Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Na huyo mkuchika anayesema kuwa kapata malalamiko mengi toka kwa watu kuhusu tuhuma alizotoa mengi, mbona hashughulikii malalamiko ya upande wa pili ya wale wanaomuunga mkono mengi?Hebu huyu mkuchika asituchanganye.Akitaka kutenda haki apime malalamiko against Mengi na yale yanayom sapoti Mengi then upande utakaolala ndo utakuwa una haki.Sofia yeye kama mwanamke anatafuta support kwa kuwa walotajwa ndo wako nyuma yake kimaisha(ndo wanaompa ulaji) hana jipya
 
Katika hili mimi naungana na mtoa hoja kuwa ukimchunguza kuku hautakula nyama yake, ni kweli kila mtu anayo mapungufu ya aina fulani.hatuwezi kusema mengi ni msafi tutakuwa tunajidanganya.Lakini pamoja na kutokuwa msafi anapozungumzia swala ambalo viongozi wetu waliopewa dhamana ya kulikemea wanaliogopa yeye akajitoa mhanga hatuna budi kumshukuru,Mbona wahusika wakuu wamekaa kimya? nikosa kuwadharau watanzania kwa vigezo vya kuwafikiria kuwa hawajui mambo. Hawa watu tunaodhania hawajui wanajua mambo mengine hata Rais wanchi hayajui.kwa hiyo Manyerere mchango wako ni mzuri utufanye tupanue ulingo wa kufikiri na zaidi tusimame na watu wanaotetea masilahi ya wananchi. kuwa na vyombo vya habari si issue hata rostam anavyo tena anaweza kuwa anavitumia kwa siri jambo ambalo ni unafiki atoke wazi ajitete kukaa kimya kunaashilia mambo, Tusingefurahia viongozi wetu ambao tunawalipa kwa pesa zetu ndo wawe mstari wa mbele kushambulia wananchi kwani wao pia hawawezi kuacha serikali ichukue mkondo?Nazidi kusema siwezi kushangaa kwa sofia kuchemsha anapomsema Mengi kwa wale msiomjua fyatilieni mtamjua ni mama wa jinsi gani?.Mengine hatuyasemi hapa jamvini kwani ni mambo ya mtu binafsi,kama ambavyo Mengi si msafi ndo Sofia asivyo msafi pia pamoja na wengine wengi.

Manyerere!

Omba Mungu akusamehe hata kama umeajiriwa na RA pamoja na CCM hapa umepotea! Hoja ya msingi ni kutaja mafisadi na ni kuitikia mwito japo mbovu wa JMK na Pinda kuwataja kwa kupiga kura wezi,majambazi;wauza unga;wauji wa Albimo; na kadhalika!! Nilisema njia wanayotumia haitazaa matunda na huo ndio ukweli wenyewe kama hapatakuwa na''KANGAROO COURT '' KUWATAJA TU bila kuwa na ushahidi ni kupotezeana muda tu na matokeo ndiyo haya!

Hakuna aliyesema Mengi ni msafi kwani hata yeye mwenyewe hajasema hivyo! Hiyo hadithi ya NBC kila mtu anaijua na ni ufisadi huo huo wa waswahili ambao Mengi anachelea kuwataja na nimesema hilo (rejea michango yangu kwenye thread hii) kwani wajamaa wa NBC waliwalipa wahindi waliotengeneza mitambao mibovu through an LC opened by IPP Holdings bila ya kupata certificate ya IPP na ndio maana ilikula kwa NBC!! Mkapa alipopata tamaa na Yona wakawapa makaburu ile Benki bure nadhani hadithi iliishia hapo!

Sijui kama kesi iliendelea kwani NBC chini ya ABSA walipofanya interbank reconcilliation walijikuta wamepata asubuhi over USD 30m kwa hiyo hawakuwa na haja ya kufuatilia madeni mengine mengi tu including hilo la IPP!

Tuje kwa marehemu Nyerere RIP why don't you let him rest in peace. Hata kama alikuwa babu yako I don't know fact ni kwamba hata yeye hakuwa msafi!! Kukataa ufadhili wa Mengi na kukubali kujengewa kule Butiama ama na Jeshi ,serikali au the presida from Msumbiji(Chisanno) it makes no difference kwa nini hakujenga mwenyewe!!

