamzuia iwapo ataamua kutumia vyombo hivyo hivyo kutaka rais ang’olewe? Huyu ni hatari kama zilivyo hatari nyingine zinazoikabili nchi yetu. Wazanaki wanasema, “nyambisabisa obhurweri, ekiriro kirambura”. Tafsiri nitaitoa toleo lijalo.

manyerere@hotmail.com

0713 335469

Katika hili mimi naungana na mtoa hoja kuwa ukimchunguza kuku hautakula nyama yake, ni kweli kila mtu anayo mapungufu ya aina fulani.hatuwezi kusema mengi ni msafi tutakuwa tunajidanganya.Lakini pamoja na kutokuwa msafi anapozungumzia swala ambalo viongozi wetu waliopewa dhamana ya kulikemea wanaliogopa yeye akajitoa mhanga hatuna budi kumshukuru,Mbona wahusika wakuu wamekaa kimya? nikosa kuwadharau watanzania kwa vigezo vya kuwafikiria kuwa hawajui mambo. Hawa watu tunaodhania hawajui wanajua mambo mengine hata Rais wanchi hayajui.kwa hiyo Manyerere mchango wako ni mzuri utufanye tupanue ulingo wa kufikiri na zaidi tusimame na watu wanaotetea masilahi ya wananchi. kuwa na vyombo vya habari si issue hata rostam anavyo tena anaweza kuwa anavitumia kwa siri jambo ambalo ni unafiki atoke wazi ajitete kukaa kimya kunaashilia mambo, Tusingefurahia viongozi wetu ambao tunawalipa kwa pesa zetu ndo wawe mstari wa mbele kushambulia wananchi kwani wao pia hawawezi kuacha serikali ichukue mkondo?Nazidi kusema siwezi kushangaa kwa sofia kuchemsha anapomsema Mengi kwa wale msiomjua fyatilieni mtamjua ni mama wa jinsi gani?.Mengine hatuyasemi hapa jamvini kwani ni mambo ya mtu binafsi,kama ambavyo Mengi si msafi ndo Sofia asivyo msafi pia pamoja na wengine wengi.
 
Naye Lipumba wa CUF kaingilia sakata hili -- na kama ilivyokuwa kwa mitambo ya Dowans -- amejikita upande wa mafisadi. Katika sakata la Dowans alijikuta alikamata pabaya kwani Hatimaye serikali imekacha kununua Dowans.

Huyu kiongozi wa CUf nilikuwa namheshimu sana lakini naona tayari ameharibiwa na RA kupitia kwa Jussa ambaye ni swahiba wa RA. Inasikitisha kuona Profesa hataki kukubali kwamba chama chake - CUF - kilitoka kapa huku bara (hata kiti kimoja cha ubunge hakikupata -- wala kiti cha udiwani ktk mkoa wa Dar) kutokana na mapesa waliyotumia CCM kutoka ufisadi wa EPA, radar, NSSF, ndege ya urais etc.
 
Hii ni kwa Pundamilia,

Wizi ni kosa la jinai (criminal). Mwenye uwezo wa kumfikisha mwizi mahakamani na kumsomea mashtaka ni Jamhuri. Raia ukishuhudia wizi, kama anaibiwa mwenzako, au jamii au mwenyewe, huna uwezo wa kwenda kumshitaki mwizi mahakamani.

Kazi yako ni kutoa ushirikiano kwa Jamhuri (kupitia jeshi la polisi), kwa kuiambia au kutoa taarifa na kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamni utakapoitwa kama shahidi.

Mengi ameiambia serikali, si kwa kwenda polisi. Kwa kuwa ananguvu ya vyombo vya habari ametumia nguvu hiyo kuiarifu Jamhuri kuwa kuna mwizi ameonekana ameiba na ushahidi anao.

Sasa sioni tatizo hapo ndugu pundamilia. Kuiambia polisi au kuiambia jamhuri mpaka uende mwenyewe kituo cha polisi na makaratasi? Hivi mtu huwezi kupiga simu polisi ukasema Mimi fulani niko mahali fulani nashuhudia au nimeshuhudia tukio la wizi??

Sijaona kosa la raia kusema kuwa mali ya umma imefujwa na yeye anao ushahidi!! Vyombo husika vichukue hatua na baada ya kufanya uchunguzi vije mbele na viseme ushahidi hautoshi kuwafikisha mahakamani. Halafu walituhumiwa ni juu yao kufungua kesi ya madai.