We are to blame him for many shortfalls including doctoring CCM na haswa alipompigia Mkapa kampeni nchi nzima na CCM new he was sick with a fragile health hawakumshauri cause in his days he never trusted any body including his family hakuwajali!! Mind you charity begins at home!!! Actually he fathered mafisadi na aliwapendelea akina Mbowe!!,Alnoor Kassum,,Jamal,,the Rupias!!! the sykes!!! hata the Chavdas!!! akina Mwapachu the list is long;akina somaiya !!Aliwapendelea people for apparent reasons hata akina JMK walipotoka CUBA there ino secret!!!!

Kwa hiyo wewe kuwa kibaraka wa mafisadi it doesn't make any breaking news!! Hicho kiliio unachosema si alificha maradhi mwenyewe na kilio kikamumbua pale National Stadium!!!

By the way hiyo ni historia fupi tu!! Back to the thread !! Serikali iache kigugumizi cha nani msafi au mchafu wakamatwe wote like wahat SOKOINE did itapeleka ujumbe kwamba Tanzania is not a safe harbour kwa mafisadi period!! Kataa kubali hata kama alikosoe marehemu Sokoine RIP but it worked japo akina Msuya na mafisadi by then walimkosovo!!!!!
 
Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora

Ndg wanahabari,
Waheshimiwa ndugu waandishi tunashukuru sana kwa kujitokeza siku ya leo kuja kutusikiliza, tunaomba muendelee na moyo huo kutumikia jamii kwa kutoa habari za uhakika zenye tija na taifa letu.Mungu awabariki sana kwa hilo.

Tungependa kwanza kutumia fursa hii kuwapa pole wakazi wa Jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala na Maeneo yote kwa Ujumla kwa tukio la jana la milipuko ya mabomu, na kuwapa pole majeruhi wote walioathirika na tukio hilo, na pia kuwapa pole familia zote waliofiwa na ndg zao kutokana na tukio hilo, mungu azilaze pema peponi roho zao, na tunawaombea majeruhi wapone haraka.

Tuliopo hapa mbele yenu ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa, Mjumbe wa Baraza kuu Taifa na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa wa tabora, maana yake wilaya ya tabora mjini, Nzega, Sikonge, Igunga, Urambo,na Uyui. Pia tunaye katibu wa Uhamasishaji Uvccm wa Mkoa wa Tabora. Tumekuja hapa Dar-es-Salaam tangu juzi kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya fundraising kwa ajili ya miradi ya vijana wa mkoa wa Tabora, na tunaomba tuwahakikishie vijana wenzetu kwamba mipango inaendelea vizuri sana, na inshaalah mungu akijalia, maandalizi yatakuwa yamekamilika wakati tunarejea Tabora.

Aidha tumeamua kuongelea kauli ya Mfanyabiashara wa IPP, Ndugu Reginald Mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake, ni kauli ambazo hazivumiliki kwa mtu aliyestaarabika kutuhumu watu kwa maslahi binafsi na anyoyafahamu mwenyewe bila kufata misingi ya sheria.

Kauli hizo licha ya kuleta harufu ya ubaguzi wa rangi pia inakuza chuki ya raia dhidi ya wenzao kwa mtazamo kuwa umasikini wao unakuzwa na kundi la watu kwa manufaa yao. Aidha linatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kiwango cha kuwaruhusu baadhi ya watu kuharibu nchi, jambo ambalo lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wake.

Bila kujali utawala wa sheria na haki ya msingi ya binadamu, tunaamini kila mtanzania anayo haki sawa kabisa. Tunapenda kuishukuru na kuipongeza sana Serikali kupitia Waziri wa Utawala Bora na Waziri wa Habari kwa kukemea kitendo hicho na kuendelea kusisitiza Taifa lenye utawala wa Sheria.

Kilichotusukuma sisi leo kama Vijana wa CCM wa mkoa wa Tabora ni jinsi ambavyo Ndugu Mengi alimtaja mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM - Mhe Rostam Aziz, ambaye vilevile ni Mbunge wa Igunga. Wadhifa nyigine ambazo amewahi kushika ni pamoja na Mweka Hazina wa CCM Taifa, pia kwa sasa ni Mjumbe wa NEC kupitia mkoa wetu wa Tabora na Kamanda wa UVCCM wilaya ya Igunga, maana yake ni KADA kwelikweli wa CCM na nyumbani kwao ni Mkoa wa Tabora, tukaona hili haliwezi kupita bila sisi kama vijana kuja kutetea Chama chetu. Kazi kubwa ya Umoja wa Vijana ni kutetea uhai wa CCM na Viongozi wake pale tunapo amini kuwa wanasimamia maslahi ya Taifa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.

Ndg wanahabari, baada ya utangulizi hapo juu, sisi kama viongozi wa UVCCM wa wilaya zote na mkoa wa Tabora na kwa niaba ya UVCCM (M) Tabora, tunaomba kusema yafuatayo:

1. Tunalaani kauli kuwa Mh Rostam Aziz, kama kiongozi wetu na kamanda wa Umoja wa Vijana wilaya ya Igunga kudhalilishwa hadharani na mtu bila kuleta ushahidi wowote, tunamtaka Mzee Reginald Mengi atuombe radhi wana CCM wa mkoa wa tabora kwa kumtuhumu kiongozi wetu ambaye wananchi wake wana imani naye sanjali na wana Tabora, na amechaguliwa kidemokrasia na wananchi wengi tu. Tukiacha kauli yake bila kukemea maana yake tumekubaliana, jambo ambalo siyo kweli na kazi zake katika mkoa wa Tabora na wilaya ya igunga ni ushahidi tosha.

2. Tunalaani matamshi ya Ndugu Reginald Mengi dhidi ya Raia wenzake, na tunahoji nafasi ya ndugu Mengi kwenye jamii mpaka achukuwe nafasi ya kutuhumu, kuchunguza na kuhukumu. Raia yoyote wa Tanzania mwenye nia njema anaruhusiwa kisheria kupeleka ushahidi au kushitaki na kufungua kesi dhidi ya yeyote anayehujumu Taifa, kama kweli anayosema kwanini asiende mahakamani kuwafungulia kesi watu hawa na kuishtaki kwa maslahi ya Nchi. Tunaomba serikali kama ambavyo Mhe Mkuchika amesema, kuchunguza kauli za Ndugu Mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.

3. Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM? Na kwanini anatumia majukwaa ya CCM kutukana viongozi kama anavyojisikia,na kutamka kuwa wateule wa Rais ni wezi. Ndugu Mengi anayo historia ya kulumbana tena kwa kashfa na Mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakuna nae kwenye majukwaa ya kisiasa

4. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye nchi, mgawanyiko na serikali iweze kupiga marufuku tabia hii ya Bwana Mengi kutumia umaskini wa watanzania kupandikizia chuki watu wengine.

5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na Ziara za Ndugu Mengi akiwa na Msafara wa Wabunge huku akitoa Misaada Mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya Mkoa wa Tabora, Uvccm Mkoa wa Tabora inatoa Angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa Chama, tunamuonya kama vijana wa Tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa Tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.

6. UVCCM tunamuunga mkono MNEC wa Mkoa wa Tabora Mh Rostam Aziz(Mb) na kuwaambia Watanzania kuwa Mkoa wa Tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya Uzalendo wake kwa Taifa hili tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka , na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu. Tunathamini sana mchango wake wa muda mrefu kwa Chama Cha Mapinduzi na maendeleo anayohangaika nao kwa wananchi wa jimbo la igunga na mkoa wa tabora kwa ujumla.

7. Uvccm Mkoa wa Tabora, tunatoa angalizo kwa watanzania wenzetu kuwa Tusiruhusu UKABURU kutuingia kwa mtu kuja na hoja ya UBAGUZI ili kuwajengea chuki Watanzania . Tabia hii Baba wa Taifa aliwahi kuikemea na kuifananisha na ukaburu tusiruhusu makaburu kuibuka katika nchi yetu.