Pundamilia unaposema Mengi ilitakiwa afuate taratibu; naomba uwe wazi ni taratibu zipi hizo?

Kipima pembe je Fisi akiwa hakimu mbuzi ana sheria?
 
Naye Lipumba wa CUF kaingilia sakata hili -- na kama ilivyokuwa kwa mitambo ya Dowans -- amejikita upande wa mafisadi. Katika sakata la Dowans alijikuta alikamata pabaya kwani Hatimaye serikali imekacha kununua Dowans.

Huyu kiongozi wa CUf nilikuwa namheshimu sana lakini naona tayari ameharibiwa na RA kupitia kwa Jussa ambaye ni swahiba wa RA. Inasikitisha kuona Profesa hataki kukubali kwamba chama chake - CUF - kilitoka kapa huku bara (hata kiti kimoja cha ubunge hakikupata -- wala kiti cha udiwani ktk mkoa wa Dar) kutokana na mapesa waliyotumia CCM kutoka ufisadi wa EPA, radar, NSSF, ndege ya urais etc.



Lipumba si mzee wa kuganga njaa!! Hana issue siku hizi.
 
NILIKUWA DODOMA WAKATI WA UCHAGUZI WA UWT NA SOPHIA SIMBA ALIKUWA AKIGAWA KATI YA Sh 150,000 na 200,000 KWA WAJUMBE, JE, HUYO ANAWEZA KUPIGA VITA RUSHWAA? UNADHANI ATAWATENGA WALIOMPA FEDHA ZA KUGAWA?

Sofia aliwagawia akina mama wenzie kiasi cha fedha kadha je inapokuwa wakati wa kuhonga akina baba nadhani huwapa mamilioni.....!!!!, lakini mnamjua Sofia tangu alipoanza kusoma cheti cha sheria hata kwenda mlimani kuchuakua sheria. Watanzania tunajua mengi lakini itafika wakati babu atataka kusema.
 
Najaribu kujiuliza, hivi ile fensi aliyotaka kujenga Mengi kwa marehemu baba wa Taifa bado ipo vile vile au imejengwa? Vile vibanda vya askari pale mlangoni vimekarabatiwa au bado vimebaki vile vile? Hivi suala la kukopa Bank ambalo ni mkataba kati ya Bank na mkopaji ni kosa la jinai? Hapa ndipo ninapokuwa na mashaka na Bwn. Manyerere. Kama sikosei, Fensi imejengwa na vibanda vimefanyiwa ukarabati. Nadhani Mengi alitaka kupaboresha nyumbani kwa baba wa Taifa. Hebu tutafute ufisadi wa mzee huyu Mengi, suala la kukopa Bank ni la kimkataba, kama Bank hawaridhiki na mteja wao, wana haki ya kuchukua hatua za kisheria. Hivi Manyerere hajawahi kusikia habari za EPA, RICHMOND, RADAR, BoT, TICS, DOWANS na kadharika? Hivi ni kipi kati hivi viaua uchumi wa nchi? Bank kukopwa na Mengi au kashfa za EPA, RICHMOND, RADAR, BoT, TICS, DOWANS? Je, ni wapi alijaribu kuwafahamisha watanzania madhara yake?
 
Kahinda, kama kungefanyika uchunguzi kt uchaguzi ule wa UWT, basi watu wengi sana wangeumbuka. Sitaki kusema mengi mengi, lakini kwa kifupi, Sofia na baadhi ya viongozi waandamizi ktk Serikali hii wamemtia aibu kubwa sana JK na chama chake. Tumshukuru Mungu kwa ushujaa, ukomavu wa kisiasa, upendo kwa nchi yake na uvumilivu wa hali juu aliouonesha mgombea aliyeporwa kura zake na kumpa ushindi wa matata saana Bi. Sofia. Kama angethubutu kusema kuwa hakubali matokeo yale, basi Dodoma na ndani ya chama pasingetosha.
 