8. Uvccm mkoa wa Tabora, tunakemea na tunashauri Chama Cha Mapinduzi kuchukua hatua kurudisha nidhamu ndani ya chama na Serikali kwani CCM ndiyo chama tegemeo. Kwani hivi sasa kuna kashfa, malumbano ambayo hayasaidii nchi na kutoruhusu mijadala ambayo itatuyumbisha kama taifa, tabia ya aina hii si jambo zuri bali ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.

9. Mwisho tunapenda kuwahakikishia wanahabari na watanzania kwa ujumla Uvccm mkoa wa tabora tunamuunga mkono MNEC wetu na hatuko tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa ushahidi wa jambo lolote na imani serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa Gharama za kuchafua wengine.

10. Uvccm Mkoa tunatoa angalizo kwa Wabunge wa Majimbo yote ya mkoa wa Tabora ,na wa viti maalum kuwa wakasimamie utekelezaji wa Ilani ya CCM kama walivyoahidi kwa wapiga kura, pia tunatoa wito kwa wabunge wa Mkoa wetu wanaoambatana na Misafara ya Bwana Mengi wajiepushe na misafara inayokashifu na kuita majina mabaya viongozi wetu na wao kuwa sehemu ya jambo hilo wakishangilia. Kwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ana Tabia ya kutumia majukwaa ya CCM na kukashifu watendaji wakuu wa serikali na wakati huo huo kumsifia Rais kwani huwezi kumsifia Rais wakati unakashifu na kuwaita watendaji wake wa chama na Serikali kuwa ni Mafisadi na hawamsaidii Rais kimantiki ni kwamba anakosoa uteuzi wa Rais na kuonyesha kuwa unamapungufu. Vijana hatutakuwa tayari kubeba wabunge 2010 wanaoshiriki katika ziara ambazo zinakichafua chama na serekali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge.

11. Tunasisitiza tunalaani kauli ya Mengi na tunaomba serekali itekeleze alichosema Mh Mkuchika.

AHSANTENI SANA, MUNGU AWABARIKI

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Bunch of suckers and losers. Walikuwa wapi wakati Rostam anatafuna EPA through Kagoda? Mbona hawakuja kusema chochote back then? Ni kina nani hawa? I bet Rostam ndio kawalipia ticket, i think there is one way kuondoa mtandao wa Rostam. Na ni kwakutumia......... (i will mention it next time)

Yaani wanasound kama wanafunzi wa darasa la nne shule ya Msingi Uhuru Wasichana. Rostam Kada, sijui nini.... Kada my behind
 
Makubwa haya, hapa ndo patamu,

Sasa wanao bisha kwamba CCM si Chama Cha Mafisadi waje hapa na waseme!

Kwahiyo CCM ndo mdomo wa kutetea mafisadi? Ama kweli Taifa limetekwa nyara!
 
Ninyi watu acheni matusi, sasa mlitegemea viongozi watukanwe huku waliowachagua wanyamaze tu kimya, acheni wamtetee kiongozi wao maana wao ndio wanaojua siri ya kumchagua. Mengi alipaswa alitambue hilo kuwa rostam pia ni sehemu ya watanzania hao masikini anaodai kuwatetea .

Cha muhimu ni facts na ziende mahala mahsusi ili zifanyiwe kazi kwa manufaa ya umma.

Mengi angeanza na wauaji wa albino , atutajie hao jamaa nadhani itakuwa relief kubwa ndugu zetu, bado hawana chombo kama pccb wanavyopambana na rushwa
 
Vibwengo nao wako uwanjani Dar. Kutetea wezi !!!

Mwambieni mkuu wenu arudishe fedha za Watanzania alizoiba.

Mfadhili wenu Rostam ndiye aliandaa hotuba mliyopewa kuisoma, ili awape nauli ya kurudi kwenu Urambo?
 
Kazi kweli kweli, UvCCM tabora inahoji mengi ni nani ndani ya CCM!!! Hapa wana Tabora hawataki kukumbushwa ma ya Kagoda. Lakini kinachotakiwa hapa ni facts sio kupiga longolongo tu.
 
Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora

Ndg wanahabari,
Waheshimiwa ndugu waandishi tunashukuru sana kwa kujitokeza siku ya leo kuja kutusikiliza, tunaomba muendelee na moyo huo kutumikia jamii kwa kutoa habari za uhakika zenye tija na taifa letu.Mungu awabariki sana kwa hilo.

Tungependa kwanza kutumia fursa hii kuwapa pole wakazi wa Jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala na Maeneo yote kwa Ujumla kwa tukio la jana la milipuko ya mabomu, na kuwapa pole majeruhi wote walioathirika na tukio hilo, na pia kuwapa pole familia zote waliofiwa na ndg zao kutokana na tukio hilo, mungu azilaze pema peponi roho zao, na tunawaombea majeruhi wapone haraka.

Tuliopo hapa mbele yenu ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa, Mjumbe wa Baraza kuu Taifa na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa wa tabora, maana yake wilaya ya tabora mjini, Nzega, Sikonge, Igunga, Urambo,na Uyui. Pia tunaye katibu wa Uhamasishaji Uvccm wa Mkoa wa Tabora. Tumekuja hapa Dar-es-Salaam tangu juzi kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya fundraising kwa ajili ya miradi ya vijana wa mkoa wa Tabora, na tunaomba tuwahakikishie vijana wenzetu kwamba mipango inaendelea vizuri sana, na inshaalah mungu akijalia, maandalizi yatakuwa yamekamilika wakati tunarejea Tabora.

Aidha tumeamua kuongelea kauli ya Mfanyabiashara wa IPP, Ndugu Reginald Mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake, ni kauli ambazo hazivumiliki kwa mtu aliyestaarabika kutuhumu watu kwa maslahi binafsi na anyoyafahamu mwenyewe bila kufata misingi ya sheria.

Kauli hizo licha ya kuleta harufu ya ubaguzi wa rangi pia inakuza chuki ya raia dhidi ya wenzao kwa mtazamo kuwa umasikini wao unakuzwa na kundi la watu kwa manufaa yao. Aidha linatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kiwango cha kuwaruhusu baadhi ya watu kuharibu nchi, jambo ambalo lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wake.

Bila kujali utawala wa sheria na haki ya msingi ya binadamu, tunaamini kila mtanzania anayo haki sawa kabisa. Tunapenda kuishukuru na kuipongeza sana Serikali kupitia Waziri wa Utawala Bora na Waziri wa Habari kwa kukemea kitendo hicho na kuendelea kusisitiza Taifa lenye utawala wa Sheria.

Kilichotusukuma sisi leo kama Vijana wa CCM wa mkoa wa Tabora ni jinsi ambavyo Ndugu Mengi alimtaja mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM - Mhe Rostam Aziz, ambaye vilevile ni Mbunge wa Igunga. Wadhifa nyigine ambazo amewahi kushika ni pamoja na Mweka Hazina wa CCM Taifa, pia kwa sasa ni Mjumbe wa NEC kupitia mkoa wetu wa Tabora na Kamanda wa UVCCM wilaya ya Igunga, maana yake ni KADA kwelikweli wa CCM na nyumbani kwao ni Mkoa wa Tabora, tukaona hili haliwezi kupita bila sisi kama vijana kuja kutetea Chama chetu. Kazi kubwa ya Umoja wa Vijana ni kutetea uhai wa CCM na Viongozi wake pale tunapo amini kuwa wanasimamia maslahi ya Taifa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.

Ndg wanahabari, baada ya utangulizi hapo juu, sisi kama viongozi wa UVCCM wa wilaya zote na mkoa wa Tabora na kwa niaba ya UVCCM (M) Tabora, tunaomba kusema yafuatayo:

1. Tunalaani kauli kuwa Mh Rostam Aziz, kama kiongozi wetu na kamanda wa Umoja wa Vijana wilaya ya Igunga kudhalilishwa hadharani na mtu bila kuleta ushahidi wowote, tunamtaka Mzee Reginald Mengi atuombe radhi wana CCM wa mkoa wa tabora kwa kumtuhumu kiongozi wetu ambaye wananchi wake wana imani naye sanjali na wana Tabora, na amechaguliwa kidemokrasia na wananchi wengi tu. Tukiacha kauli yake bila kukemea maana yake tumekubaliana, jambo ambalo siyo kweli na kazi zake katika mkoa wa Tabora na wilaya ya igunga ni ushahidi tosha.