Katika hili mimi naungana na mtoa hoja kuwa ukimchunguza kuku hautakula nyama yake, ni kweli kila mtu anayo mapungufu ya aina fulani.hatuwezi kusema mengi ni msafi tutakuwa tunajidanganya.Lakini pamoja na kutokuwa msafi anapozungumzia swala ambalo viongozi wetu waliopewa dhamana ya kulikemea wanaliogopa yeye akajitoa mhanga hatuna budi kumshukuru,Mbona wahusika wakuu wamekaa kimya? nikosa kuwadharau watanzania kwa vigezo vya kuwafikiria kuwa hawajui mambo. Hawa watu tunaodhania hawajui wanajua mambo mengine hata Rais wanchi hayajui.kwa hiyo Manyerere mchango wako ni mzuri utufanye tupanue ulingo wa kufikiri na zaidi tusimame na watu wanaotetea masilahi ya wananchi. kuwa na vyombo vya habari si issue hata rostam anavyo tena anaweza kuwa anavitumia kwa siri jambo ambalo ni unafiki atoke wazi ajitete kukaa kimya kunaashilia mambo, Tusingefurahia viongozi wetu ambao tunawalipa kwa pesa zetu ndo wawe mstari wa mbele kushambulia wananchi kwani wao pia hawawezi kuacha serikali ichukue mkondo?Nazidi kusema siwezi kushangaa kwa sofia kuchemsha anapomsema Mengi kwa wale msiomjua fyatilieni mtamjua ni mama wa jinsi gani?.Mengine hatuyasemi hapa jamvini kwani ni mambo ya mtu binafsi,kama ambavyo Mengi si msafi ndo Sofia asivyo msafi pia pamoja na wengine wengi.
Hata kama Mengi angekuwa ni ufisadi wa aina yake kama huyu Manyerere anavyodai bado TWO WRONGS DOES NOT MAKE A RIGHT. Twambie Bw Manyerere na wenzake wote wanaojaribu kufunika hao waliotajwa na Mengi na kuwa spokesperson wao je NI KWELI WATU HAWA NI MAFISADI PAPA AU NI WATU SAFI? Mbona issue yenyewe inayozungumzwa ni mafisadi wanaotafuna nchi yetu. Je watu hawa waliotajwa ni safiii? Kama Mengi naye ni fisadi basi wanaomjua wamtaje, na sio kutueleza kuwa alikopa fedha NBC akashindwa kulipa akaweka mawakili ili wamtetea asichukuliwe hatua. Sasa huo ni ufisadi? Hayo ni yale yaliyotajwa kuwa ni ufisadi wa Mbowe kukopa na kutolipa kwa wakati kisha kuweka mawakili. Labda watwambie huo ni uzembe wa kibiashara au ni mipango mibaya au hawakuwa makini walipobuni miradi yao lakini huwezi kutwambia huo ni ufisadi. Je ROSTAM na hao wenzake NI SAFI? Nakumbuka story moja nyani walipomlalamika binadamu kuwa anawaonea kwa kuwakamata kwa mitego na kuwapiga na kuwaua. Jibu la mwanadamu lilikuwa rahisi sina ugomvi na nyani ila napambana na wezi wa mahindi yangu. Bahati mbaya kila ninapoweka mtego wa kunasa wezi wa mahindi yangu nakuta walionaswa ni nyani. Sasa hata kama si wabaguzi ila kama kila mara issue za ufisadi papa zikitokea tunakuta ni kina Patel sasa tusemeje. Hawa wanacorrupt system nzima. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Ahsanteni ndugu wana JF
 
Hata kama Mengi angekuwa ni ufisadi wa aina yake kama huyu Manyerere anavyodai bado TWO WRONGS DOES NOT MAKE A RIGHT. Twambie Bw Manyerere na wenzake wote wanaojaribu kufunika hao waliotajwa na Mengi na kuwa spokesperson wao je NI KWELI WATU HAWA NI MAFISADI PAPA AU NI WATU SAFI? Mbona issue yenyewe inayozungumzwa ni mafisadi wanaotafuna nchi yetu. Je watu hawa waliotajwa ni safiii? Kama Mengi naye ni fisadi basi wanaomjua wamtaje, na sio kutueleza kuwa alikopa fedha NBC akashindwa kulipa akaweka mawakili ili wamtetea asichukuliwe hatua. Sasa huo ni ufisadi? Hayo ni yale yaliyotajwa kuwa ni ufisadi wa Mbowe kukopa na kutolipa kwa wakati kisha kuweka mawakili. Labda watwambie huo ni uzembe wa kibiashara au ni mipango mibaya au hawakuwa makini walipobuni miradi yao lakini huwezi kutwambia huo ni ufisadi. Je ROSTAM na hao wenzake NI SAFI? Nakumbuka story moja nyani walipomlalamika binadamu kuwa anawaonea kwa kuwakamata kwa mitego na kuwapiga na kuwaua. Jibu la mwanadamu lilikuwa rahisi sina ugomvi na nyani ila napambana na wezi wa mahindi yangu. Bahati mbaya kila ninapoweka mtego wa kunasa wezi wa mahindi yangu nakuta walionaswa ni nyani. Sasa hata kama si wabaguzi ila kama kila mara issue za ufisadi papa zikitokea tunakuta ni kina Patel sasa tusemeje. Hawa wanacorrupt system nzima. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Ahsanteni ndugu wana JF
 
1.
Kweli, Mengi hakuonekana tena kwa Mwalimu, labda wakati wa msiba. Tangu siku hiyo, nikawa nataka kujua sababu za mtu huyu kuchukiwa na Mwalimu.