2. Tunalaani matamshi ya Ndugu Reginald Mengi dhidi ya Raia wenzake, na tunahoji nafasi ya ndugu Mengi kwenye jamii mpaka achukuwe nafasi ya kutuhumu, kuchunguza na kuhukumu. Raia yoyote wa Tanzania mwenye nia njema anaruhusiwa kisheria kupeleka ushahidi au kushitaki na kufungua kesi dhidi ya yeyote anayehujumu Taifa, kama kweli anayosema kwanini asiende mahakamani kuwafungulia kesi watu hawa na kuishtaki kwa maslahi ya Nchi. Tunaomba serikali kama ambavyo Mhe Mkuchika amesema, kuchunguza kauli za Ndugu Mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.

3. Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM? Na kwanini anatumia majukwaa ya CCM kutukana viongozi kama anavyojisikia,na kutamka kuwa wateule wa Rais ni wezi. Ndugu Mengi anayo historia ya kulumbana tena kwa kashfa na Mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakuna nae kwenye majukwaa ya kisiasa

4. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye nchi, mgawanyiko na serikali iweze kupiga marufuku tabia hii ya Bwana Mengi kutumia umaskini wa watanzania kupandikizia chuki watu wengine.

5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na Ziara za Ndugu Mengi akiwa na Msafara wa Wabunge huku akitoa Misaada Mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya Mkoa wa Tabora, Uvccm Mkoa wa Tabora inatoa Angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa Chama, tunamuonya kama vijana wa Tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa Tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.

6. UVCCM tunamuunga mkono MNEC wa Mkoa wa Tabora Mh Rostam Aziz(Mb) na kuwaambia Watanzania kuwa Mkoa wa Tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya Uzalendo wake kwa Taifa hili tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka , na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu. Tunathamini sana mchango wake wa muda mrefu kwa Chama Cha Mapinduzi na maendeleo anayohangaika nao kwa wananchi wa jimbo la igunga na mkoa wa tabora kwa ujumla.

7. Uvccm Mkoa wa Tabora, tunatoa angalizo kwa watanzania wenzetu kuwa Tusiruhusu UKABURU kutuingia kwa mtu kuja na hoja ya UBAGUZI ili kuwajengea chuki Watanzania . Tabia hii Baba wa Taifa aliwahi kuikemea na kuifananisha na ukaburu tusiruhusu makaburu kuibuka katika nchi yetu.

8. Uvccm mkoa wa Tabora, tunakemea na tunashauri Chama Cha Mapinduzi kuchukua hatua kurudisha nidhamu ndani ya chama na Serikali kwani CCM ndiyo chama tegemeo. Kwani hivi sasa kuna kashfa, malumbano ambayo hayasaidii nchi na kutoruhusu mijadala ambayo itatuyumbisha kama taifa, tabia ya aina hii si jambo zuri bali ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.

9. Mwisho tunapenda kuwahakikishia wanahabari na watanzania kwa ujumla Uvccm mkoa wa tabora tunamuunga mkono MNEC wetu na hatuko tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa ushahidi wa jambo lolote na imani serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa Gharama za kuchafua wengine.

10. Uvccm Mkoa tunatoa angalizo kwa Wabunge wa Majimbo yote ya mkoa wa Tabora ,na wa viti maalum kuwa wakasimamie utekelezaji wa Ilani ya CCM kama walivyoahidi kwa wapiga kura, pia tunatoa wito kwa wabunge wa Mkoa wetu wanaoambatana na Misafara ya Bwana Mengi wajiepushe na misafara inayokashifu na kuita majina mabaya viongozi wetu na wao kuwa sehemu ya jambo hilo wakishangilia. Kwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ana Tabia ya kutumia majukwaa ya CCM na kukashifu watendaji wakuu wa serikali na wakati huo huo kumsifia Rais kwani huwezi kumsifia Rais wakati unakashifu na kuwaita watendaji wake wa chama na Serikali kuwa ni Mafisadi na hawamsaidii Rais kimantiki ni kwamba anakosoa uteuzi wa Rais na kuonyesha kuwa unamapungufu. Vijana hatutakuwa tayari kubeba wabunge 2010 wanaoshiriki katika ziara ambazo zinakichafua chama na serekali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge.

11. Tunasisitiza tunalaani kauli ya Mengi na tunaomba serekali itekeleze alichosema Mh Mkuchika.

AHSANTENI SANA, MUNGU AWABARIKI

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

- Nonsense, kwani maneno ya Kitine yana tofauti gani na haya ya Mengi mbona hawakumlilia Kitine?

FMES
 
Nadhani mnaweza kunifahamisha maana nimesoma katika tamko hapo juu kuwa Mengi anafanya ziara na wabunge kwenye majimbo,
je hizo ziara anazifanya na wabunge gani, wa CCM au na wa vyama vingine pia?
Je, ni nini hasa madhumuni ya ziara hizo?
Je, ni ziara za kisiasa?
 
- Kufanya ziara na wabunge sio crime against our law of the land, isipokuwa ufisadi ni uhalifu kisheria, hata mimi niko mbioni kusaifiri na wabunge what is wrong with that?

- Labda ungetuambia tu kwamba hao wabunge anaosafiri nao ni mafisadi au?

FMES
 
6. UVCCM tunamuunga mkono MNEC wa Mkoa wa Tabora Mh Rostam Aziz(Mb)

Ni dhahili wafanye hivyo as he engineered wizi in the 2005 elections which they benefited as well!

na kuwaambia Watanzania kuwa Mkoa wa Tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya Uzalendo wake kwa Taifa hili

Hii imani ni katika kufanikisha wizi na mauchafu yao au nini?

tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka

Hawa jamaa wako serous kweli? Do they know what they are saying?

na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu.

Ama kweli maajabu, mwenye mali kukimbizwa na mwizi........!
 
- Kufanya ziara na wabunge sio crime against our law of the land, isipokuwa ufisadi ni uhalifu kisheria, hata mimi niko mbioni kusaifiri na wabunge what is wrong with that?

- Labda ungetuambia tu kwamba hao wabunge anaosafiri nao ni mafisadi au?

FMES

You have gone too far, kwangu mimi hii nimeona ni kitu kipya I just want to know.

Kwahiyo kwa yule anayefahamu please naomba kujua kupitia maswali yangu hapo juu. I believe si kila mtu anajua kila kitu.
 
Mh!. La kuvunda halina ubani. Mimi naungana na Mengi Rostam ni fisadi. Nakumbuka sana tangu anagombea Ubunge pale kwetu Igunga.

Hawa vijana (UVCCM Tabora) wana mlinda "mfadhili" wao hawajui huo ufadhili ndio ni vijisenti vyao wenyewe?!

Naona uongo ndani yao, sidhani km ubunge wa RA umevinufaisha vijiji km Mbutu, Itumba, Mwanzugi, Mradi wa umwagiliaji wa Mwamapuli, baada UNDP kuondoka mradi chali!

Tutafika tu,
 
Ninyi watu acheni matusi, sasa mlitegemea viongozi watukanwe huku waliowachagua wanyamaze tu kimya, acheni wamtetee kiongozi wao maana wao ndio wanaojua siri ya kumchagua. Mengi alipaswa alitambue hilo kuwa rostam pia ni sehemu ya watanzania hao masikini anaodai kuwatetea .

Cha muhimu ni facts na ziende mahala mahsusi ili zifanyiwe kazi kwa manufaa ya umma.