- Hii habari sio ya kweli,nimeshuhudia Mwalimu akisafiri na Mengi katika ndege yake ya serikali mara chungunzima, na besides wakati huo Mengi bado alikuwa ni Mwenyekiti wa lile shirika la Accounts la taifa alikuwa na access na Mwalimu, all the times. Mara kwa mara Mengi alikua na tabia ya kuomba ride kwenye ile ndege ya Mwalimu, hakuna hata siku moja Mwalimu, alimfukuza ndani ya ile ndege, infact alikuwa akimuona tu anamuita hata kama yuko nyuma aje karibu na ataongea naye mpaka mwisho wa safari, kwa hiyo hili la fensi sio kweli kwa sababu kisheria linaangukia kwenye bajeti ya Ikulu, ambayo Mwalimu hakuwa na say nalo na kama kweli fensi ilikuwa imechoka ni uamuzi wa usalama wa taifa kuitengeneza sio Mengi.

- Ni kichekesho kikubwa sana kwamba Mengi, anaweza kuingilia kazi ya usalama wa taifa kwa kuwakumbusha kwamba fensi ya Mwalimu haifai na hata bosi wa usalama kwenda kwa Mwalimu na kumfikishia ujumbe wa Mengi, that is hillarious! Enzi hizi aliyekua anaongoza usalama wa rais alikua Mwangota, hivi huyu mwandishi anamfahamu au alishawahi kumsikia? Maana huyu alikuwa na tabia ya kuwalamba vibao viongozi magoi goi, sasa kama kuna usalama wa kumfikishia ujumbe wa Mengi Mwalimu then, basi alikuwa ni huyu Mnyaki, kwanza angeanza kumla vibao Mengi mwenyewe, kwa kumuingilia kazi yake, hai-make make a sense at all!



2.
Mwalimu alikuwa “kiona mbali”. Pengine alijua kwamba akiruhusu Mengi amjengee hiyo fensi, baadaye yangekuwa matangazo kuanzia kwenye televisheni, redio hadi magazeti anayoanzisha kama uyoga.


- Mwalimu alikuwa kiona mbali sana ndio maana aliona mbali sana kwa kutupatia Mr. Clean bin Kiwira, what a kiona mbali!

3.
Mwalimu alipofoka kuhusu msaada wa Mengi, alifoka kwa sababu alijua Mengi si msafi kama anavyotaka jamii imtambue. Alijua Mengi jinsi alivyofaidi fedha kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mali ya wananchi, lakini akawa anakwepa kulipa kwa kutumia wanasheria. Hadi leo bado Mengi anakabiliwa na utata mkubwa kuhusu mabilioni aliyokopa yeye au familia yake.

- Another joke, hivi Mengi alichukua hela NBC au alikopa kama wananchi wengine wanavyoruhusiwa kukopa na kurudisha? Yes it is a fact kwamba Mengi alikopa hela toka bank na kuzifanyia biashara, huku akitoa ajira kwa wananchi ambao hata serikali ya Mwalimu ilikuwa imeshindwa kuwapa ajira, is that a crime?

- Kukwepa kulipa inakubaliwa kwa sababu za kisheria, sio blah! blah! hivi huyu muandishi hajasikia kuwa benki za US zimeshindwa kulipa madeni na zimelipiwa na serikali, sasa hapa cha ajabu ni kipi? Kama biashara haizalishi mkopaji ana haki kisheria kuifahamisha benki aliyokopa kwamba wampe break mpaka atakapokaa sawa, mbona Donald Trump anafanyiwa kila wakati, I mean kama ni kumchafua Mengi basi watafute angalau convincing facts, badala ya hizi pwagu na pwaguzi ambazo sio siri ni pathetic!

FMES
 
Can I make up a story about Nyerere na maoni yake juu ya Rostam? where by I'm the only witness!?
 
Back
Top Bottom