Mengi angeanza na wauaji wa albino , atutajie hao jamaa nadhani itakuwa relief kubwa ndugu zetu, bado hawana chombo kama pccb wanavyopambana na rushwa

POLE SANA FDR.Jr;

NANI KAMTUKANA KIONGOZI WENU??? MANJI, NI KIONGOZI WENU? PATEL NI KIONGOZI WENU? AAAGGGHHHRR====

KATIKA PRESS YA MENGI Ulimisikia akisema kwamba Rostam sio jamii ya watanzania?

kuhusu facts kwemnda sehemu sahihi --- HIYO IDEA mazee

Hayo ya Mengi kuanza na mauaji ya Albino usimpangie aseme nini!!!! Mbona na wewe una haki ya kuchagua pa kuanzia!! YEYE AMEKUNA ANAPOJIWEZA, NA KWASABABU YA DATA ZAKE AMEONGEA ALIYOONGEA, KUHUSU KUSEMA KWAMBA MAALBINO HAWANA CHOMBO KAMA PCCB NI KUJITUSI MWENYEWE, JUKUMU ZIMA NI LA JAMII NA POSILI NA VYOMBO VINGINE HUSIKA USIPOTOSHE WATU---- MAADILI NDIYO MABAYA NA KILA MTU ANA WAJIBU NA USIMPANGIE MENGI ASEME NINI

DUH, HII KALI AISEE
 
I cant believe.. yaani hawa UVCCM wanasema eti Mengi anachochea ubaguzi wa rangi? what the hell? kweli UVCCM wako brain washed..manji na RA amewaandikia hiyo speech ? Kama ni wao wenyewe wameandika then dah kweli UVCCM is full of Bunch of suckers and losers. Mtu gani kweli mwenye akili timamu na anayejua history ya tanzania na watanzania atasema hivyo? how many asians-Tanzanians wanafanya biashara tanzania, wanaishi tanzania na wameajiriwa tanzania? alafu how many of them wametajwa kama mafisadi!

masikini vijana wa CCM mnatumiwa bila kujijua na mkiendele kuwa a Bunch of suckers and losers kunasiku hawa mafisadi wataanza kuwatumia vibaya zaidi..

ushauri wangu run away as quick as possible money isn't everything. Dirty politics inaishia kubaya siku zote, na hamna free lunch vijana chungeni kama mnatafuta umaarufu au liziki angalieni sehemu nyingine sio kwenye mambo yausio right and freedom of milions of vulnerable people. na kama nyie ni really politicians then you are being wasted by these mafisadi tafuteni chama kingine
 
Njaa kitu kibaya sana. Adui yako muombee njaa ili umshinde. Ndo kitu walicholipiwa kuja kukifanya Dar hicho? Mkae na amani na kamanda wenu RA.Ameni
 
Nadhani mnaweza kunifahamisha maana nimesoma katika tamko hapo juu kuwa Mengi anafanya ziara na wabunge kwenye majimbo,
je hizo ziara anazifanya na wabunge gani, wa CCM au na wa vyama vingine pia?
Je, ni nini hasa madhumuni ya ziara hizo?
Je, ni ziara za kisiasa?

Sijui ni ziara za aina gani ila inaweza zikawa ni za community/Charity work
(kusaidia jamii). Watu wengi Famous especial in developed countries wanafanyaga hivyo. Ila siko sure if this is the same!!
 
Ninyi watu acheni matusi, sasa mlitegemea viongozi watukanwe huku waliowachagua wanyamaze tu kimya, acheni wamtetee kiongozi wao maana wao ndio wanaojua siri ya kumchagua. Mengi alipaswa alitambue hilo kuwa rostam pia ni sehemu ya watanzania hao masikini anaodai kuwatetea .

Cha muhimu ni facts na ziende mahala mahsusi ili zifanyiwe kazi kwa manufaa ya umma.

Mengi angeanza na wauaji wa albino , atutajie hao jamaa nadhani itakuwa relief kubwa ndugu zetu, bado hawana chombo kama pccb wanavyopambana na rushwa

dah mshikaji ( kama vijiweni washemavyo) unachemsha.. nani amemtukana kiongozi wa CCM? kumshutumu ni mwizi? sikujua hilo ni tusi? sasa tuambie UVCCM kusema kwamba mengi anachochoa ubagunzi wa rangi walikuwa na maana gani? mengi amesema kitu chochote kuhusu rangi za hao mafisadi au wamesema mafisadi regardless of their skin colour?

waambie vijana wako watulie watanzania wameamka na hawalali they should now wake up as well
 
Back
Top Bottom